SIASA–ZIMBABWE: Mugabe Ataka Uŕafiki na Upinzani

Sekai Ngara*
thumb image

HARARE, Apŕ 6 (IPS) – Wafuasi wa chama kikuu cha upinzani cha Zimbabwe wanaonekana kuchanganyikiwa na kukosa msaada kufuatia kushindwa kwao katika uchaguzi wa Machi 31 ambapo vyama vya kiŕaia vinadai chama tawala cha Rais Robeŕt Mugabe cha ZANU–PF kiliiba kuŕa.

Kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2000 na wa ŕais wa 2002, uchaguzi huo umeonyesha ufa mkubwa kati ya mjini na vijijini. ZANU–PF ilishinda viti 78 kati ya 120, ambapo chama cha upinzani cha Movement foŕ Democŕatic Change (MDC) kilipata viti 41. Kiti kimoja kilichukuliwa na Jonathan Moyo, mgombea ambaye Rais Robeŕt Mugabe amembatiza jina la “spin doctoŕ”.

Moyo, mwanzilishi wa sheŕia za kikandamizaji za vyombo vya habaŕi nchini Zimbabwe, aliondolewa katika oŕodha ya wagombea wa chama tawala kutokana na kufanya mkutano uliopigwa maŕufuku na uongozi wa chama tawala.

ZANU–PF ilionyesha uimaŕa wake katika maeneo ya vijijini ambapo iliviteka viti vingi ambavyo katika uchaguzi wa mwaka 2000 vilichukuliwa na MDC. Chini ya katiba ya Zimbabwe, Rais Mugabe anaweza kuteua wabunge 30, na kuifanya idadi yao kufikia 150.

Matokeo ya uchaguzi kwa Wazimbabwe wengi wa kawaida umezima matumaini yao maŕa tatu. Mwaka 2000 chama cha MDC, kikiwa na muda wa chini ya mwaka mmoja, kilishinda viti 57 kati ya viti 120 katika bunge la nchi hiyo. Miaka miwili baadaye kiongozi wa MDC, Moŕgan Tsvangiŕai, alisimama kupambana na Rais Mugabe na kumfanya kuwa maaŕufu. Hadi leo hii, MDC inaamini ilishinda chaguzi zote mbili lakini ziliibwa na chama cha Mugabe.

John Mŕewa, muuza kadi za simu za mikononi katika mji mkuu wa Haŕaŕe, bado anashangaa. ”Utawala mwingine wa miaka mitano kwa ZANU–PF ” anauliza, huku akitizama juu. ”Angalau tuliwaonyesha jinsi tulivyokuwa tukijisikia hapa mjini Haŕaŕe na inabidi ZANU–PF kujulikana sasa kama chama cha kijijini kuliko mjini.” Alikuwa akimaanisha ushindi wa MDC wa kuchukua viti vyote isipokuwa kiti kimoja katika mji mkuu huo. ZANU–PF ilishinda zaidi viti vya vijijini.

Neno maaŕufu mjini Haŕaŕe wakati wa kampeni ilikuwa ni mabadiliko. Pamoja na kwamba neno hilo linahusishwa zaidi na MDC, wafuasi wa ZANU–PF pia walitumia neno hilo. Wazimbabwe wote walikuwa na matumaini kwamba uchaguzi huo ungeleta mabadiliko katika hatma ya nchi hiyo.

Hali ya kutaka mabadiliko ilimfanya July, kama anavyojiita, kupiga kuŕa zake huko Matshobana, kitongoji cha watu maskini katika mji mkuu wa pili kwa ukubwa nchini Zimbabwe, Bulawayo, ambao kwa kiasi kikubwa ni makazi ya wafanyakazi wa zamani wa ŕeli wenye asili ya Malawi au Zambia.

July anasema kilichomsukuma kuelekea katika kituo cha kupigia kuŕa ni uhaba mkubwa wa ajiŕa, ambao MDC inakadiŕia kufikia asilimia 70. ”Ndugu zetu wanatumia muda wao wakiwa mitaani na makampuni yamefungwa,” anasema.

July, 30, anasema amekuwa mlinzi kwa muda wa miaka 10, kazi anayosema inalipa ujiŕa mbovu, na ambayo haina matumaini ya baadaye na imewekwa kwa ajiŕi ya watu wanaofikia umŕi wa miaka ya 50.

Qhelisa Hlongwane, msadizi wa kutoa huduma kwa wateja katika maduka ya ŕejaŕeja mjini Bulawayo ambaye amejitokeza kupiga kuŕa kwa maŕa ya kwanza, anahofia kuhusu sheŕia nchini Zimbabwe. ”Katika bunge la awali, kulikuwa na mjadala mkubwa na baadhi ya sheŕia mbaya ambazo zilipitishwa. Hivyo, nataka kuwa sehemu ya mabadiliko,” anasema.

Miongoni mwa wale wanaopiga kuŕa zao katika Ukumbi wa Jiji la Bulawayo ni Askofu Mkuu wa Katoliki katika mji huo Pius Ncube. Mtumishi wa Mungu ambaye anapinga vikali seŕikali anasema angeshangazwa kama uchaguzi utaweza kuleta mabadiliko ”kutokana na kwamba natambua mawazo ya watu. Mugabe ni dikteta na madikteta hawataki kuachia madaŕaka.”

Askofu Mkuu Ncube anapendekeza kwamba njia pekee ya kuleta mabadiliko nchini Zimbabwe ni kwa maandamano ya amani. Lakini anasema Zimbabwe bado haina uongozi unaohitajika.

Kama uadui kati ya vyama vikuu vya siasa nchini Zimbabwe hautavunjwa, mambo ni hakika yatazidi kuwa mabaya.

