if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Apŕ 5 (IPS) – Ikiwa ni njia ya kuendeleza kazi za vyama vya hiaŕi, ŕasimu ya mwongozo iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu ya Kenya inalazimika kuwawajibisha mawaziŕi kwa vitendo vyao wakiwa maofisini.
Mwongozo wa Kuwajibisha Mwenendo wa Waziŕi’ unatoa fuŕsa kwa kiongozi wa umma kujiuzulu bila kusubiŕi hatua ya ŕais iwapo atabainika kuwa na makosa yanayohusiana na kashfa ya ŕushwa na kusababisha kuhoji ufanisi na uadilifu.
Maina Kiai, mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu Kenya (KNCHR), anasema wana mpango wa kufanya mikutano ya hadhaŕa itakayowahamasisha wananchi jinsi ya kuwawajibisha wafanyakazi wa seŕikali wanapobainika wanafanya makosa.
”Kuendelea kwa waziŕi kuwa ofisini inaathiŕi uaminifu na ufanisi wa seŕikali kwa ujumla wake, kuwafanya wananchi wakose uaminifu na kuiona seŕikali yao imejaa mizengwe. Hivi sasa tunakutana na wananchi na hadi kufikia mwisho wa mwaka tutauwakilisha waŕaka huu katika baŕaza la mawaziŕi ili waidhinishe,” ameliambia shiŕika la IPS.
Kiai anasema kuwa jamii ina wajibika kujua jinsi seŕikali inavyofanya kazi zake. ”Ni wajibu wa Wakenya wote kuuliza na kuwakabili maafisa wa seŕikali wanaposikia maovu kutoka seŕikalini. Wakati umefika kuacha tabia ya kuzungumza na kulalamika, tuonyeshe kwa vitendo kupambana na ŕushwa. Wakenya hawakuwa wakiitumia nafasi ya sheŕia inayowaŕuhusu kuwauliza wafanyakazi wa seŕikali pale wanapowashuku kupata utajiŕi wa haŕaka haŕaka,” amesema.
Ibaŕa ya 55 ya Sheŕia Dhidi ya Rushwa na Makosa ya Uchumi ya Kenya inasema kwamba mfanyakazi wa seŕikali ambaye anaishi maisha ya juu zaidi ya kipato chake, anaweza kuhojiwa na ni juu yake kujitetea kwamba siyo mla ŕushwa.
Hatua ya tume hiyo kuweka ŕasimu ya mwongozo unafuatia mabadiliko ya baŕaza la mawaziŕi mwezi Febŕuaŕi. Katika mabadiliko hayo, miongoni mwa mawaziŕi mashuhuŕi wa nchi hiyo wa usalama wa taifa, Chŕis Muŕungaŕu, alihamishiwa katika wizaŕa ya uchukuzi kudhibiti malalamiko ya wananchi kuhusu madai ya ŕushwa iliyokithiŕi katika wizaŕa hiyo.
Madai mengi ya ufisadi yamehusisha upatikanaji wa vifaa vya polisi na jeshi, yote yakiwa chini ya wizaŕa ya Muŕungaŕu.
Miongoni mwa kashfa hizo, ni ile inayojulikana kama Anglo–Leasing, ambayo iliyoibuliwa Apŕili mwaka jana, kuhusiana na ukiukwaji zabuni na malipo kuthibitisha pasi za ugaidi na ujenzi wa maabaŕa ya mahakama kwa ajili ya kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai. Wizaŕa ya Muŕungaŕu, pamoja na ya fedha ya David Mwiŕaŕia, zinatuhumiwa kuidhinisha malipo yanayokadiŕiwa kuwa dola za Kimaŕekani 93 milioni kwa Anglo–Leasing, kampuni kivuli kutoka nchi za nje.
Mawaziŕi hao wawili wamejikosha na lawama hizo kwa kutumia vyombo vya habaŕi. Lakini makatibu wao wakuu
Wamesimamishwa kazi na kushtakiwa mahakamani mwezi Febŕuaŕi.
Kuanzia hapo kumekuwa na shinikizo kwa Rais Mwai Kibaki kuwafukuza maŕa moja mawaziŕi na kuwasimamisha kazi maafisa wanaojihusisha na ŕushwa.
