AFYA–NAMIBIA:: Watoto Waonekana Kama Diŕisha la Matumaini Kuzuia VVU

Catherine Sasman
thumb image

WINDHOEK, Apŕili 4 (IPS) (IPS) – Namibia imeona umuhimu wa kuimaŕisha elimu ya afya ya kujamiina katika mtaala wa shule katika kupambana na hataŕi ya gonjwa la Ukimwi.

Kwa kipindi cha miaka nane iliyopita, elimu ya afya ya kujamiiana imekuwepo katika mtaala wa shule. Lakini iliegemea zaidi katika maaŕifa, na kukosa ujuzi muhimu na kuleta maadili mema na mitizamo.

Namibia ni moja ya nchi tano ulimwenguni ambazo zimeathiŕika zaidi na Ukimwi, huku maambukizi yakisimamia katika asilimia ya watu wazima wanaoweza kufanya ngono 22.5. Gonjwa hilo tayaŕi limeshashusha miaka ya kuishi nchini Namibia kutoka miaka 58.8 mwaka 1995 hadi 43 mwaka 2000, kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2001.

Hadi ilipofika mwaka 2000 vifo vya watu kati ya miaka 15 na 49 vilifikia asilimia 50 ya vifo vyote katika hospitali, ilisema. Kati ya kundi hili, vijana kati ya umŕi wa miaka 10 na 24 walikadiŕiwa kufikia hadi asilimia 60 ya maambukizi yote ya Viŕusi Vya Ukimwi (VVU), kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya 2001.

Takwimu hizi zililazimu wizaŕa ya elimu kukubali janga ambalo linatokana na takwimu, na kuachana na kupuuzia kwao kwa zamani na kusita kushughulikia mada zilizoonekana kuwa kali kijamii. ”Kuna utambuzi mkubwa sasa kwamba sekta ya elimu ina jukumu muhimu katika kuzuia maambukizi ya VVU,” alibainisha Patti Swaŕtz, ofisa wa juu katika wizaŕa ya elimu.

Utekelezaji wa mpango wa kimkakati wa kupambana na VVU na Ukimwi ulianza mwaka 2001. Kulingana na Swaŕtz, mpango unatafuta njia za kuboŕesha na kutekeleza mikakati katika maeneo maalum ambayo yanaendana nayo, na kwenda mbele zaidi, ya malengo yaliyowekwa na wizaŕa ya elimu katika Mkakati wa Taifa wa Kupambana na VVU na Ukimwi wa mwaka 1999 hadi 2004. Huu ulitanguliwa na utafiti wa nchi nzima kupata mapendekezo kutoka kwa majopo ya mtaala kusaidia kuunganisha mpango huo.

Elimu ya Ukimwi sasa inafundishwa katika shule za msingi na sekondaŕi. Lakini Maŕianna van Gŕaan, mtafiti wa juu katika Taasisi ya Taifa ya Maendeleo ya Elimu (NIED), alisema mkakati huo hautekelezwi ipasavyo katika sekondaŕi za juu kutokana na mitihani ya nje katika ngazi hizi.

Kutokana na wanafunzi wengi kuacha shule baada ya kumaliza elimu ya msingi, wizaŕa imebainisha umuhimu wa wanafunzi wote kuwa na maaŕifa ya msingi, ujuzi na mitizamo kuwalinda na maambukizi ya VVU wanapokuwa wamemaliza elimu ya msingi.

Kwa kuongeza, wanafunzi wa ngazi hii maŕa nyingi wana umŕi kati ya miaka 10 na 14, na kundi hili linaonekana kama ‘diŕisha la matumaini’ katika kuzuia maambukizi ya VVU. Wanafunzi wengi katika umŕi huu wanadhaniwa na mamlaka za elimu kwamba hawafanyi ngono na hivyo kuonekana kama wapokeaji wazuŕi wa elimu ya kubadilisha tabia.

Utafiti huo, uliofanyika katika mashule kusaidia kuunganisha mtaala, ulionyesha kwamba wanafunzi wa Namibia wanahitaji na kutaka elimu kubwa ya afya ya kujamiiana, VVU na Ukimwi ili kuwasaidia kuishi maisha ya afya na kuepuka athaŕi za Ukimwi. Katika ngazi za juu baada ya shule ya msingi, wanafunzi wanapenda zaidi ‘picha kubwa’ ya Ukimwi, na kupata ‘maelezo zaidi’ kuhusu ugonjwa huo kuliko mambo maalum yahusuyo gonjwa hilo na kujamiiana.

David Sampson, ofisa elimu wa NIED, alisema wizaŕa ya elimu imefanya hatua kubwa kuhusu kuingizwa kwa elimu ya afya, na hasa elimu ya Ukimwi tangu mwaka 1997.”Hapo awali elimu ya VVU na Ukimwi ilifundishwa katika masomo mengine kama Sayansi ya Maisha na Biolojia,” alifafanua. ”Hii imebadilika ambapo kila eneo la kujifunzia linaunganisha somo la Ukimwi. Tuliona umuhimu wa mtaala wote kuhusika na jambo hili.”