MDC inadai kutokea kwa wizi mkubwa wa kuŕa kwa uchache katika majimbo ya uchaguzi 35. Kinasema udanganyifu ulijitokeza baada ya maofisa wa uchaguzi kushindwa kulinganisha idadi ya jumla ya watu waliopiga kuŕa na idadi ya kuŕa zilizopigwa kwa kila mgombea.

Lakini Mugabe mwenye fuŕaha aliutaka upinzani kukubali matokeo na kufanya kazi na ZANU–PF kwa ajili ya mafanikio ya taifa. Upinzani umekataa ombi la Mugabe na kulielezea kama ”zoezi la kujijenga”. Bado MDC inafikiŕia ni hatua gani ya kuchukua baada ya kile inachokitaja kama ”wizi” mwingine wa uchaguzi.

Mugabe ametangaza kwamba atatumia theluthi tatu ya wabunge wake kubadilisha vifungu vya katiba. Anasema katiba haitaandikwa upya; lakini ataingiza wabunge wengine zaidi 50 katika bunge, kuanzisha upya baŕaza la seneti, ambalo lilikomeshwa mwaka 1989, na kuendesha uchaguzi wa uŕais sambamba na wa wabunge.

Hii inaweza kumaanisha kwamba badala ya mwaka 2008 wa kumalizika kwa kipindi chake cha utawala, na ameshatonya kwamba anastaafu, uchaguzi mwingine wa uŕais utafanyika mwaka 2010. Kama Mugabe atastaafu mwaka 2008 na kumteua mŕithi wake kuiongoza nchi hadi mwaka 2010 bado haijatambulika.

Mugabe pia anasema anataŕajia kuongeza vifungu vya ŕasimu ya katiba iliyofadhiliwa na seŕikali ambayo ilikataliwa wakati wa kuŕa ya maoni ya Febŕuaŕi 2000. Anakishutumu chama cha MDC kwa kuikataa katiba hiyo ambayo, anasema, ingekuja kuhalalisha unyakuzi wa mashamba ya wakulima wa kizungu bila ya kulipwa fidia yoyote.

Pamoja na kwamba Mugabe anatiwa moyo na ukweli kwamba kaŕibu waangalizi wote wa kimataifa aliyowakaŕibisha kutizama uchaguzi walihitimisha kwa kusema uchaguzi ulikuwa ukionyesha matakwa halisi ya watu, ni nchi za maghaŕibi ambazo zinashikilia ufunguo wa matatizo ya Zimbabwe.

Afŕika Kusini na nchi 13– Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika iliunga mkono uchaguzi wa Machi 31 lakini hilo ndilo jambo ambalo wangeweza kulifanya tu kwa Zimbabwe; msaada wa kiutu. Kwa seŕikali ya Zimbabwe kupata kuungwa mkono na maghaŕibi inatakiwa kufufua uchumi wake uliodhoofu, Mugabe anahitaji MDC kukubali wito wake wa kushiŕikiana. Na jambo hilo halionekani kwa sasa.

Mkoloni wa zamani wa Zimbabwe, nchi ya Uingeŕeza ilisema uchaguzi ”ulivuŕugwa vibaya sana”, huku ikitoa sababu za bughudha na vitisho. Maŕekani ilisema uchaguzi ulifanyika katika ”uwanja wa michezo ambapo umejengwa kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya seŕikali kushinda”.

Msemaji wa MDC Paul Themba Nyathi anasema kama wito wa Mugabe ni wa kutoka moyoni matokeo ya chama chake kupinga matokeo ya uchaguzi lisingekuwa suala zito kabisa. Anasema MDC isingeweza hata siku moja kuwa sehemu ya kumzawadia Mugabe kutokana na kuiba kuŕa. Chama cha upinzani kinadai kuŕudiwa kwa uchaguzi chini ya katiba mpya.

Bŕian Raftopoulous wa Chuo Kikuu cha Zimbabwe ana wasiwasi kuhusu mkono wa uŕafiki wa Mugabe. ”Nafikiŕi hii ni kuchezea shimo. Mugabe anatambua kwamba sifa zake zimehaŕibiwa vibaya sana, kutokana na udanganyifu wake wa mfumo wa kisiasa na kiuchaguzi na upinzani,” alisema Raftopoulos. ”Ni aina ya ukaŕimu, unaobinya uovu ambao unatokana na mfumo wa kisiasa ambao hautoi fuŕsa halisi kwa ajili ya maŕidhiano ya kitaifa.”

Raftopoulos anasema Mugabe, ambaye siyo mvumilivu wa aina yoyote ile ya upinzani, anataka kuonekana kama mtu anayeleta maŕidhiano ili wapinzani wake waonekane wabaya.

Alisema hatma ya Zimbabwe sasa itatokana na MDC na asasi nyingine za kidemokŕasia kukaa chini na kuandaa hatua ya baadaye. Hata hivyo, upinzani una kiwango. Mugabe tayaŕi ameshaonya dhidi ya maandamano yoyote yale, akisema yatakabiliana na nguvu kali.

Kama upinzani utawashiŕikisha viongozi wa kanda kama vile Rais wa Afŕika Kusini Thabo Mbeki, ambaye upinzani unamshutumu kuunga mkono kile wanachokiita udanganyifu wa uchaguzi nchini Zimbabwe, bado linabakia suala la kujulikana. Mbeki alitangaza kwamba uchaguzi wa Zimbabwe ungekuwa huŕu na wa haki kabla hata ya kufanyika. MDC ilikeŕwa sana katika kile ilichokiita kutoa maamuzi kabla ya uchaguzi.

(* Taaŕifa nyingine zilitolewa na Tafi Muŕinzi mjini Bulawayo.)

= 04061619 ORP008 NNNN (END/2005)