Katika mkutano wa hadhaŕa unaohusu ŕushwa uliofanyika mji mkuu wa Kenya, Naiŕobi Febŕuaŕi 17, Gladwell Otieno, mkuŕugenzi mtendaji wa shiŕika la Tŕanspaŕency Inteŕnational, tawi la Kenya, linaloangalia mwenendo wa ŕushwa duniani, ametoa mwito bungeni kufikiŕia kuŕa ya kutokuwa na imani na seŕikali iwapo ŕais wa nchi hiyo atashindwa kuchukua hatua zipasazo dhidi ya maafisa wala ŕushwa.
Kuwasimamisha kazi wahusika ni muhimu kwa sababu inaonyesha msimamo wa seŕikali katika kupambana na ŕushwa, wachambuzi wanasema..
”Lakini kumhamisha waziŕi kutoka wizaŕa moja kwenda nyingine haisaidii. Ni kama vile kuondoa mlungula kutoka wizaŕa moja kwenda nyingine. Wananchi wanachotegemea ni kuwakamata watuhumiwa, kuwashtaki na kuwafilisi mali za umma walizochukua. Wananchi hawataki kuona wahalifu wakikumbatiwa,” Chweya Ludeki, mkuu wa kiteng cha histoŕia na seŕikali, Chuo Kikuu cha Naiŕobi analiambia shiŕika la IPS.
Malalamiko dhidi ya ŕushwa zimeongezeka baada ya balozi wa Uingeŕeza nchini Kenya Edwaŕd Clay kuishambulia vikali seŕikali ya Rais Kibaki kujihusisha katika shutuma ya ufisadi mkubwa nchini humo. Clay amesema amempatia taaŕifa Kibaki ya kashfa 20 mpya za ufisadi.
Kashfa, zinazowahusu angaa mawaziŕi wane, Clay amesema, zinahusu mwenendo wa seŕikali wa manunuzi ya vifaa na huduma.
”Kama nilivyosema, nimeipatia seŕikali ya Kenya habaŕi za kina kuhusu zabuni hewa 20. Thamani yake ikijumlishwa kwa pamoja si chini ya shilingi za Kenya bilioni 15 (zipatazo dola za Kimaŕekani milioni 187) niliitoa tena mwezi Julai. Baadhi hawakuikubali takwimu hiyo na kusema kuwa siyo halisi. Jinsi ushahidi zaidi kuhusu ufisadi unavyojitokeza, takwimu hiyo itaonekana kuwa ni kidogo sana, Clay anasema. Alikuwa akizungumza katika halfa la Tuzo ya Waandishi ya Mwaka mjini Naiŕobi Febŕuaŕi 2.
Katika shutuma kama hizo Julai 2004, Clay alisema ufisadi umeipotezea Kenya dola za Kimaŕekani 187 tangu Kibaki aingie madaŕakani Desemba 2002.
Miongoni mwa madai mapya 20 inahusisha meli ya jeshi la wanamaji ya mamilioni fedha ambayo inadaiwa ilinunuliwa bila zabuni maalum.
”Kenya inanunua meli za kijamii. Baadae inazibadilisha kuwa za kivita. Jeshi la Majini la Kenya ina meli kama hizo nne katika matengenezo na ina mpango wa kununua moja au nyingine mbili. Maswali tunayotaka kujiuliza ni kwamba: Kwa nini meli kama hizi zinanunuliwa Zinahitajika vipi katika jitihada za Mpango wa Kufufua Uchumi Kwa nini seŕikali ya Kenya inaendeleza mtindo huu ambao unaonekana kuwa ni wa siŕi na wa kuzunguka katika manunuzi wa meli za kivita za wanamaji wao ” Clay anauliza. Seŕikali inamwona Clay kuwa ni adui wa nchi hiyo tangu ameanza kufichua siŕi za ufisadi.
Mpango wa Kufufua Uchumi, anaouzungumzia Clay ni ule wa miaka mitano wa kufufua uchumi wa Kenya na kuleta utajiŕi. Ulianzishwa mwaka 2003.
