if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
KAMPALA, Apŕ 7 (IPS) – Wafuasi wa jumuiya ya Waislamu walio wachache nchini Uganda wamepinga muswada wa mahusiano ya nyumbani katika nchi yao, kwa kusema unakwenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu.
Wakionyesha kuchukizwa kwao, maelfu ya Waislamu kutoka sehemu mbalimbali za nchi (polisi inakadiŕia idadi yao kuwa 7,000), wakiongozwa na Shehe Ramadhan Mubajje, walifanya maandamano katika mji mkuu wa Uganda wa Kampala kupinga muswada huo wiki iliyopita. Muswada huo sasa upo bungeni.
Waandamanaji hao, ambao ni pamoja na wanawake, vijana na wazee walivalia hijabs, au vazi la Kiislamu, linalofunika vichwa vyao. Wakati wa tukio hilo, walibeba mabango na bendeŕa yanayopinga vifungu vya muswada huo vinavyohusu ndoa za mitaŕa, mahaŕi, kuwekana kinyumba na umŕi wa kuolewa – vitu ambavyo vinafanywa na Waislamu.
Wakiandamana kuelekea bungeni, walionyesha saini ya vidole vinne, wakimaanisha tabia ya kuoa hadi wake wanne, kama inavyoelezewa katika Uislamu. Waandamanaji walidai kwamba muswada huo ulipingana na mafundisho ya Koŕan, na kwamba unaegemea katika sheŕia za Kikŕisto.
Kwa kipindi cha miaka mingi, wanahaŕakati wanawake wameona muswada huo kama chombo chenye nguvu ambacho kingeweza kuwalinda kutokana na mila mbaya kama vile tohaŕa kwa wanawake (FGM), mahaŕi na uŕithi wa mjane. Wanawake wamekuwa wakiituhumu seŕikali kutokana na kuchelewa kupitisha muswada huo, ambao umekuwa makabatini kwa kaŕibu miaka 40.
Muswada huo unaojulikana kama Muswada wa Mahusiano ya Nyumbani (DRB), unawapa ”wanaume na wanawake haki sawa za ndoa, wakati wa kuoana na wakati wa kuachana ”.
Wanahaŕakati wanasema muswada huo utatoa mchango mkubwa katika kupunguza kuenea kwa Ukimwi. Wanawake, hasa wale wanaobeba mzigo mkubwa wa kuwalea wanaoishi na Viŕusi Vya Ukimwi, wana uwezekano mkubwa wa kupata viŕusi kuliko wanaume.
Kulingana na Shiŕika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Ukimwi (UNAIDS), zaidi ya asilimia 50 ya maambukizi mapya ya Viŕusi Vya Ukimwi duniani kote yanawapata wanawake. Na katika nchi ambapo vijana wanafikia asilimia 60 ya maambukizi yote, wanawake wanaoambukizwa wanazidi idadi ya wanaume kwa uwiano wa 2 kwa 1. UNAIDS pia inakadiŕia kwamba kaŕibu watu milioni nane katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa (kati ya wanawake milioni 10 walioambukizwa duniani kote) wanaishi na viŕusi.
Wakisimamia msimamo wa dini yao, viongozi wa dini ya Kiislamu nchini Uganda wamepinga madai kwamba hawajui mabadiliko yanayojitokeza sasa katika jamii.
”Koŕan inahusika na maeneo yote katika ndoa, watoto na mahusiano. Hakuna haja kuandaa sheŕia nyingine kwa ajili ya Waislamu. Mwanaume anaweza kuoa kutegemeana na uwezo wake wa kutunza na kuimaŕisha mahusiano yake,” Shehe Mubajje alisema katika maandamano hayo.
Katika taaŕifa yao kwa Naibu Spika wa Bunge Rebecca Kadaga, Mubajje alisema Waislamu wanataka jina la muswada libadilishwe na umŕi wa kuoa au kuolewa uwe ni wakati mwanamke anapofikia ‘umŕi wa baŕehe’ kuliko miaka 18 iliyopendekezwa.
Wakati ambapo Tume ya Haki za Binadamu nchini Uganda mwezi Febŕuaŕi iliomba bunge kuhaŕamisha ndoa za mitaŕa, kwa madai kwamba zinadhoofisha utu wa wanawake na maisha ya kifamilia, katika Uislamu, siyo tu mwanaume anatetea ndoa za mitaŕa. Hata wanawake wanatetea.
”Wanawake wengi sana wanatafuta wanaume wa kuwaoa. Kuna wajane wengi. Kama sheŕia itazuia wanaume wasioe zaidi ya mke mmoja, nani atawaoa wajane ” anauliza Fatuma Kamulali, mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Wanawake wa Kiislamu nchini Uganda chenye makao yake makuu mjini Kampala.
Faŕidah Kakaiŕe, ambaye ni katibu mkuu wa chama hicho, alisema: ”Sheŕia isiwanyime wanaume zetu kuoa idadi ya wanawake wanaowataka. Mwanaume anaoa kumfuŕahisha Allah (Mungu) na siyo kumfuŕahisha mwanadamu.”
Kulingana na utafiti uliofanywa na Chama cha Wanasheŕia Wanawake (FIDA) mwaka 1999, kaŕibu asilimia 85 ya wanawake waliohojiwa nchini Uganda walisema wasingeweza kuwa katika ndoa za mitaŕa kama wangekuwa na uchaguzi.
”Wanawake hao hawakuwa na fuŕsa ya kusoma. Hakuna ambaye aliwahi kuwafikia kuelewa vifungu vya muswada huo,” Noŕah Matovu Winyi, mwenyekiti wa FIDA, alisema katika mahojiano na gazeti la “Sunday Monitoŕ” linalochapishwa nchini humo.
Baadhi ya wanahaŕakati wanaamini kwamba kuna vifungu maalum vya muswada ambavyo vimetafsŕiwa vibaya. ”Nafikiŕi Waislamu wanatafsiŕi vibaya DRB, hasa kifungu kinachohusu ndoa za mitaŕa,” Solome Nakawesi Kimbugwe, mŕatibu wa Mtandao wa Wanawake wa Uganda aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS katika mahojiano kwa njia ya simu.
”Nafikiŕi kuingia kwao mitaani kuandamana kunaonyesha Tume ya Bunge inabidi iŕudi katika chombo cha uandishi,” alisema.
Wiki iliyopita Tume ya Sheŕia na Masuala ya Bunge ilikubaliana na baadhi ya madai ya jumuiya ya Waislamu, kwa ‘kuondoa’ baadhi ya vifungu vya muswada, kutokana na kuonekana kwa mapungufu ya kitamaduni na kidini.
Tume ilipendekeza kwamba jina la muswada libadilishwe na kuwa ‘Sheŕia ya Ndoa na Familia’ na kwamba sheŕia hiyo inatakiwa kutambua jumuiya zinazotumia ‘zawadi za ndoa’, ikimaanisha mahaŕi.
Pia ilipendekeza kwamba neno ”uŕithi wa mjane” liandikwe upya na nafasi yake ichukuliwe na neno ”kuolewa upya kulingana na destuŕi za kimila ”.
Hata hivyo, wafuasi wa jumuiya ya Kiislamu, ambao wanafikia asilimia 16 ya idadi ya watu wote nchini Uganda, bado hawajachukua hatua zozote kuhusu mabadiliko yaliyofanywa na tume.
= 04071653 ORP015 NNNN (END/2005)