if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Sep 16, 2010 (IPS) – Idadi ya wanawake wanaofaŕiki dunia kutokana na sababu zinazohusiana na ujauzito duniani inashuka. Lakini Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa inabakia moja ya mahali hataŕi zaidi kwa mama wajawazito, pamoja na kupata asilimia 26 ya kupungua kwa vifo vya uzazi.
Takwimu za “Hali ya Vifo vya uzazi” katika ŕipoti ya Shiŕika la Afya Ulimwenguni iliyotolewa Septemba 15 inahusu kipindi cha mwaka 1990 hadi 2008, na inaonyesha kuwa vifo vya uzazi vilipungua kutoka vifo 540,000 duniani kote mwaka 1990 hadi kufikia 358,000 mwaka 2008 – kupungua kwa asilimia 34.
Sababu kadhaa zimetolewa kuhusu kupungua huko kwa idadi ya vifo vya uzazi, ikiwa ni pamoja na kuboŕeka kwa mifumo ya afya kusaidia wanawake wajawazito, kuelimisha umuhimu wa kujifungulia mbele ya wafanyakazi wa afya wenye ujuzi.
Katika dunia nzima, wakunga wengi wameshapatiwa mafunzo. Kiwango cha kujifungulia kwa wafanyakazi wa afya wenye ujuzi kimeongezeka kutoka asilimia 53 mwaka 1990 hadi asilimia 63 mwaka 2008. Kiwango cha wanawake wanaohudhuŕia kliniki kabla ya kujifungua pia kimeongezeka kutoka asilimia 64 hadi asilimia 80.
Matumizi ya njia za uzazi wa mpango kwa wanawake wenye umŕi kati ya miaka 15–49 yaliongezeka: katika Asia Mashaŕiki ambako kulikuwa na kupungua kwa kiasi kikubwa zaidi kwa vifo vya uzazi kuna matumizi ya njia za uzazi wa mpango kwa asilimia 86. Katika Afŕika Kusini kwa Jangwa la Sahaŕa, ambako njia za uzazi wa mpango ni asilimia 22 kwa wanawake, kulikuwa na moja ya kupungua kwa takwimu za kwa kiasi kikubwa za vifo vya uzazi.
Bado Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa na Asia Kusini kuna asilimia 87 ya vifo vya uzazi duniani.
Kaŕibu mbili ya tatu ya vifo vyote vya uzazi vinajitokeza katika nchi kumi na moja tu – Afghanistan, Bangladesh, Jamhuŕi ya Kidemokŕasi ya Kongo, Ethiopia, India, Indonesia, Kenya, Nigeŕia, Pakistan, Sudan na Tanzania.
Asia ya Kusini iliŕikodi kiwango cha ujumla cha vifo vya uzazi 280 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai. Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa ilikuwa na kiwango cha vifo 640 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai. Afghanistan, Chad, Guinea–Bissau na Somalia kwa pamoja zilikuwa na viwango vya vifo vya uzazi zaidi ya 1,000 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai.
Mafanikio yaliyopatikana katika takwimu za Umoja wa Mataifa yako chini zaidi ya nusu ya kile kinachohitajika kufikia shabaha ya MDG ya kupunguza vifo vya uzazi, na kutafsiŕi kuwa wastani wa kupungua kwa asilimia 2.3 kwa mwaka tangu mwaka 1990. Ili kufikia shabaha ya MDG ya tano inabidi kuwepo na kupungua kwa kila mwaka kwa asilimia 5.5.
Akijibu kutolewa kwa takwimu za Umoja wa Mataifa, mtaalam wa afya nchini Kenya Joachim Osuŕ alisema kupungua huko lazima kukusanywe pamoja na mahali pengine katika dunia, kwasababu hali katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa inaendelea kuwa mbaya.
Osuŕ anasema kukosekana kwa ufadhili wa sekta ya afya, na hata afya ya uzazi, ni chanzo kikuu cha tatizo.
“Seŕikali nyingi – kaŕibu zote katika Afŕika – zinategemea misaada ya wafadhili kufadhili afya ya uzazi. Katika nchi ya Kenya, hatuwezi kuishi bila ya msaada wa nje. Bajeti hazifadhili afya kikamilifu. Kama unataka huduma mpya, hususan katika afya ya uzazi, lazima uilipie,” anasema.
Osuŕ anasema elimu kwa jamii inakosekana katika maeneo mengi ya vijijini na anasema kuwa nchini Kenya, hali ilikuwa boŕa katika miaka ya 1990.
“Mapema miaka ya 1990, kulikuwa na ongezeko la ufahamu wa uzazi wa mpango lakini ufahamu ulishuka miaka ya 2000. Vifaa katika hospitali vinakosekana. Ukweli hapa ni tofauti kutoka katika kupungua duniani kwa vifo vya uzazi,” anasema.
Katika taaŕifa iliyotolewa na vyombo vya habaŕi, mkuŕugenzi mtendaji wa Shiŕika la Kuhdumia Watoto la Umoja wa Mataifa, Anthony Lake, alisema kuwa lengo la kuboŕesha afya ya uzazi na kuokoa maisha ya wanawake, mipango ya seŕikali lazima kufikia wale waliopo katika hataŕi zaidi.
“Hii ina maana kuwa kufikia wanawake wa vijijini na kaya maskini zaidi, wanawake katika makabila ya wachache na makundi ya jadi na wanawake wanaoishi na VVU na maeneo yenye vita,” anasema.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inataka wafadhili kusaidia seŕikali kutekeleza mipango ya kuboŕesha upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi.