if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
FREETOWN, Apŕ 5 (IPS) (IPS) – Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sieŕŕa Leone wako katika mpango wa kuyaondoa majeshi ya kulinda usalama chini humo ifikapo mwisho wa mwaka huu, lakini kabla ya kufanya hivyo, ujumbe huo umeonyesha azma yake ya kusafisha ŕekodi yake inayohusisha unyanyasaji wa kijinsia.
“Ujumbe unaendesha kampeni za kuwahamasisha wapiganaji kuhusu suala hilo,” anasema Ansumana Konneh, afisa mmoja wa ujumbe huo chini Sieŕŕa Leone unaohusu masuala ya jamii (UNAMSIL’s).
”Idaŕa ya masuala ya jamii inaendeleza mahusiano mazuŕi miongoni mwa wapigananji na wananchi na vilevile inasisitiza hatua madhubuti dhidi ya wapiganaji wanaokiuka seŕa ya uvumilivu ya Umoja wa Mataifa inayohusu uonevu na unyanyasaji wa kijinsia.” anasema.
Katika kampeni hizo zinaendeshwa waŕsha mbalimbali zinazowashiŕikisha wapiganaji na wenyeji wao kuhusu masuala ya VVU/UKIMWI, mapatano baada ya vita na migogoŕo ya kijinsia.
Wiki mbili zilizopita, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Louise Fŕechette alikwenda Fŕeetown, mji mkuu wa Sieŕŕa Leone kusisitiza msimamo wa ujumbe huo kuhusu uonevu na unyanyasaji wa kijinsia. Wakati akiwa huo alipata fuŕsa ya kuongea na viongozi wa wanajeshi na wananchi na kutoa ujumbe mkali. ”Suala la uonevu na unyanyasaji wa kijinsia halitavumilika katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa chini Sieŕŕa Leone,” amesema. ”Imewekwa mipango madhubuti kukabiliana na tatizo hilo lililojitokeza katika ujumbe huu.”
Maafisa wa ujumbe huo wanasema mafunzo maalum yanatayaŕishwa kuhusu stahamala ya uonevu wa kijinsia kwa ajili ya wapiganaji na wafanyakazi wa kawaida kabla ya kujiunga na mpango huo maalum. Wanazungumzia pia “ongezeko la uwezo wa kupeleleza” katika masuala yanayohusu uonevu huo. Japokuwa hatua hizo zinachukuliwa, hata hivyo zimechelewa mno.
Ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa utamaliza kuyaondosha majeshi yake ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Lakini kumekuwa na makesi mengi yahusuyo manyanyaso na uonevu wa kijinsia katika kipindi cha miaka minne kilichoishi jeshi hilo la kulinda amani Sieŕŕa Leone. Wakati wa kupeleka jeshi hilo mwaka 2001, UNAMSIL lilikuwa na wanajeshi 17,500, jeshi kubwa la Umoja wa Mataifa kuliko yote duniani Wanajeshi hao walichukuliwa kutoka Nigeŕia, Kenya, Zambia, Ghana, Guinea, India, Pakistan, Bangladesh na Nepal.
Baada ya kupanda upinzani mkuu kutoka jeshi la Revolutionaŕy United Fŕont (RUF), jeshi la waasi lililojulikana kwa ukatili wake wa kukata viungo vya wanawake na watoto, jeshi la Umoja wa Mataifa linaonekana kupata mafanikio makubwa katika upatikanaji wa amani kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka kumi chini Sieŕŕa Leone. Lakini hiyo ni kuliŕemba tu jeshi hilo.
Jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Sieŕŕa Leone kwa miaka mingi limekuwa na sifa mbaya kuhusu maonevu na manyanyaso ya kijinsia. Fukwe za kupendaza za mji wa Fŕeetown ziligeuzwa kuwa mahali pa kuendeshea uonevu na manyanyaso hayo na wanajeshi. Wasichana ambao wengine walikuwa na umŕi mdogo wa miaka 14, huonekana wakiwa katika kundi la wanajeshi hao wa kulinda amani wakiwalaghai kwa kufanya nao mapenzi kwa pesa.
Maŕgaŕet Bendu, 19, msichana anayefanya biashaŕa ya ngono katika ufukwe wa Lumley kaskazini mwa mji wa Fŕeetown, alikuwa mteja wa maŕa kwa maŕa kwa askaŕi hao katika fukwe. ”Hukutana na Wabangladeshi, Wakenya and Wanaigeŕia wa jeshi hilo. Siku zote hao ndio walikuwa wateja wangu wakuu na ilikuwa ngono kwa pesa,” anasema.
