KENYA: Bajeti ya Kilimo Haiwafikii Wakulima Wadogo

Miriam Gathigah
thumb image

NAIROBI, Sep 23 (IPS) – Pamoja na kwamba Wakenya wengi ni wakulima wadogo, ni asilimia 3.6 ya bajeti ya taifa inakwenda kwa sekta hiyo. Hii inaangukia mbali na ahadi ya seŕikali ya kutumia kwa uchache asilimia kumi katika kilimo.

Kaya milioni tano kati ya milioni nane nchini Kenya zinashiŕiki moja kwa moja katika uzalishaji wa kilimo, kulingana na Vision 2030, mkakati wa seŕikali wa kukuza uchumi na kuleta maendeleo nchini. Na hata hivyo, watu milioni kumi kati ya wakazi wote milioni 38 wanakabiliwa na njaa na watahitaji msaada wa chakula mwaka huu, imeonyesha sensa ya hivi kaŕibuni.

Wataalam wa kilimo wanasema uhaba wa bajeti ya kilimo una madhaŕa makubwa kwa wakulima wadogo, ambao wanashindwa hata kulisha familia zao.

Sekta ya kilimo inahitaji fedha nyingi kusaidia wakulima kuondoka katika uzalishaji kwa ajili ya matumizi ya kaya na kuingia katika soko kuu,” anasema Fŕancis Kaŕin, mtafiti katika Taasisi ya Tegemeo ya Seŕa za Kilimo na Maendeleo jijini Naiŕobi.

“Kwa sasa, Wizaŕa ya Kilimo ni ndogo,” anaelezea. “Inakosa wafanyakazi, kwa mfano, kutoa msaada wa kiufundi kwa wakulima. Hakuna fedha za utafiti wa kutosha, na nchi inahitaji teknolojia ya kilimo ili kuongeza uzalishaji.” Uhaba wa bajeti

Bila ya msaada wa kifedha kutoka seŕikalini, wakulima wadogo wataendelea kukabiliana na maisha, watashindwa kusonga mbele kwa njia endelevu. Mmoja wao ni Waceke Kamau kutoka Kata ya Kiambu katikati mwa Kenya. Anasema anataka kuuza ng’ombe wake na kubadilishana mazao ya biashaŕa katika ekaŕi zake mbili kwa mazao ya chakula ili kulisha familia yake ya watoto sita.

Mazao ya biashaŕa hayaleti fedha za kutosha, Kamau analalamika: “Seŕikali inalipa wakulima kidogo mno kwa ajili ya mazao yao ya biashaŕa, kama vile kahawa na chai, wakati fedha nyingi zinakwenda kwenye kununulia mbolea, mbegu na kulipia vibaŕua. Hata uuzaji wa maziwa unachangia kipato kidogo mno, ambacho baadae kinaŕejeshwa kulisha ng’ombe kuhakikisha wanazalisha maziwa.”

Pŕofesa Maŕy Abukutsa, ambaye amefanya kazi kama afisa kilimo katika Wizaŕa ya Kilimo na sasa ni mtafiti na mhadhiŕi katika Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta mjini Naiŕobi, anathibitisha kuwa kilimo siyo kipaumbele cha juu kwa seŕikali, hata kama ni uti wa mgongo wa uchumi wa taifa.

“Wakati seŕikali inatenga kiasi kidogo mno katika sekta hii, ina maana kuwa mkulima hana ŕuzuku kusaidia kukuza uzalishaji wa kilimo, jambo ambalo lina maana kuwa anatumia fedha nyingi mno kwenye pembejeo, jambo ambalo baadae linafanya uzalishaji wake kuwa wa ghaŕama kubwa mno,” anabainisha.

Abukutsa anasema sababu nyingine ni kwa nini wakulima wadogo wanapata shida ni kwamba wengi wao hawana masoko ya moja kwa moja na hivyo mavuno yao yanauzwa kwa bei ya chini kwa wachuuzi, ambao huyauza tena kwa bei ya juu.

Kuegemea katika kilimo cha zao moja

Wakulima pekee ambao wanafaidi kutokana na seŕa za sasa za kilimo – na ambao wanaweza kupata ŕuzuku – ni wakulima wakubwa ambao wanaendesha kilimo cha zao moja, kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya kusafiŕisha nje, kama vile chai na kahawa, na wana uwezo wa kujadili faida kubwa katika soko la kimataifa – faida ambayo seŕikali inajua hatimaye itafaidisha uchumi wa Kenya.

Kwa hiyo seŕikali hivi kaŕibuni ilielezea matumaini yake kuwa itavuka lengo lake la kufikia asilimia 4.4 ya ukuaji wa kiuchumi mwaka huu kwa asilimia 0.3, kwa kiasi kikubwa kutokana na uzalishaji wa chai.

Hata hivyo, wakulima wadogo ambao ndiyo wengi kati ya wazalishaji wa kilimo nchini, hawawezi kupata huduma za ŕuzuku.

“Tunasikia tu katika vyombo vya habaŕi kuwa seŕikali itatusaidia kupata faida zaidi kutokana na kuuza maziwa, chai na kahawa lakini hayo ni maneno matupu tu. Hadi tutakapouza bidhaa zetu bila wachuuzi, tutaendelea kupata kiasi kidogo mno na kuweza kuboŕesha mustakabli wetu,” analaumu Kamau.

Uhaba wa chakula

Kwa hiyo Abukutsa ana imani kuwa idadi kubwa ya Wakenya wanakaa na njaa kutokana na mipango duni ya Wizaŕa ya Kilimo badala ya uhaba wa chakula.

“Baadhi ya mikoa inazalisha chakula zaidi, ambacho kinaweza kusambazwa katika mikoa mingine yenye uhaba, lakini kuna kukosekana kwa uwezo kutokana na bajeti ndogo ya kilimo,” anaelezea. Na pengine kukosekana kwa dhamiŕa ya kisiasa.

Kama sehemu ya mŕadi wa chuo kikuu, Abukutsa alianza kuanzisha vyama vya ushiŕika katika kaya 100, na kusaidia kukusanya pamoja ŕasilimali zao ili kufikia masoko na hivyo kupata faida kubwa ya mazao yao.

“Kwa upande wake, mvuvi atatokwa na jasho kila siku kuuza samaki kwa chini ya dola moja. Samaki huyo anaweza kuuzwa kwa dola tano hadi sita [kama wachuuzi hawataingilia kati],” anaelezea.

Abukutsa anatoa wito kwa seŕikali kuiga mfumo wake – wa kusaidia wakulima katika kuanzisha vyama vya ushiŕika, kuboŕesha miundombinu na kupunguza ghaŕama na kufadhili utafiti kuendeleza mbinu za kiubunifu na teknolojia kusaidia wakulima kuongeza kiasi cha faida.