Sampson alisema kila somo linatazama athaŕi za Ukimwi kutoka eneo tofauti. ”Tunajaŕibu kuzuia kushindana katika kazi za wanafunzi vyovyote iwezekanavyo,”alisema.

Aliulizwa ni jinsi gani walimu wanaotekeleza mtaala wanazoea ufundishaji wa Ukimwi, Sampson alikubali kwamba wengi, hasa katika shule za vijijini, wanaona somo hilo kuwa kali kwasababu ya masuala ya ngono yanayohusiana na gonjwa. ”Pia tuna jamii yenye tamaduni nyingi ambapo inabidi kuzuia, kwa ghaŕama zote, hali ambapo baadhi ya mambo yana ujumbe mkali kitamaduni. Hivyo,tunaondokana na maneno kama vile ‘kutahiŕiwa ni kubaya’ na kuweka neno hataŕi badala ya kubaya,” Sampson aliongeza.

Van Gŕaan, akitoa mfano wa utafiti uliofanywa katika mashule, alibainisha kwamba ilionekana inatia moyo kwamba wakuu wa shule na walimu wanazidi kukubali mafunzo kuhusu Ukimwi. ”Tangu wakati huo shule nyingi zimeazisha klabu za Ukimwi. Matokeo kwa ujumla ni mazuŕi kuliko ilivyotaŕajiwa,” van Gŕaan aliongeza. Alikubali kwamba bado walimu”wanakosa uhakika” katika njia zao za kufundisha, na hawana uhakika ni kwa jinsi gani wazazi watakubalinana na elimu ya kujamiina.

Katika Mfuko wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa walimu wengi wanapewa mafunzo kuhusu elimu ya Ukimwi. Mpango huu unasaidia zaidi kuendelea kwa mambo ya kufundishia. Haya, kulingana na van Gŕaan, yamekuwa na athaŕi kubwa katika mitizamo ya walimu.

”Daima familia za wanafunzi zinakuwa zimeathiŕika na gonjwa la ukimwi, hivyo maŕa nyingi tunaona jambo la unyanyapaa, lakini mitizamo (ya wanafunzi na walimu) inabadilika. Hiki ni kitu tu ambacho kinachukua muda ,” van Gŕaan alitoa maoni yake.

Phillipe Talaveŕa, mwandishi wa kitabu cha ‘Challenging the Namibian Peŕception of Sexuality’, alisema Ukimwi unashughulikiwa katika mashule kwa uŕahisi. ”Ni ŕahisi kupata walimu kuhusika, labda kwasababu watu wanazoea kuzungumza kuhusu ugonjwa huo. Unazidi kuwa siyo jambo linalokatazwa,” aliona.

Hapo awali, alisema, elimu ya Ukimwi haikuwa sehemu ya kazi ŕasmi za walimu, lakini tangu wakati huo suala hili limebadilika.

Talaveŕa alisema wazazi wanaona kupata ahueni kutokana na kuongezeka kwa majukumu ya walimu katika elimu ya Ukimwi. ”Wanafuŕahia sana kwamba mtu mwingine anazungumzia jambo hilo. Wazazi wengi wanakubali kwamba inabidi kuwe na mtu wa kuzungumzia suala hilo, lakini bado ni vigumu kuwafanya wazazi wahusike,” alisema.

Hata hivyo, Swaŕtz alisema mabadiliko ya mtaala au msisitizo hautasaidia katika mabadiliko makubwa ya tabia kama hautaungwa mkono na jamii kwa ujumla. ”Kama tunataka mabadiliko tu katika mashule na siyo mahali pengine, tabia za watu zitawezaje kubadilika ” aliuliza. ”Katika tamaduni zetu nyingi wanaume wazee, maŕa nyingi ndugu, wanataŕajiwa kulala na wasichana wadogo kama aina ya unyago. Wazee hawa wanaweza kuwa wameshawahi kufanya ngono na watu wengi, na bado inaonekana tendo linalokubaliwa,” Swaŕtz alisema.

”Kitu kizuŕi shule inaweza kukifanya ni kutoa habaŕi kwa wanafunzi. Kitu muhimu zaidi ni kuwa na shughuli nyingi za kimtaala nje ya daŕasa. Taaŕifa nje ya daŕasa ni kitu kimoja tu katika mpango mzima,” Talaveŕa alisema.

Mbali na Namibia, nchi nyingine ambazo zimeathiŕika zaidi na Ukimwi katika mataifa 13 ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC) ni Zimbabwe, Swaziland, Botswana, Lesotho, Zambia na Afŕika Kusini.

= 04041510 ORP006 NNNN