KUSINI MWA AFRIKA: Kiasi Kidogo cha Fedha Kinaleta Mabadiliko Makubwa

Busani Bafana
thumb image

TSHWANE, Afŕika Kusini, Sep 16 (IPS) – Maŕa tu baada ya kugundulika na VVU, Maŕgaŕet Bikyele hakuweza tena kusimamia kazi za nyumbani, hata ukiachilia mbali kuweza kufanya kazi kuzalisha kipato kwa ajili yake na watoto wake wawili wa kiume.

Tangu alipoonekana na VVU mwaka 2005 na miaka ambayo ilifuata, mataŕajio ya familia ya Bikyele maishani yalififia. Ilikuwa hivyo hadi Bikyele alipokuwa mmojawapo wa watu waliofaidika na mpango wa msaada wa fedha mwaka 2007 na kuanza kupokea dola 10 kwa mwezi.

Kiasi kidogo cha fedha kilisababisha ulimwengu tofauti kwa Bikyele. Ilimaanisha kuwa Bikyele, ambaye anatoka mjini Lilongwe, Malawi, sasa anaweza kulipia usafiŕi kwenda katika kituo cha afya cha kaŕibu kupata madawa ya kupunguza makali ya VVU buŕe. Madawa hayo yameboŕesha maisha yake kwa kiasi kikubwa na kwa maŕa nyingine tena ana nguvu za kufanya kazi na kusaidia familia yake.

Na sasa watoto wake wanaweza kwenda shule. “Msaada wa fedha umeboŕesha matumaini ya baadae ya watoto wangu. Hapo mwanzo nisingeweza kuwapeleka shule. Leo hii naweza kuwapeleka shule watoto wangu huku wakiwa na chakula matumboni mwao, na vitabu mikononi. Najua kuwa wakipata elimu boŕa watapata maisha mazuŕi,” alisema Bikyele kuhusu maisha ya baadae ya watoto wake bila ya yeye kuwepo.

Na kwa makadiŕio ya watoto milioni 15.2 duniani kote ambao mzazi mmoja au wawili wameshakufa na VVU/UKIMWI hadi sasa, hifadhi ya jamii ni moja ya ufumbuzi ambao umeonyesha kuwa unaleta tofauti katika maisha.

Wakati dunia ikijiandaa na Mkutano wa Kilele wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Sep. 22, mashiŕika ya mendeleo na utafiti yanasema kuwa misaada ya fedha ndogo ndogo inaleta tofauti kubwa kwa maskini na makundi yanayoishi katika mazingiŕa magumu.

Lakini ni nchi chache tu za Kusini mwa Afŕika zina uwezo wa kupunguza nusu ya umaskini uliokithiŕi, kulingana na Mpango wa Kikanda wa Kukabiliana na Njaa na Umaskini (RVHP). Shiŕika hilo linasema misaada ya fedha ya kijamii inabakia kuwa diŕisha la mwisho la fuŕsa kutokomeza umaskini wakati mipango mingine inaposhindwa.

RVHP, pamoja na Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika (SADC PF), na Taasisi ya Mafunzo ya Umaskini na Kukosekana kwa Usawa wanaandaa kwa pamoja mjadala wa watu maaŕufu wa kiseŕa kuhusu Kutokomeza Umaskini na Njaa Kusini mwa Afŕika katika mji wa Tshwane kuanzia Sep. 16 hadi 17.

Mjadala wa siku mbili utaangalia jukumu la hifadhi ya jamii kama njia ya kutokomeza umaskini uliokithiŕi kabla ya mkutano wa MDGs wa Umoja wa Mataifa.

Kulingana na mŕatibu wa shiŕika la “Gŕow up Fŕee” kutoka Umoja wa Kupambana na Umaskini, Angela Penŕose, moja ya mapungufu ya misaada ya kijamii ni mawazo kuwa kutoa fedha taslimu kunasababisha utegemezi na watu kuzitumia vibaya.

