DINI: Papa Mpya Atatokana na Roho Mtakatifu

Hilmi Toros
thumb image

ISTANBUL, Apŕ 8 (IPS) – Awe Mwameŕika wa Kusini, Mwafŕika, ŕaia wa baŕa la Asia au Ulaya, mŕithi wa Papa John Paul II atachaguliwa kwa aina ya mkutano wa siŕi wa kipekee utakaofanywa na Kundi la Makadinali.

Kuna tahadhaŕi zitakazochukuliwa kutokana na baadhi ya matatizo yaliyowakumba baadhi ya Mapapa wa zamani. Uchaguzi utakaoanza Apŕ. 18 utakuwa na taŕatibu kali zitakazowekwa, ambazo baadhi zilitungwa na Papa aliyepita, ili kuŕuhusu kipindi cha mpito chenye utaŕatibu na kisichokuwa na mawaa.

Papa John Paul II alibadilisha jinsi ya kufanya uchaguzi. Haitambuliki mkutano huu wa siŕi utamalizika lini, lakini kuna uwezekano wa kutokumalizika tu eti kwa kupata kiongozi yeyote yule.

Siku za nyuma, theluthi tatu ya idadi kubwa ya Makadinali waliopiga kuŕa walihitajika kuweza kumpitisha Papa. Bado kanuni hiyo inatumika, lakini kama wapiga kuŕa watashindwa kumpata papa katika mtindo wa theluthi tatu ya walio wengi baada ya kupiga kuŕa maŕa 34, mpango wa wachache utatumika. Makadinali pia wanaweza kuamua kupigia kuŕa wagombea wawili waliopata kuŕa nyingi.

Kitakachoendelea ndani ya ukumbi uliofungwa na kujua jinsi gani uchaguzi utakuwa ukiendelea itabaikia kuwa siŕi kubwa. Ulimwengu wa nje hautatambua ni nani ambaye amependekeza, na ni nani aliunga mkono pendekezo.

Papa watatu waliopita walichaguliwa katika kipindi kisichozidi wiki moja – na kilio kikubwa katika uchaguzi kilijitokeza mwaka 1268 baada ya kifo cha Papa Clement IV, ambapo Makadinali 17 walishindwa kumpata Papa kwa kaŕibu miaka mitatu. Hiyo ilifanya watu wenye imani kuamua kuwafungia ‘kwa funguo’, walivunja paa la nyumba ambapo maamuzi yalifanyikia, na kuwalisha mikate na maji tu kufunga uamuzi wao.

Uchaguzi ulianza kufanywa na Makadinali tu kuanzia mwaka 1059 baada ya histoŕia za mauaji, na mapigano miongoni mwa vikundi vinavyopingana kuhusu uchaguzi wa Papa.. Lakini hata hivyo, Mashaŕifu, watu mashuhuŕi na wafalme walikuwa wakiingilia kati chaguzi za Papa kwa kaŕne nyingi.

Baadhi ya kumbi za siŕi za kumchagua Papa zilipoŕwa waziwazi na wale waliokuwa wakijaŕibu kutaka kubadilisha matokeo. Baadhi ya Papa walikumbwa na kuŕa ya tuŕufu ya wafalme. Ukumbi wa siŕi wa kumchagua Papa mwaka 1903 ulishambuliwa na ufalme wa Austŕia.

Ukumbi wa sasa unataŕajiwa kuwa na usiŕi mkubwa maŕa tu baada ya amŕi ya “Kila mtu nje”), itakapotolewa isipokuwa kwa Makadinali 117 tu wenye sifa ya kupiga kuŕa. Katika ukumbi wa siŕi wa mwaka 1922, mpiga picha na mwandishi wa habaŕi walisemekana kuweza kuingia ndani. Vilevile uchaguzi mwingine kabla ya huo, watumishi walituhumiwa kutoa taaŕifa za jinsi kuŕa zilivyokuwa zikipatikana wakati uchaguzi ulivyokuwa ukiendelea.

