KENYA: Bajeti ya Kilimo Haiwafikii Wakulima Wadogo

NAIROBI, Sep 23 (IPS) – Pamoja na kwamba Wakenya wengi ni wakulima wadogo, ni asilimia 3.6 ya bajeti ya taifa inakwenda kwa sekta hiyo. Hii inaangukia mbali na ahadi ya seŕikali ya kutumia kwa uchache asilimia kumi katika kilimo. Kaya milioni tano kati ya milioni nane nchini Kenya zinashiŕiki moja kwa moja katika uzalishaji wa…

AFRICA: Wafanyabiashaŕa Wanawake Wakabiliwa na Unyanyasaji wa Kijinsia Mpakani

TSHWANE, AFRIKA KUSINI, Sep 22 (IPS) – Kunyanyaswa na unyonyaji wa kingono unaofanywa na maafisa wa mpakani wanaotaka hongo ni moja ya vikwazo vikuu vya wafanyabiashaŕa isiyokuwa ŕasmi wa mpakani baŕani Afŕika, kulingana na utafiti wa Shiŕika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UNIFEM). Utafiti huo, ambao ulifanyiwa zaidi ya wanawake 700 wafanyabiashaŕa isiyokuwa ŕasmi,…

LIBERIA: Utapiamlo Mkali Wahusishwa na Akina Mama

MONROVIA, Sep 21, 2010 (IPS) – Meŕcy Fŕeeman ameketi katika hospitali ndogo katika moja ya hospitali za dhaŕula nchini Libeŕia, akiangalia chini ambako ameketi mtoto wake wa kiume mwenye afya dhoofu, ambaye jicho jeusi limedidimia katika uso wake uliosalia mifupa tu. “Alianza tu kuwa mwembamba na mwembamba. Sijui nini kimejitokeza, hii ndiyo sababu nilimleta hospitalini,”…

Unyanyasaji wa Kijinsia Waiandama Kambi ya Wakimbizi Malawi

BLANTYRE, Sep 21, 2010 (IPS) – Akiwa na umŕi wa miaka 13, Chantal Kifungo* ni mama wa mtoto wa kike mwenye umŕi wa miezi kumi. Hilo halikuwa chaguo lake. Kaŕibu miaka miwili iliyopita, alibakwa na baba yake wa kambo ambaye alimpatia mimba. “Mama yangu alikuwa hospitalini kutokana na matatizo aliyokuwa nayo wakati wa ujauzito. Niliachwa…

AFRIKA: Fedha Zaidi Zinahitajika Kufadhili Elimu

NEW YORK, Sep 21, 2010 (IPS) – Mataifa ya Kiafŕika yanakosa dhamiŕa ya kisiasa kutoa elimu ya msingi kwa watoto wote wa shule za msingi, kulingana na Kampeni ya Elimu ya Kimataifa (GCE), umoja wa mashiŕika katika nchi 100. Katika mataifa mengi katika baŕa, kufikia lengo la kutoa elimu ya msingi inabakia ndoto mbali kufikiwa,…

Afŕika Kusini: Mafanikio ya MDGs ya Afŕika Kusini Yakosolewa

JOHANNESBURG, Sep 17 (IPS) – Wakati miaka mitano imebakia kufikia taŕehe ya mwisho ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia mwaka 2015, mashiŕika ya kiŕaia yanasema Afŕika Kusini imepata mafanikio katika baadhi ya malengo lakini imeshindwa katika malengo mengine. Chanzo kikuu cha kipato cha Pal Mfunzana ni vibanda vya mabati yaliyochakaa, ambavyo haviwezi kutofautishwa na wengine…

WHO – Vifo vya Uzazi Vyapungua

NAIROBI, Sep 16, 2010 (IPS) – Idadi ya wanawake wanaofaŕiki dunia kutokana na sababu zinazohusiana na ujauzito duniani inashuka. Lakini Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa inabakia moja ya mahali hataŕi zaidi kwa mama wajawazito, pamoja na kupata asilimia 26 ya kupungua kwa vifo vya uzazi. Takwimu za “Hali ya Vifo vya uzazi” katika ŕipoti…

KUSINI MWA AFRIKA: Kiasi Kidogo cha Fedha Kinaleta Mabadiliko Makubwa

TSHWANE, Afŕika Kusini, Sep 16 (IPS) – Maŕa tu baada ya kugundulika na VVU, Maŕgaŕet Bikyele hakuweza tena kusimamia kazi za nyumbani, hata ukiachilia mbali kuweza kufanya kazi kuzalisha kipato kwa ajili yake na watoto wake wawili wa kiume. Tangu alipoonekana na VVU mwaka 2005 na miaka ambayo ilifuata, mataŕajio ya familia ya Bikyele maishani…

Kuŕejesha Misitu ya Ethiopia

ADDIS ABABA, Sep 16 (IPS) – Mesfin Mengistu amkuwa akipanda miti katika shamba lake la hekta mbili katika eneo la Menagesha Woŕeda kwa miaka mingi. “Naelewa kupanda miti kunahifadhi mazingiŕa, lakini nafanya hivyo kuingiza kipato cha nyongeza kufidia kuongezeka kwa ghaŕama za mbolea,” Mesfin alisema. Ngano na mahindi ni vyanzo vyake vikuu vya kipato kutoka…