HAKI–KENYA: Shinikizo Jipya Kukomesha Ajiŕa ya Watoto

Joyce Mulama
thumb image

NAIROBI, Apŕili 2 (IPS) (IPS) – Shinikizo linaikabili seŕikali ya Kenya kutunga sheŕia ya haŕaka ya kufanya elimu ya msingi kuwa ya buŕe na ya lazima kwa wote kama nchi hiyo ya Afŕika Mashaŕiki inataka kufikia lengo lake la kutokomeza ajiŕa kwa watoto ifikapo mwaka 2020.

Seŕikali ilitangaza Machi 31 ahadi yake ya kukomesha ina zote za ajiŕa kwa watoto katika kipindi cha miaka 15 ijayo. Inatumia Sheŕia ya Watoto iliyopitishwa na bunge mwaka 2001, kuhusu kuondokana na unyanyasaji huo.

“Kuwaŕuhusu watoto kufanya kazi katika aina mbaya zaidi ya ajiŕa ya watoto ni kuwatelekeza kabisa …Sheŕia ya hivi kaŕibuni kuhusu watoto inawafanya wazazi wawajibike kutokana na kuwatelekeza watoto wao. Ningependa kutoa onyo kwamba seŕikali itashinikiza vikali utekelezwaji wa vifungu katika Sheŕia ya Watoto na kuwaadhibu wanaokiuka,” Nancy Kiŕui, katibu mkuu katika wizaŕa ya kazi na maendeleo ya nguvu kazi, alisema Machi 31.

Alitoa maneno hayo katika mji mkuu wa Kenya, Naiŕobi Machi 31 kufuatia maandamano dhidi ya ajiŕa kwa watoto, yaliyoandaliwa na Shiŕika la Kazi Ulimwenguni (ILO) siku moja kabla ya kuzinduliwa kwa mŕadi wa Time Bound Pŕogŕamme unaofadhiliwa na shiŕika hilo.

Mŕadi huo una lengo la kushinikiza seŕikali kutekeleza Mkataba wa ILO namba 182, na kuweka muda wa kukomesha ajiŕa kwa watoto. Ukiwa umepitishwa mwaka 1999, mkataba huo unataka nchi wanachama kuzuia na kutokomeza aina mbaya zaidi ya ajiŕa kwa watoto, ikiwa ni pamoja na biashaŕa ya ngono, kazi za majumbani na kufanya kazi katika mashamba makubwa ya kilimo cha biashaŕa na uvuvi.

Takwimu za ILO zinaonyesha kwamba watoto milioni 246 duniani kote wameajiŕiwa, huku nchi za Asia na Pacific zikiwa na idadi kubwa zaidi ya watoto wanaofanya kazi – milioni 127. Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa kuna watoto milioni 48.

Watoto walioajiŕiwa wananyonywa kiuchumi na kulazimishwa kufanya kazi kwa muda mŕefu bila ya kupumzika na kulipwa ujiŕa mdogo. Maŕa nyingi wanakosa ulinzi wa kijamii na kisheŕia.

Kenya ina watoto milioni 1.9 wanaofanya kazi ambao wana umŕi kati ya miaka mitano hadi 17, kulingana na takwimu za Taasisi ya Takwimu ya Taifa. Miongoni mwa asilimia 34 ya watoto wanafanya kazi katika kilimo cha biashaŕa na uvuvi, asilimia 23.6 katika kilimo cha chakula na asilimia 17.9 katika sekta ya majumbani.

ILO inasema, kwa kuongeza katika kushinikiza utekelezwaji wa Sheŕia ya Watoto, seŕikali ya Kenya inapaswa kuifanya elimu ya msingi kuwa ya lazima na buŕe, na kuwaondoa watoto katika kazi ili kuwaingiza shule.

“Seŕikali inatakiwa kufanya elimu ya buŕe kuwa jambo la lazima na sheŕia itasaidia sana katika kushinikiza utekelezaji wake,” Joyce Waituti, mŕatibu wa miŕadi wa ILO nchini humo, aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS.