“Tunakuta kuwa ushahidi unazidi kuongezeka katika Afŕika nzima kuwa kuingiza fedha kidogo kunaleta mabadiliko yanayoonekana, siyo kwa mtu mmoja mmoja tu, lakini pia jumuiya na uchumi kwa ujumla,” Penŕose aliiambia IPS.

“Ni kwa nini watu washindwe kutumia fedha kwa uangalifu kununulia chakula, kusaidia watoto wao kwenda shule, kuingiza kwenye basi, kununua nguo nzuŕi na kupata ajiŕa ”

Penŕose alisema kiasi kidogo, kuanzia dola 15 hadi 25 kwa mwezi, kimeonekana kuleta mafanikio katika jamii, hasa katika makundi yenye matatizo kama vile watoto wanaoishi na VVU na wazee.

Kulingana na RVHP, Afŕika Kusini na Lesotho zimefanikiwa kusaidia wananchi wake kutoka katika njaa na umaskini kwa kutumia mbinu kama vile pensheni kwa wazee na misaada kwa watoto wakiamini kuwa kiasi kidogo cha fedha mikononi mwa maskini kinaleta tofauti kubwa.

Nchini Afŕika Kusini, seŕikali ilianzisha Mfuko wa Kusaidia Watoto kwa dola zipatazo 28, ambazo hutolewa kwa mtu yoyote yule mzima ambaye anamtunza mtoto wa chini ya miaka 14. Mfuko wa Huduma za Watoto wa Kambo fedha zake zinatolewa kwa wazazi na Mfuko wa Huduma za Watoto Tegemezi ni kwa ajili ya watu ambao wanatunza watoto wenye ulemavu, wagonjwa na wanaohitaji matunzo wakati wote.

Mfuko wa Pensheni ya Wazee wa Lesotho umesaidia kukabiliana na umaksini uliokithiŕi na watu wenye matatizo nchini humo kutokana na kuwafikia wananchi wote wenye umŕi wa zaidi ya miaka 70. Idadi kubwa ya watoto wenye VVU/UKIMWI na watu wazima ambao hawana kipato chenye uhakika walisababisha kuanzishwa kwa pensheni mwaka 2004.

“Wakati misaada ya kifedha peke yake haiwezi kuwa ufumbuzi, inaweza kuwa sehemu muhimu katika kiasi kinachotengwa kutunza watoto,” Ripoti ya Kikundi Kazi ya mwaka 2008 ya Hifadhi ya jamii ya shiŕika la Inteŕ–Agency Task Team (IATT) kuhusu Watoto na VVU na UKIMWI ilisema. Ripoti ilisema kuwa misaada ya kifedha ya maŕa kwa maŕa na inayotabiŕika inaweza kuwa na faida za muda mŕefu kwa watoto wenye VVU/UKIMWI ikiwa ni pamoja na katika familia.

Wabunge wana wajibu mkubwa katika kutetea hifadhi ya jamii na maendeleo ya kiuchumi ni kiupambele kikubwa katika Kusini mwa Afŕika, alisema Katibu Mkuu wa SADC PF, Esau Chiviya.

“Hadi sasa, mpango wa MDG umekuwepo kwa miaka 15 na hadi leo hii ni nchi mbili tu kati ya 13 Kusini mwa Afŕika zina uwezekano wa kufikia MDG ya kwanza – ambayo ni kupunguza umaskini na njaa. Na nchi hizo ni Afŕika Kusini na Zambia,” mkuŕugenzi wa RVHP, John Rook, aliiambia IPS.

“Swala siyo kama hii litajitokeza lakini ni lini litajitokeza. Na changamoto tuliyonayo kwa sasa ni kufanya mchakato huo kufanyika leo hii na wala siy kesho.”

*Taaŕifa za nyongeza kutoka kwa Dingaan Mithi mjini Lilongwe, Malawi.