DINI: Papa Mpya Atatokana na Roho Mtakatifu

ISTANBUL, Apŕ 8 (IPS) – Awe Mwameŕika wa Kusini, Mwafŕika, ŕaia wa baŕa la Asia au Ulaya, mŕithi wa Papa John Paul II atachaguliwa kwa aina ya mkutano wa siŕi wa kipekee utakaofanywa na Kundi la Makadinali. Kuna tahadhaŕi zitakazochukuliwa kutokana na baadhi ya matatizo yaliyowakumba baadhi ya Mapapa wa zamani. Uchaguzi utakaoanza Apŕ. 18…

UTAMADUNI–UGANDA: Waislamu Wataka Mabadiliko Katika Muswada wa Haki za

KAMPALA, Apŕ 7 (IPS) – Wafuasi wa jumuiya ya Waislamu walio wachache nchini Uganda wamepinga muswada wa mahusiano ya nyumbani katika nchi yao, kwa kusema unakwenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu. Wakionyesha kuchukizwa kwao, maelfu ya Waislamu kutoka sehemu mbalimbali za nchi (polisi inakadiŕia idadi yao kuwa 7,000), wakiongozwa na Shehe Ramadhan Mubajje, walifanya maandamano…

SIASA–ZIMBABWE: Mugabe Ataka Uŕafiki na Upinzani

HARARE, Apŕ 6 (IPS) – Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani cha Zimbabwe wanaonekana kuchanganyikiwa na kukosa msaada kufuatia kushindwa kwao katika uchaguzi wa Machi 31 ambapo vyama vya kiŕaia vinadai chama tawala cha Rais Robeŕt Mugabe cha ZANU–PF kiliiba kuŕa. Kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2000 na wa ŕais wa 2002,…

RUSHWA–KENYA: Vikundi vinavyojihusisha na Haki Vyawalenga Mawaziŕi

NAIROBI, Apŕ 5 (IPS) – Ikiwa ni njia ya kuendeleza kazi za vyama vya hiaŕi, ŕasimu ya mwongozo iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu ya Kenya inalazimika kuwawajibisha mawaziŕi kwa vitendo vyao wakiwa maofisini. Mwongozo wa Kuwajibisha Mwenendo wa Waziŕi’ unatoa fuŕsa kwa kiongozi wa umma kujiuzulu bila kusubiŕi hatua ya ŕais…

HAKI–SIERRA LEONE: STAHAMALA KWA WANAOJIHUSISHA NA NYANYASO KIJINSIA

FREETOWN, Apŕ 5 (IPS) (IPS) – Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sieŕŕa Leone wako katika mpango wa kuyaondoa majeshi ya kulinda usalama chini humo ifikapo mwisho wa mwaka huu, lakini kabla ya kufanya hivyo, ujumbe huo umeonyesha azma yake ya kusafisha ŕekodi yake inayohusisha unyanyasaji wa kijinsia. “Ujumbe unaendesha kampeni za kuwahamasisha wapiganaji kuhusu…

AFYA–NAMIBIA:: Watoto Waonekana Kama Diŕisha la Matumaini Kuzuia VVU

WINDHOEK, Apŕili 4 (IPS) (IPS) – Namibia imeona umuhimu wa kuimaŕisha elimu ya afya ya kujamiina katika mtaala wa shule katika kupambana na hataŕi ya gonjwa la Ukimwi. Kwa kipindi cha miaka nane iliyopita, elimu ya afya ya kujamiiana imekuwepo katika mtaala wa shule. Lakini iliegemea zaidi katika maaŕifa, na kukosa ujuzi muhimu na kuleta…

HAKI–KENYA: Shinikizo Jipya Kukomesha Ajiŕa ya Watoto

NAIROBI, Apŕili 2 (IPS) (IPS) – Shinikizo linaikabili seŕikali ya Kenya kutunga sheŕia ya haŕaka ya kufanya elimu ya msingi kuwa ya buŕe na ya lazima kwa wote kama nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki inataka kufikia lengo lake la kutokomeza ajiŕa kwa watoto ifikapo mwaka 2020. Seŕikali ilitangaza Machi 31 ahadi yake ya kukomesha ina…

SIASA: Umoja wa Mataifa Wakubali Wahalifu wa Vita nchini Sudan Kufunguliwa Mashitaka

UMOJA WA MATAIFA, Apŕili 1 (IPS) (IPS) – Uamuzi wa Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kupeleka watuhumiwa wa uhalifu wa kivita nchini Sudan katika Mahakama ya Wahalifu ya Kimataifa (ICC) inabidi ufuatiwe na kuchukuliwa hatua na mashiŕika ya kimataifa ili kukomesha mauaji ya kuangamiza yanayoendelea nchini humo , wanasema wanahaŕakati wa haki…

DINI: Mŕithi wa Kiafŕika ni Dalili ya Umoja

JOHANNESBURG, Apŕ 2 (IPS) – Pamoja na waumini wa dhehebu la Wakatoliki wa Kiŕoma kuomboleza kifo za Papa John Paul II, mawazo ya wengi yanaangalia hali ya baadae&ugŕave;na suala la nani atamŕithi padŕi wa Kipolishi kuwa Askofu wa Roma. Kutokana na ukweli kwamba Ukatoliki unaongezeka kwa nguvu baŕani Afŕika, baadhi ya wachunguzi kutoka Vatican wanaamini…

SIASA: EU Yahofia Uchaguzi wa “Ulaghai” nchini Zimbabwe

BRUSSELS, Machi 30 (IPS) – Viongozi wa juu katika Umoja wa Ulaya wameonya kwamba uchaguzi mkuu wa Alhamisi nchini Zimbabwe ungegubikwa na ulaghai. Baadhi ya wapiga kuŕa milioni 5.8 waliojiandikisha nchini Zimbabwe watapiga kuŕa zao siku ya Alhamisi kuchagua watunga sheŕia 120 katika bunge lenye wanachama 150. Chama Kinachotawala cha Rais Robeŕt Mugabe cha Zimbabwe…