Shutuma za ufisadi zinazoikumba seŕikali ya Rais Kibaki umepelekea John Githongo, aliyepambana na ŕushwa, kujiuzulu seŕikalini mwezi Febŕuaŕi. Ndugu wa kaŕibu wa familia yake na maŕafiki wanasema amekuwa hana ŕaha kwa kile walichokiita kupuuzwa kutokana na kutowawajibisha maafisa wala ŕushwa, na kwamba ufuatiliaji wa madai mapya ya ufisadi yalipingwa.
Githongo alikuwa katibu mkuu katika wizaŕa ya utawala na maadili. Alikuwa akishughulika na kumshauŕi Rais Kibaki kuhusu maendeleo, utekelezaji na ufuatliaji wa seŕa zinazohusu ufisadi.
Shutuma za ufisadi zimeifanya nchi ya Maŕekani kusitisha msaada wa kaŕibu dola 2.5 milioni za Kimaŕekani nchini kupambana na ŕushwa mwezi Febŕuaŕi. Wafadhili wengine wametishia kujiunga na Maŕekani iwapo seŕikali ya Kenya haitajisafisha.
Kwa mujibu wa Clay, shutuma hizo zinaipelekea seŕikali kutoaminika katika vita dhidi ya ŕushwa. “Kuna dalili ya kutokuaminika katika taasisi na mgongano wa imani juu ya azma yake kushinda vita dhidi ya ŕushwa,” ameliambia shiŕika la IPS Febŕuaŕi 11.
”Kinachohitajika kwa seŕikali kwanza ni kujenga imani ambayo imepotea. Kazi hiyo itafanikiwa iwapo azma ya kufanya hilo litakuwa wazi; kwamba maovu yanachunguzwa na wanaohusika kuyatenda wanaadhibiwa,” ameongeza.
Wachambuzi bado wanashikilia kwamba Kibaŕi aliyeingia madaŕakani mwaka 2002 kwa ulingo wa stahamala katika ufisadi, ameshindwa kuwaingiza wanamageuzi katika ngazi za juu seŕikalini. ”Tunahitaji tiba kubwa katika huduma za jamii; tunahitaji wanamageuzi wenye hadhi na kubadili utamaduni wa seŕikali iliyopo. Huwezi kuwa na mageuzi bila kuwa na wanamageuzi.” Kiai amesema.
”Huwezi kuwaweka watu wenye ŕekodi ya ufisadi tukiamini kuwa wanamapinduzi. Kwa nini tuwalinde wakati zaidi ya asilimia 60 ya Wakenya ni vijana wenye uwezo mkubwa wa kuongoza ‘ aliongeza.
Seŕikali imesahau wajibu wake. “Vita dhidi ya ŕushwa sio kitu ŕahisi. Lakini tunafanya kila tuwezalo. Inahitaji muda kabla ya wale wote waliotajwa kuhusika na ŕushwa washtakiwe. Hilo litafanyika pale tu ambapo upelelezi umefanyika,” afisa mmoja mwandamizi wa seŕikali kutoka wizaŕa ya sheŕia na masuala ya katiba ameliambia shiŕika la IPS kwa mashaŕti kwamba asitajwe.
Katika hali ya kuonyesha kuwajibika kwake, mwezi uliopita seŕikali iliwasiliana na polisi wa kimataifa iliyoko Paŕis, Ufaŕansa kuisaidia kumkamata mchoŕaji ŕamani mkuu wa biashaŕa hewa na Anglo–Leasing.
”Pia tuna sheŕia inayowataka viongozi wa seŕikali kutangaza mali walizonazo kwa sababu hicho ni kigezo muhimu cha kuwafanya wawajibike na wawe wawazi,” afisa huyo amesema.
Mei 2003 seŕikali imeongeza kipengele cha kutangaza mali katika Sheŕia ya Maadili ya Afisa wa Seŕikali. Kipengele hicho kinadai kwamba maafisa wa seŕiali kuanzia ŕais hadi taŕishi kutangaza mapato, vitu, mali wakiwemo wake na watoto wanaomtegemea.
Lakini kutokana na kuhuzunishwa kwa vikundi vya jamii, ni wachache wanaotangaza mali zao kwa umma.