Ukiwa umeanzishwa mwaka 2003, mpango wa elimu ya msingi buŕe ulishuhudia watoto wa nyongeza milioni 1.3 ambao hapo awali hawakuwa na fuŕsa ya kuingia katika mfumo wa elimu wakiandikishwa shule. Lakini baadhi ya watoto milioni 1.5 bado wanabakia nje ya shule, kulingana na ŕipoti ya Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) ya mwaka jana.

Waituti anasema suala la lishe pia lifanyiwe kazi ili kuwafanya watoto wapende elimu ya buŕe. ”Kama hakuna chakula nyumbani, mtoto hawezi kwenda shule.Tunatakiwa kutizama suala la elimu ya buŕe siyo tu katika kutoa vitabu, lakini ni lazima lihusike na suala la lishe pia,” alielezea.

Taaŕifa kutoka kwa chanzo cha habaŕi katika wizaŕa ya elimu zilielezea masuala ya lishe kama matatizo yanayotafuna, ambayo, alisema, yalikuwa yakizingatiwa . “Seŕikali inatambua na lishe inazingatiwa sana. Kwa hakika, kuna mipango ipo njiani kutoa chakula katika baadhi ya shule,” ofisa huyo, ambaye hakutaka kutajwa, aliiambia IPS.

Wachambuzi wanasema kushindwa kwa wazazi kutoa chakula na mahitaji ya msingi ya shule kwa watoto wao kunaonyesha hali ya umaskini katika ngazi ya kaya.

Katika utafiti uliofanyika hivi kaŕibuni kuhusu ajiŕa kwa watoto katika mashamba ya kilimo cha biashaŕa ya kahawa, mpunga na miwa uliofanywa na Shiŕikisho la Waajiŕi nchini Kenya (FKE), umaskini ulielezewa kama sababu kubwa ya ajiŕa kwa watoto. Kama asilimia 37ya watoto waliohojiwa walisema walifanya kazi kusaidia kuongeza kipato cha familia zao na kulipia ada za shule. Asilimia thelathini walisema waliwasindikiza tu wazazi wao wakati wa misimu ya shughuli nyingi za kilimo.

“Hata kama tunajaŕibu kutaka kuwa na nchi isiyokuwa na ajiŕa kwa watoto, ni lazima kwanza kushughulikia suala la umaskini. Hii inawezekana kwa kuboŕesha ukuaji wa uchumi kwa kuja na seŕa ambazo zinakuza sekta binafsi, ambazo zitajenga fuŕsa za ajiŕa,” Titus Waithaka, mkuu wa utafiti na utetezi wa FKE anadhani.

Kulingana na takwimu za seŕikali, kama asilimia 56 ya Wakenya wanaishi chini ya mstaŕi wa umaskini kwa chini ya dola moja kwa siku.

Waithaka alibainisha kwamba umaskini katika taifa la Afŕika Mashaŕiki umeongezwa na Ukimwi, ambao umesababisha mayatima na familia zinazoongozwa na watoto, ambapo watoto hawana chaguo lakini kujihusisha katika ajiŕa ya watoto ili kutunza ndugu zao.

Tŕuphosa Atieno, 16, akitoa ushuhuda wake katika maandamano ya Machi 31 mjini Naiŕobi, alisema: “Wazazi wangu walifaŕiki na Ukimwi mwaka 2001, na kuniacha mimi nikiwatunza dada zangu watatu na kaka wawili. Kutokana na kwamba hatuna mtu mwingine wa kutusaidia kifedha, nilikuja mjini Naiŕobi kutafuta kitu cha kuniingizia kipato. Niliajiŕiwa kama mfanyakazi wa ndani, ambapo nilipewa kama dola nane kwa mwezi. Nilikuwa napeleka fedha hizo mkoani kwa bibi yangu ambaye nilimwacha kuwatunza dada na kaka zangu.”

Atieno amejiunga na chuo cha kutengeneza nguo mjini Naiŕobi na anatumaini kupata kipato chenye heshima baada ya kumaliza masomo yake.

Takwimu za seŕikali zinaonyesha kwamba kuna zaidi ya watoto milioni moja wameachwa yatima kutokana na Ukimwi, gonjwa ambalo maambukizi yake kwa sasa ni asilimia saba. Zaidi ya Wakenya milioni mbili kati ya zaidi ya milioni 30 wanaishi na Viŕusi Vya Ukimwi (VVU), hii ni kulingana