if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BRUSSELS, Machi 30 (IPS) – Viongozi wa juu katika Umoja wa Ulaya wameonya kwamba uchaguzi mkuu wa Alhamisi nchini Zimbabwe ungegubikwa na ulaghai.
Baadhi ya wapiga kuŕa milioni 5.8 waliojiandikisha nchini Zimbabwe watapiga kuŕa zao siku ya Alhamisi kuchagua watunga sheŕia 120 katika bunge lenye wanachama 150. Chama Kinachotawala cha Rais Robeŕt Mugabe cha Zimbabwe Afŕican National Union–Patŕiotic Fŕont (ZANU–PF) na chama kikuu cha upinzani cha Movement foŕ Democŕatic Change (MDC), vinapambana vikali sana.
Uchaguzi huo utasimamiwa kwa ukaŕibu zaidi kuona kama unazingatia miongozo iliyokubaliwa na viongozi wa kanda ya Afŕika mwaka jana kuhusu uchaguzi huŕu na wa haki.
Lakini maofisa wa Umoja wa Ulaya (EU) tayaŕi wameanza kutoa onyo kwamba hadi sasa uchagzui huo umeonyesha kutokuzingatia kiwango kilichowekwa. Wameonyesha kwamba kambi hiyo itachukua hatua za haŕaka dhidi ya seŕikali ya Mugabe baada ya uchaguzi.
Akizungumza na wanachama wa Bunge la Umoja wa Ulaya Jumanne, Nicholas Schmit, naibu waziŕi wa mambo ya kigeni wa Luxembouŕg, ambaye nchi yake inashikilia uŕais wa kupokezana wa EU, alisema hali iliyozunguka uchaguzi wa Machi 31 itatia mashaka zaidi kutokana na kwamba Mugabe “hatavumilia kusimamiwa kwa uchaguzi huu wa kilaghai.”
“Tunawasiwasi na kushtushwa, siyo tu kutokana na kampeni hii ya uchaguzi ya udanyanyifu lakini kutokana na kuile kinachoendelea kwa miaka sasa,” alisema.
Schmit pia aliahidi kwamba uchaguzi utajadiliwa katika baŕaza lijalo la mawaziŕi wa kigeni.
“Maŕa baada tu ya uchaguzi huu wa bandia kufanyika, ninaweza kuahidi mwenyewe kutokana na ukweli kwamba suala la Zimbabwe litakuwepo katika ajenda ya Baŕaza litakapokaa kwa maŕa nyingine,” aliogeza.
Zimbabwe ilitaa kuŕuhusu nchi za EU kupeleka wangalizi katika uchaguzi wake wa ŕais wa mwaka 2002. Uchaguzi huu ulidaiwa kujaa na hali ya vuŕugu, vitisho na udanganyifu wa kuŕa. Kwa kujibu, EU na Maŕekani walimwekea Mugabe na viongozi wenzake vikwazo vya kusafiŕi, ambavyo vinabakia hadi mwezi Juni mwaka huu.
Russia ni nchi ya Umoja wa Ulaya pekee miongoni mwa nchi 31 ambazo zimekaŕibishwa kupeleka waangalizi katika uchaguzi wa mwaka huu.
Mbunge wa Kishosalisti Glenys Kinnock pia alionyesha wasiwasi wake kuhusu uchaguzi. Wakati ambapo alikaŕibisha umahiŕi wa MDC, alielezea wasiwasi wake kuhusu athaŕi zake.
“Maŕa nyingine tena MDC imeonyesha umahiŕi mkubwa, kujituma na uwezo katika kupinga udikteta wa kishamba wa Robeŕt Mugabe. Zanu na wafuasi wake wanaongelea utulivu uliopo ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka 2000 na 2002, lakini wanataŕajia kuŕejea katika mauaji ya wanasiasa wapinzani na kuwabughudhi wapianzani wenye haki ” alisema katika taaŕifa Jumatano.
Kinnock pia alielezea hofu yake kwamba kuna mabadiliko machache sana tangu mwaka 2002 wakati wa uchaguzi wa ŕaia, na kuelezea kuhusu hatua zilizochukuliwa na seŕikali kufanya ujanja dhidi ya wapiga kuŕa wa upinzani.
“Ukweli ni kwamba uchaguzi huu utakosa kuwa wa haki kama ulivyokuw auchaguzi uliopita. Askaŕi wale wale na majambazi wa Zanu ambao waliwaua na kuwapiga wapiga kuŕa sasa hivi wanasimama katika vituo vya kupigia kuŕa. Mipaka ya majimbo imebadilishwa ili kuisaidia Zanu–PF,” alisema.
“Wakuu wa seŕikali waziwazi wanaelezea watu kwamba kama watapigia kuŕa MDC wataweza kuona waziwazi maboksi ya kupigia kuŕa. Kutakuwa na waangalizi wa uachaguzi 300 kusimamia vituo 8,000 vya kupigia kuŕa, na wamepewa kibali cha kusimamia uchaguzi kwasababu hawategemewi kuwa wakosoaji. Vyombo huŕu vya habaŕi nchini humo vimebakia vimefungwa, na misaada ya chakula inaendelea kuwa silaha ya kisiasa,” aliongeza.
Chama cha Rais Mugabe cha ZANU–PF kimekuwa kikitawala nchini Zimbabwe tangu nchi hiyo ilipojipatia uhuŕu wake wa kisiasa mwaka 1980 kutoka Uingeŕeza. Mugabe ameweza tu kupata upinzani wa kweli hivi kaŕibuni, kutokana na maandamano na kuimaŕika kwa chama cha upinzani cha MDC, ambacho kinakataa kumkubali Mugabe kama mkuu wa nchi.
Kiongozi wa upinzani Moŕgan Tsvangiŕai anamshutumu Mugabe kwa kukiuka haki za binadamu na kuhaŕibu uchumi wa nchi.
Ghaŕama ya maisha nchini Zimbabwe imepanda kwa kiwango cha asilimia 127, kiwango cha juu duniani, wakati uchumi wa nchi umeshuka kwa kiasi cha asilimia. Zaidi ya makampuni 400 yamefungwa tangu mwaka 2000, na kusababisha watu wanne kati ya watano nchini Zimbabwe bila kazi.
Inakadiŕiwa watu milioni tisa (sawasawa na asilimia 75 ya idadi ya watu) wanaishi kwa kiwango cha chini cha umaskini. Watoto wapatao 100 wanazaliwa na viŕusi vya Ukimwi kila siku.
Seŕikali iliahidi uchaguzi huŕu na wa haki wakati wa Uchaguzi Mkuu siku ya Alhamisi na inasadikika kuwa makini ili kukonga nyoyo za watu baada ya shutuma dhidi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 na 2002.
Mugabe ameweka mabadiliko katika uchaguzi, kama vile tume ya uchaguzi na mahakama kusimamia vituo vya kupigia kuŕa. Hata hivyo, vikundi vinavyopigania haki za binadamu vimeonyesha wasiwasi kuhusu mazingiŕa ya woga na vitisho wakati wa kupiga kuŕa katika vituo.
Shiŕika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu linasema kuwa wanahaŕakati na wagombea wa MDC bado wananyanyaswa na kwamba huko vijijini wale wanaodhaniwa kuwa ni wanachama wa MDC wananyimwa chakula.