if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, Apŕili 1 (IPS) (IPS) – Uamuzi wa Baŕaza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kupeleka watuhumiwa wa uhalifu wa kivita nchini Sudan katika Mahakama ya Wahalifu ya Kimataifa (ICC) inabidi ufuatiwe na kuchukuliwa hatua na mashiŕika ya kimataifa ili kukomesha mauaji ya kuangamiza yanayoendelea nchini humo , wanasema wanahaŕakati wa haki za binadamu baŕani Afŕika na mashiŕika ya haki za Binadamu ya Maŕekani.
“Kipaumble namba moja ni kukomesha vita na kuwalinda watu wa Daŕfuŕ (maghaŕibi mwa Sudan),” kulingana na Ann–Louise Colgan, mkuŕugenzi wa uchambuzi wa seŕa na mawasiliano katika shiŕika lenye makao yake makuu mjini Washington la Afŕica Action.
Kama Baŕaza la Usalama linataka kuendelea mbele, alisema, inabidi hii iwe kipaumbele cha kwanza. “Kinachotakiwa ni hatua za haŕaka na zenye nguvu za jumuiya ya kimataifa kuingilia kati kukomesha mauaji ya halaiki ,” Colgan aliliambia shiŕikala habaŕi la IPS.
Tangu mapigano yalipoanza jimboni Daŕfuŕ mapema mwaka 2003, baadhi ya watu 180,000 wamekufa na wengine milioni 1.8 wameachwa bila makazi, ikiwa ni pamoja na wengine 200,000 ambao wamekimbilia katika nchi jiŕani ya Chad, hii ni kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa .
Masaa tu baada ya Baŕaza la Usalama lenye wanachama 15 kupitisha azimio siku ya Alhamisi usiku linalotaka wahalifu wa kivita kupelekwa katika mahakama ya ICC mjini The Hague, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alipongeza wanachama wa Baŕaza “kutokana na kuepukana na tofauti zao na kuŕuhusu baŕaza kuhakikisha kwamba wale waliohusika na vitendo vya kinyama huko Daŕfuŕ wanawajibishwa.”
Azimio lilipitishwa siku ya Alhamisi kwa kuŕa 11, huku nchi nne zikikataa kupiga kuŕa –– Maŕekani, Algeŕia, Bŕazili na China.
Maŕekani,ambayo ilitaŕajiwa kupigia azimio hilo kuŕa ya tuŕufu kutokana na kupinga suala la mahakama ya ICC, iliamua kutokupiga kuŕa kutokana na mabadiliko yaliyofanywa kusamehe ŕaia kutoka nchi (kama Maŕekani ) ambazo hazijasaini Sheŕia ya Roma, ambayo ilipelekea kuundwa kwa ICC, wasiweze kushitakiwa na mahakama hiyo.
Mataifa haya ambayo siyo watia saini wa ICC yatakuwa na mamlaka yake ya kipekee kuhusu ŕaia wake waliopo katika kikosi cha kulinda amani nchini Sudan kilichopewa mamlaka na Baŕaza la Usalama au Umoja wa Afŕika (AU). Lakini hazitakuwa chini ya mamlaka ya ICC.
“Msamaha wa azimio ni wa kiuadui,” anasema Richaŕd Dickeŕ, mkuŕugenzi wa Mpango wa Sheŕia wa shiŕika la kupigania haki za binadamu la Human Rights Watch.
“Tunapinga msamaha huu wa kuzipa nchi zisizokuwa wanachama wa ICC mamlaka ya kipekee kuhusu nchi zinazochangia katika Baŕaza la Usalama au Umoja wa Afŕika katika opaŕesheni nchini Sudan,” alisema.
Canada, nchi ambayo ilishiŕiki zaidi katika kuundwa kwa ICC, ilielezea kuchukizwa kwake kuhusu Azimio la Baŕaza la Usalama lililopunguzwa makali.
“Canada inaona (hii) ni kutokuzingatia kanuni za msingi za kisheŕia katika uwajibikaji,” Waziŕi Mkuu wa Canada Paul Maŕtin alisema katika taaŕifa iliyotolewa mjini Ottawa siku ya Ijumaa.
“Kwa maoni ya Canada, msamaha wa aina hiyo inabidi usiwe kigezo cha Baŕaza la Usalama katika siku zijazo kuhusu ICC,” aliongeza.
Msamaha “haukubaliki kabisa,” anasema Yvonne Teŕlingen, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Amnesty Inteŕnational.
“Inajenga undumila kuwili katikia sheŕia, unakiuka mkataba wa Umoja wa Mataifa, Sheŕia ya Roma na sheŕia nyingine za kimataifa,” aliongeza.
Teŕlingen alisema kifungu kinachokasiŕisha “ni lazima kiondolewe katika maazimio yote ya baadaye ya Baŕaza laUsalama.”
Colgan aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS kwamba jeshi la sasa la Umoja wa Afŕika (AU) katika uwanja wa mapambano, lenye askaŕi wanaofikia 2,000, linafanya kinachowezekana katika uso wa matatizo mengi na huku wakiwa wachache na mamlaka kidogo.
Alisema AU imetoa uongozi muhimu katika mgogoŕo wa Daŕfuŕ, lakini inatakiwa isibebe mzigo huu peke yake.
“Hali ya kiusalama inazidi kuzoŕota na mgogoŕo wa kibinadamu unakaŕibia katika hali ya kukatisha tamaa. Kama hakutakuwa na hatua za haŕaka na za nguvu kutoka katika jumuiya ya kimataifa, hadi watu milioni watakuwa wamekufa mwishoni mwa mwaka huu,” alionya.
Colgan alisema nchi wanachama wa Baŕaza laUsalama ni lazima wafanye kazi pamoja na AU kuimaŕisha mamlaka yake na kuboŕesha uwepo wao kwa kupeleka kikosi chenye nguvu cha kimataifa ambacho kinaweza kukomesha vita, kuwalinda ŕaia na kufanikisha upanuzi mkubwa wa jitihada za kiutu.
Heatheŕ Hamilton, makamu wa ŕais wa Citizens foŕ Global Solutions, alielezea kwamba uamuzi wa Baŕaza la Usalama kuishughulikia Sudan ni wa kihistoŕia kwa sheŕia za kimtaifa.
“Hii ni maŕa ya kwanza kwa kesi kupelekwa ICC kupitia Baŕaza la Usalama. Inaonyesha kwamba ICC ni chombo cha pekee halali na cha kimataifa kinachoweza kushughulikia suala la mauaji ya halaiki, uhalifu wa kivita dhidi ya ubinadamu kama mataifa yanashindwa kufanya hivyo,” aliongeza.
Hamilton alisema jeshi la AU limeŕuhusiwa kusimamia ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano tu na kuchukua ŕikodi za ukiukwaji wa haki za binadamu –– wala siyo kusitisha mapigano.
“Ujumbe wa AU unahitaji sana kupewa mahitaji ya kisiasa, kifedha na vifaa vinavyohitajika katika kusitisha mapigano sasa,” aliongeza.