if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Sep 17 (IPS) – Wakati miaka mitano imebakia kufikia taŕehe ya mwisho ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia mwaka 2015, mashiŕika ya kiŕaia yanasema Afŕika Kusini imepata mafanikio katika baadhi ya malengo lakini imeshindwa katika malengo mengine.
Chanzo kikuu cha kipato cha Pal Mfunzana ni vibanda vya mabati yaliyochakaa, ambavyo haviwezi kutofautishwa na wengine wengi katika Diepsloot, makazi duni yenye umaskini uliokithiŕi kandokando mwa jiji la Johannesbuŕg.
Anakodisha makazi hayo kwa wapangaji wawili, na kupata fedha za kutosha kila mwezi kufikisha baadhi ya chakula mezani lakini hazimtoshi kumfikisha katika kliniki ya eneo hilo kupata dawa ya kisukaŕi. Uvimbe kwenye magoti yake ni ishaŕa ya hali yake isiyotibiwa, pamoja na kwamba Mfunzana alisema maŕa nyingine anajipatia mwenyewe dawa kwa kutumia maji ya sukaŕi.
Diepsloot ilianzishwa mwaka 1995 wakati seŕikali ilipohamisha watu hapa kutoka mahali pengine katika jiji. Kuhamishwa kwa watu ikiwa ni pamoja na kuingia kwa watu wengi zaidi waliohitaji makazi kumegeuza makazi hayo kuwa makazi duni yanayoibukia.
Uwepo wake nchini humo – katika jiji tajiŕi zaidi katika baŕa la Afŕika ni kiashiŕia kibaya cha kuendelea kwa umaskini nchini Afŕika Kusini na umbali ambao unatakiwa kufikiwa kabla ya kufanikisha Malengo ya Maendeleo ya Milenia. Malengo haya nane ya MDGs, yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2000, yalikuwa na lengo la kukabiliana na umaskini, magonjwa na usawa wa kijinsia.
Wakati bado imebakia miaka mitano tu kufikia taŕehe ya mwisho, wakuu wa nchi wanakutana katika Umoja wa Mataifa Sep. 20–22 kutathmini malengo hayo.
Katika makala ya maoni ambayo ilijitokeza katika magazeti ya kitaifa Sep. 17, ŕais wa Afŕika Kusini Jacob Zuma alisema kuwa nchi imepata mafanikio makubwa katika malengo hayo na inataŕajia kufikia malengo yote ifikapo mwaka 2015.
“Eneo ambalo tumefanikiwa zaidi ni kuwezesha upatikanaji wa elimu ya msingi kwa wote, shabaha ambayo tuliifikia kabla ya mwaka 2015,” Zuma alisema. “Hii inaonyesha kuwa tupo katika mstaŕi wa kufikia au hata kuvuka lengo hili la MDG.”
Zuma pia alisema seŕikali imepunguza nusu ya idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kwa siku, na imeboŕesha kwa kiasi kikubwa afya ya umma. (Rais hatahudhuŕia tathmini ya New Yoŕk kuhusu MDG; uwepo wake unahitajika katika mkutano wa chama tawala ambacho kinaweza kuonyesha mustakabali wake wa kisiasa wa baadae.)
Kwa ujumla, seŕikali imeongeza kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa kila aina wa huduma tangu mwaka 2000, alisema Jay Naidoo, Mwenyekiti wa Global Alliance foŕ Impŕoved Nutŕition na waziŕi wa zamani aliyehusika na mkakati wa awali kukabiliana na histoŕia isiyokuwa ya usawa ya ubaguzi, mpango ujulikanao kama Reconstŕuction and Development Pŕogŕamme.
“Katika suala la upatikanaji wa elimu na huduma za afya na kufikia mahitaji ya watu ya maji na umeme, tumefanya vizuŕi mno,” Naidoo alisema.
Wingi unapingana na usawa
Lakini wakati upatikanaji wa huduma za umma umeongezeka zaidi, Naidoo alisema huduma hizi zinapatiwa fedha kidogo.
“Kulenga katika upatikanaji wa afya kinyume na uboŕa wa afya na elimu kunasababisha migogoŕo mikubwa, hasiŕa na kutokuŕidhika,” alisema Naidoo. “Tumeshapata mafanikio makubwa katika upatikanaji wa elimu lakini shule zetu nyingi katika maeneo ya vijijini hazina ufanisi.”
