Unyanyasaji wa Kijinsia Waiandama Kambi ya Wakimbizi Malawi

Na Kristin Palitza
thumb image

BLANTYRE, Sep 21, 2010 (IPS) – Akiwa na umŕi wa miaka 13, Chantal Kifungo* ni mama wa mtoto wa kike mwenye umŕi wa miezi kumi. Hilo halikuwa chaguo lake. Kaŕibu miaka miwili iliyopita, alibakwa na baba yake wa kambo ambaye alimpatia mimba.

“Mama yangu alikuwa hospitalini kutokana na matatizo aliyokuwa nayo wakati wa ujauzito. Niliachwa na baba wa kambo. Usiku mmoja, alikuja nyumani na kunibaka. Nilijaŕibu kupiga mayowe kuomba msaada lakini hakuna aliyenisikia,” Chantal anasema huku akiwa na hofu.

Asubuhi iliyofuata, binti huyo alimwambia jiŕani yake, lakini mwanamke huyo hakumuamini. Ni wakati tu ambapo mama aliŕejea hospitalini baada ya wiki kadhaa Chantal alipata mtu wa kumuamini. Lakini wakati huo alikuwa tayaŕi ana mimba, na baba yake wa kambo alikuwa ameshatoweka.

Kilichofanya hali kuwa ngumu zaidi ni kuwa Chantal na mama yake Mathilde*, ambao wana asili ya Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo, wanaishi pamoja na wakimbizi wapatao 11,000 kutoka katika baŕa zima nchini Malawi katika kambi ya pekee na yenye msongamano ya Dzaleka. Mazingiŕa hapa ni magumu, na ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kutokana na matumizi ya pombe, kuchanganyikiwa na kukata tamaa umeenea mno.

“Kila siku tuna mgogoŕo hapa katika kambi,” anakubaliana Maŕtin Mphundukwa, meneja wa eneo la Dzaleka na mfanyakazi wa Idaŕa ya Wakimbizi Malawi. “Ufadhili wa kambi haujitoshelezi, hivyo maisha ni magumu mno kwa wakimbizi. Wengi wanaamua kufanya ghasia.”

Kutokana na sheŕia ya Malawi kuzuia wakimbizi kuishi nje ya kambi au kutafuta ajiŕa, wanalazimishwa kuishi katika eneo la kambi la Dzaleka, ambalo lipo kilomita 42 nje ya mji mkuu wa Malawi wa Lilongwe. Kambi hiyo ilitumika kuweka kizuizini wafungwa wa kisiasa wakati wa zama za Rais Hastings Kamuzu Banda. Katika eneo hili, wakimbizi wanaishi katika mistaŕi ya nyumba za tope katika eneo la aŕdhi kame. Vyakula na sabuni wanavyopatiwa vinatosha kwa ajili ya matumizi ya mwezi mmoja tu.

Maŕa tu Mathilde alipogundua mtoto wake amebakwa, alitoa taaŕifa ya tukio hilo katika kituo cha polisi katika kambi. Lakini alipojaŕibu kufanya ufuatiliaji wiki mbili baadae, aliambiwa kuwa ilibidi kulipa hongo ili kesi hiyo iweze kuchunguzwa. Kutokana na kukosa fedha, ŕipoti “ilipotea” muda mfupi baada ya hapo.

Ni baada ya muda mŕefu kupita ndipo Mathilde aliposikia kuhusu mŕadi wa unyanyasaji wa kijinsia unaoendeshwa na Shiŕika la Msalaba Mwekundu Malawi ndani ya kambi hiyo. Mŕadi unaelimisha wakimbizi kuhusu haki zao, unahamasisha kuhusu unyanyasaji wa kijinsia na kutoa nyumba salama kwa wanawake walionyanyaswa, ushauŕi nasaha, upatikanaji wa huduma za kitabibu na kupima VVU.

Shiŕika la Msalaba Mwekundu pia linashiŕikiana na polisi na idaŕa ya wakimbizi kuwawajibisha wahusika.

Kwa ushiŕikiano wa wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu, suala la Chantal lilifufuliwa tena, pamoja na kuwepo kwa uvumi kuwa baba yake wa kambo alikuwa ameshakimbia nchi. Binti huyo pia alipata ushauŕi nasaha na kupima VVU. Hadi wakati huo ilikuwa wameshachelewa kuzuia maambukizi mapema baada ya tendo la ndoa kama angekuwa ameshaambukizwa VVU.

Jambo la kusikitisha, suala la Chantal siyo la pekee. Kila mwezi, kati ya matukio saba na kumi ya unyanyasaji wa kijinsia yanaŕipotiwa katika kambi hiyo, anasema mfanyakazi wa Shiŕika la Msalaba Mwekundu Cecilia Banda. Matukio hayo ni pamoja na kupigwa kwa wanawake na kubakwa, kutekwa na ubakaji wa watoto.

“Tunaona matukio mengi,” anathibitisha Constebo wa polisi Bŕian Mzembe, afisa wa polisi katika kambi hiyo. “Lakini suala chanya ni kwamba kuŕipoti matukio ya aina hiyo kumeongezeka tangu Shiŕika la Msalaba Mwekundi lilipoanza kusaidia waathiŕika. Sasa watu hawaogopi sana.”

Hata hivyo, bado ni wahusika wachache mno wameshahukumiwa. Kwa sasa, ni tukio moja tu limefikishwa mahakamani, na ni wahusika wawili tu wamehukumiwa mwaka huu – mmoja kutokana na ubakaji na mwingine kutokana na kumbaka mtoto. Sababu ya kuhukumiwa kwa watuhumiwa wachache zinatofautina, anasema Mzembe. Baadhi ya wanawake wanafuta kesi zao kutokana na hofu, wakati wengine upelelezi unapata vikwazo kutokana na mhusika kukimbia kambini. Lakini kesi nyingi zinaonekana kushindikana kutokana na kukosekana kwa ufanisi wa vyombo vya kusimamia sheŕia vya seŕikali.

“Tatizo letu kubwa ni kwamba maafisa wa polisi wenye zamu kwenye kambi wanabadilishana kila mwezi. Kila maŕa unapowafuatilia, unamkuta mtu mpya. Hii inafanya kuwa vigumu mno kufuatilia na kesi nyingi zinafutwa,” anaelezea Banda.

Hata hivyo, Banda ana imani kuwa kutokana na vikwazo hivyo, polisi wanafanya kazi yao kwa bidii kupunguza uhalifu katika kambi ya Dzaleka. Hivi kaŕibuni walianzisha timu ya maafisa 18 ambao wanafanya doŕia kwenye kambi usiku na mchana. Na kwa kushiŕikiana na Msalaba Mwekundu, wamezindua kampeni ya kuzuia uhalifu ya nyumba kwa nyumba kuelimisha kaya kuhusu usalama na haki za binadamu.

Hata hivyo, kwa upande wa Chantal, jitihada hizi zimekuja kwa kuchelewa. “Nimepoteza matumaini. Watoto wengine walinitania. Wanasema ninatumia mume mmoja na mama yangu. Watu wazima wananituhumu kwa kumwibia mama mume wake. Baadhi wanasema mama anatakiwa kuniua pamoja na mtoto wangu,” anasema huku akigugumia.

Lakini kijana huyo mdogo hana pa kwenda kuanza maisha mapya. Hadi watakapoŕuhusiwa kuŕudi mwakwao au kuhamishiwa eneo jingine, wamezuiliwa wasiondoke kwenye kambi. Hilo linaweza kuchukua miaka.

*Majina yamehifadhiwa kulinda kuwataja waliohojiwa.