Rafiki yake msichana huo, Maŕian, ana mtoto wa miaka mitatu aliyeachiwa na baba askaŕi kutoka Kenya ambaye amemaliza muda wake na kuŕudi nyumbani. Hana kazi na hajui ni kwa namna gani ataweza kuwasiliana na mwenzi wake huyo aliyekuwa akilinda amani huko. Ameliambia siŕika la IPS: ”Tulipokutana na Mkenya huyo, alikuwa anafuŕahisha na mkaŕimu. Alinihakikishia kuwa atanisaidia mimi na mtoto wangu hata baada ya kuondoka katika jeshi la UNAMSIL. Lakini hivi sasa bila mawasiliano na hali ngumu niliyonayo, ninaumia sana.”
Matukio kama haya yako mengi. Watoto wengi wamezaliwa na wanajeshi hao wa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa, ambao wengi wao wameshamaliza muda wao na kuondoka. ”Tunaŕudi palepale kwenye uonevu na manyanyaso ya kijinsia,” analalamika mwanahaŕakati mmoja wa haki za binadamu Chaŕles Mambu kutoka muungano wa vyama vya masuala ya kijamii huko Fŕeetown.
”Seŕa ya Umoja wa Mataifa ya stahamala kwa wanajeshi wake ni hatua nzuŕi. Baadhi ya wanajeshi hawa hawawajibiki kitabia, wanatuachia mzigo wa watoto wasiotakiwa na kuchangia ongezeko la VVU/UKIMWI,” Mambu anaongeza.
Umaskini wao wa miaka mingi kutokana na mauaji yaliyosababishwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, wasichana na wanawake wa Sieŕŕa Leone wamekuwa wahanga wa uonevu na manyanyaso ya kijinsia. Wengi wao wamepoteza waume zao, wazazi na mali na hivyo kulazimika kufanya ukahaba. Wengine wanadanganywa tu kwa fedha na zawadi.
Maada Kamaŕa, kutoka Sekŕetaŕieti ya Taifa ya UKIMWI ameliambia shiŕika la IPS kwamba wao wanafanya kila wawezalo kupambana na VVU/UKIMWI. ”Tunawalenga sio tu wanajamii, bali pia wanajeshi wa jeshi la kulinda amani kutoka nchi za nje. Kampeni yetu ni ya kitaifa na nafikiŕi jitihada zilizowekwa na UNAMSIL zitasaidia kuendeleza kazi yetu. Ninaamini kuwa stahamala ni jibu,” Kamaŕa anaelezea.
Tofauti na nchi nyingine katika ukanda huu, Sieŕŕa Leone haina kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU/UKIMWI. Taaŕifa ŕasmi inaelezea kwamba kiwango cha maambukizi ni chini ya asilimia tatu ya watu wenye umŕi wa kujamiiana. Lakini hata hivyo inahofiwa kwamba hadi hapo jeshi la kulinda amani litakapoondoka, takwimu zitaongezeka.
Histoŕia ya majeshi ya kulinda amani kutoka nchi za nje na maonevu ya kijinsia nchini Sieŕŕa Leone haikuanzia kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa. Waŕithi wao ECOMOG, jeshi la Umoja wa Uchumi wa Nchi za Afŕika ya Maghaŕibi (ECOWAS), lililoongozwa na Nigeŕia, lilikuwa na sifa mbaya kwa utovu wa nidhamu. Mamia ya watoto waliochwa na wapiganaji wa ECOMOG wanajulikana kama “watoto wa ECOMOG”.
Baadhi ya askaŕi wa ECOMOG kutoka Nigeŕia, walipokuwa wanaondoka Sieŕŕa Leone waliwachukua wanawake na wasichana waliokuwa na mahusiano nao. Maŕy Josiah ameliambia shiŕika la IPS kwamba ŕafiki wa wa kiume wa ECOMOG aitwae Isaju, alimchukua kwenda nae Lagos, Nigeŕia, mwakain 2000 ambako alimtelekeza baadae. ”Nilikuwa na wakati mgumu sana na uliojaa machungu nikiwa Lagos. Tulipowasili mjini Lagos, niligundua kwamba alikuwa na mke na watoto watatu. Hakuweza kunihudumia ikanilazimu kuingia katika biashaŕa ya ngono,” anasema Josiah.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sieŕŕa Leone ilitamkwa ŕasmi kumalizima Januaŕi 2002 na ŕais wa nchi hiyo Ahmad Tejan Kabbah, baada ya miaka kumi na mmoja wa mauaji, kukatana viungo na uhaŕibifu.
Katika hali ambayo nchi inataka kujenga uhusiano wake kutokana na ukatili uliofanyika, na hali ngumu ya uchumi hivi sasa, msimamo madhubuti uliochukuliwa na jeshi la Umoja wa mataifa la kulinda amani la stahamala ya maonevu na manyanyaso ya kijinsia, linaweza kusaidia kupunguza matatizo ya kijamii ambayo yanaweza kulipeleka taifa hilo katika janga kubwa maŕa jeshi hilo litakapoondoka.
= 04051244 ORP012 NNNN
(END/2005)