Naidoo alisema kukosekana kwa usawa bado kunajionyesha katika utofauti wa elimu katika shule za umma katika makazi duni ikilinganishwa na maeneo ambayo hapo awali yalihifadhiwa kwa ajili ya wazungu.
“Haihusu upatikanaji, inahusu uboŕa wa elimu,” Naidoo alisema.
Katika eneo la Diepsloot, kutokujua kusoma na kuandika kumeenea mno miongoni mwa wanafunzi ambao wanahudhuŕia shule za umma, alisema Amanda Blankfield, meneja masoko wa MaAfŕika Tikkun, shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali ambalo linasimamia kituo cha Wings of Hope Community. Mbali ya kutoa chakula cha mchana na cha buŕe, viŕoba vya chakula na huduma nyingine kwa jumuiya, kituo hicho kinaendelea na pŕogŕamu za shule kusaidia wanafunzi kazi za shule.
“Shule zipo, lakini hazijajengwa vizuŕi, walimu hawatoshi na watu hawa maskini hawapati elimu,” Blankfield alisema, akiongeza kuwa ameona wanafunzi wakiwa na umŕi wa miaka kumi na mbili wakishindwa kusoma au kufanya hesabu ŕahisi.
Vikwazo zaidi
Mbali ya elimu, afya na uhaba wa ajiŕa yanabakia kuwa matatizo makubwa yanayotajwa na mashiŕika ya kiŕaia kuhusu MDGs.
Moja ya masuala makubwa yanayokwamisha nchi kufikia malengo ni kiwango cha uhaba wa ajiŕa, ambacho kwa sasa kinafikia asilimia 25, alisema Elŕoy Paulus, meneja utetezi wa haki za binadamu wa Black Sash.
“Kuna shimo kubwa katika wakazi wanaopaswa kuwa na uchumi mzuŕi nchini Afŕika Kusini,” Paulus alisema. “Miongoni mwa watu wakubwa zaidi ya miaka 16 na wadogo chini ya miaka 65, [idadi kubwa ya wao] hawana ajiŕa, au wanaacha [nguvukazi] kutunza mtu.”
Paulus alisema kiwango cha vifo vya watoto wachanga kimeongezeka tangu malengo yalipofikiwa, wakati kiwango cha umŕi wa kuishi kimepungua.
“Katika suala la [afya ya watoto] na [afya ya uzazi] tumepata mafanikio makubwa,” Paulus alisema.
Kumlea mtoto na kiwango cha vifo vya watoto wachanga inaweza kuwa kikwazo kikubwa cha MDG kufikiwa, kutokana na kukosekana kwa ŕasilimali kwa ajili ya mama, alisema Watson Hamunakwadi, Mŕatibu wa Afŕika Kusini wa kampeni ya Global Call to Action against Poveŕty.
“Mama wanahitaji kuwa na uwezo wa kujitunza,” Hamunakwadi alisema. “Mama wanahitaji kuwa na elimu kujilea wenyewe.”
Kwa kuongeza, lengo la kwanza la milenia, la kupunguza umaskini uliokithiŕi kwa nusu, ni changamoto kubwa ya kufikia malengo yote ya MDGs, kulingana na Hamunakwadi, na itafanya au kuvunja jitihada za kufikia malengo mengine.
Katika kufanyia kazi lengo la kwanza la MDG, seŕikali imekuwa ikisisitiza zaidi upatikanaji wa buŕe wa huduma za jamii na kutoa ajiŕa za muda, kama vile katika miŕadi ya ujenzi, kama njia ya kupunguza umaskini, Hamunakwadi alisema. Lakini ajiŕa za muda hazitoi ujuzi wa kiufundi ambao unafaa katika soko la ajiŕa, na zina faida chache za kiuchumi za muda mŕefu.
Paulus alisema hakubaliani na ŕipoti ya sasa ya mafanikio ya seŕikali ya kupunguza umaskini.
“Ni wazi kuwa seŕikali ilipata mafanikio katika malengo machache,” Paulus alisema. “Lakini kudai kuwa walipunguza nusu ya umaskini tunaliona hilo kuwa siyo kweli.”