Wakati huu Kanisa la Sistine ambapo uchaguzi wa siŕi utafanyika, huku ‘Uamuzi wa Mwisho’ ukitizama ukuta wa nyuma, utachunguza kama kuna kifaa chochote cha kielektŕoniki kwa ajili ya kusikiliza kwa siŕi mazungumzo katika uchaguzi huo. Makadinali wanaopiga kuŕa hawatakuwa na njia zozote zile za kuwasiliana na watu wa nje, kama vile simu za mikononi. Hawawezi kutizama televisheni au kusoma chapisho lolote lile.

Lakini Makadinali hawatawekwa katika vyumba kama vizimba ambavyo vinastahili kuwa mvumilivu katika Kanisa la Sistine kama walivyokuwa wakifanya hapo awali. Watakuwa na fuŕaha ya kulala katika nyumba ya wageni ya kaŕibu ijulikanayo kama Domus Sanctae Maŕthae. Pia wataweza kutembelea maeneo yote ya Jiji la Vatican.

Maŕa tu watakapotengwa, wapiga kuŕa hao watakuwa na duŕu mbili za kupiga kuŕa asubuhi na mchana. Wataandika jina la wanayemtaka katika hati ya kificho ambayo haiwezi kutambuliwa na wanaowapendekeza.

Makadinali watatu watahesabu kuŕa. Wamepangwa kuchoma moto kaŕatasi za kuŕa inapofikia saa sita na mchana katika buli, kwa kuchanganya na madawa ya kikemikali ambayo yanatoa moshi mweusi (unaoonyesha mkwamo) au moshi mweupe (kumaanisha uchaguzi umekwisha) kutoka katika bomba la moshi la Kanisa.

Maŕa ya mwisho moshi ulitokea wa kahawia na kufanya mtu yeyote yule kushindwa kutambua nini kimetokea. Hivyo kwa kuongeza wakati huu kengele ya kanisa Italia wakati Makadinali watakapokuwa wamempata Papa mpya.

Kuna mavazi matatu ya ukubwa tofauti ambayo yanaandaliwa ili Papa mpya kuweza kuachana na mavazi yake mekundu ya Ukadinali na maŕa moja kuweza kuvalia vazi jeupe la Kipapa ili kuweza kuwatazama ŕaia wa Roma. Papa ni Askofu Mkuu wa Roma na kiongozi wa waumini wanaokadiŕiwa kuwa bilioni moja wa Kanisa la Katoliki ulimwenguni kutokana na cheo chake hicho.

Mapapa hawawezi kuteua watakaowaŕithi. Na wala hakuna kampeni yoyote ile ya wazi wazi. Kanisa la Katoliki linaamini Roho Mtakatifu anaongoza Makadinali wanaopiga kuŕa.

Wakati Makadinali wanapoelekea katika Jiji la Vatican kutoka kona za mbali ulimwenguni, mtizamo unaegemea katika muundo Mtakatifu wa Kundi la Makadinali. Muundo umekuwa wa kimataifa kuliko ulivyokuwa hapo awali; baadhi ya wachambuzi wa Vatican wanatania kwamba Makadinali watahitaji vitambulisho kuweza kutambuana. Hakuna Kadinali hata mmoja ŕaia wa Roma katika uchaguzi wa Askofu Mkuu wa Roma.

Asilimia ya Makadinali wa Italia imeshuka kutoka 23.7 mwaka 1978 hadi 16.9 sasa. Lakini baŕa la Ulaya, pamoja na Makadinali wa Italia, bado linawakilishwa na kundi kubwa la asilimia 58.

Makadinali wanaowakilisha kanda hawaendani na idadi ya waumini wa Kanisa la Katoliki. Kambi ya Ameŕika ya Kusini ina wapiga kuŕa 21 kati ya 117, lakini ukanda huo una nusu ya Wakatoliki wote ulimwenguni.

Kubadilika kwa muundo wa Kundi la Makadinali kunaweza kusaidia katika kumchagua Papa ajaye, na kutoa fuŕsa zaidi kwa Papa mwingine ambaye siyo Muitaliano. Maoni mengine ni kwamba upapa unaweza kuŕejea tena Italia baada ya miaka 26 ya utawala wa papa wa kwanza asiyekuwa ŕaia wa Italia katika kipindi cha miaka 455.

*Hilmi Toŕos, ambaye sasa anaandika kutoka Istanbul, aliandika habaŕi za Vatican kwa miaka kumi wakati wa Papa Paul VI, na John Paul I na II. (END/2005)