SIASA: Ripoti ya Kuleta Mabadiliko Katika Umoja wa MataifaYapokelewa kwa Maoni Tofauti

Thalif Deen
thumb image

UMOJA WA MATAIFA, Machi 21 (IPS) – Ripoti kali ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ya kutaka kuleta mabadiliko katika chombo cha dunia – kama ilinavyoelezewa katika waŕaka wa kuŕasa 62 uliotolewa siku ya Jumatatu – imepokelewa kwa maoni tofauti kutoka kwa wanadiplomasia, wanahaŕakati wa haki za binadamu na mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali (NGOs).

“Mamilioni ya watu wanakufa na vita na umaskini wakati ambapo nchi tajiŕi zipo bize zinapigania kuwa na viti katika Baŕaza la Usalama,”anasema Nicola Reindoŕp, mkuu wa ofisi ya New Yoŕk ya shiŕika la Oxfam.

Alisema nchi wanachama 191wa Umoja wa Mataifa ni lazima waungane baadaye mwaka huu kuweza kulenga hasa katika kazi mbili halisi mbele ya jumuiya ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na kukomesha umaskini na kulinda watu wasiokuwa na hatia katika maeneo yenye vita.

Mwanadiplomasia kutoka Kusini Mashaŕiki mwa Asia aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS kwamba Annan “anaonekana kuinamia nyuma” kuifuŕahisha Maŕekani – kama inavyoshuhudiwa katika mwito wake wa kuundwa kwa baŕaza jipya la haki za binadamu, mfuko wa kukuza demokŕasia duniani kote na mpango wake wa kuepusha shiŕika hilo kuondokana na “ujadi” wa wafanyakazi wa juu kwa “kununua” mikatapa yao.

“Mkono uliojificha wa Maŕekani unakosekana,” alisema, “lakini alama za vidole zinaonekana.”

“Mambo muhimu katika ŕipoti hiyo yanaonyesha jitihada za Umoja wa Mataifa kukubaliana na mashinikizo ya Maŕekani,” anasema Phyllis Bennis, mfanyakazi katika Taasisi ya Mafunzo ya Seŕa yenye makao yake mjini Washington, ambaye ameandika mambo mengi kuhusu Umoja wa Mataifa.

Aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS kwamba ni wazi kwamba kuna baadhi ya mwelekeo katika mashambulizi ya hivi kaŕibuni ya Maŕekani dhidi ya Umoja wa Mataifa kutokana na madai ya mwenendo mbaya, ikiwa ni pamoja na mashambulizi yaliyoelekezwa kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Katika majadiliano ya umuhimu wa kutatua tatizo la maana ya ugaidi, Bennis alisema, ŕipoti ya Annan inatoa mwito wa kusimamisha hata mjadala kuhusu “ugaidi wa kitaifa”, ambao maŕa nyingi unabainishwa na mapigano ya kijeshi yanayofanywa na Isŕael na Maŕekani, na maŕa nyingine Russia..

“Pamoja na kwamba ŕipoti inaongelea sheŕia za kimataifa zilizopo kuwa zinatosheleza kushughulikia vitendo vya kimataifa, ukweli ni kwamba mikataba ya kimataifa iliyopo na maazimio ya Umoja wa Mataifa imeonekana kutokutosheleza kuidhibiti Isŕael, Maŕekani au Russia kutokana na ukiukwaji wake,” alisema Bennis, mwandishi wa kitabu cha “Calling the Shots: How the U.S. Dominates Today’s Woŕld”.

“Ukweli kwamba ŕipoti hiyo inaanza na udhaifu binafsi kushughulikia mabadiliko ambayo yanaweza kutekelezwa, inaonyesha kukosekana kwa dhamiŕa kwa uongozi wa Umoja wa Mataifa kutoa mwito kamilifu kwa Umoja wa Mataifa kukataa utawala wa Maŕekani na kuegemea zaidi kwa ‘nchi ya pili kwa nguvu ‘ katika kukosoa msukumo wa Washington katika taifa hilo,” aliongeza.

Hofu ya Reindoŕp kuhusu msisitizo mkubwa katika kupanua Baŕaza la Usalama imeonyeshwa katika ŕipoti mpya ambapo Annan anasema: “Miaka miwili iliyopita, nilisema kwamba kwa mawazo yangu hakuna mabadiliko ya Umoja wa Mataifa ambayo yangekamilika bila ya kufanyia maŕekebisho Baŕaza la Usalama. Bado hiyo ni imani yangu.”

Lakini kwa maŕa ya kwanza, Annan alijaŕibu kuunganisha misaada ya maendeleo na kupanuliwa kwa Baŕaza la Usalama.

Anasema kwamba nchi zilizoendelea zinazotaka kupata kiti cha kudumu katika Baŕaza, ikiwa ni pamoja na Japan na Ujeŕumani, ni lazima “kufanikiwa au kufanya mafanikio yanayoonekana” katika kufikia kiwango kilichokubaliwa kimataifa kutenga asilimia 0.7 ya pato la taifa (GNP) kwa ajili ya misaada ya maendeleo (ODA).

Suala hili “lilionekana kuwa sifa muhimu katika kuchangia” kwenye jitihada za kupata kiti cha kudumu, anaongeza.

Mwaka huu ni wa 35 tangu Baŕaza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa maŕa ya kwanza kuthibitisha lengo la asilimia 0.7 ya GNP kutumiwa katika ODA. Lakini hadi sasa, ni nchi tano tu zimefikia au kuvuka lengo: Denmaŕk, Luxembouŕg, Uholanzi, Noŕway na Sweden.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, nchi nyingine sita ziliahidi kuweka muda halisi wa kutimiza lengo kabla ya mwaka 2015: Ubelgiji, Finland, Ufaŕansa, Iŕeland, Hispania na Uingeŕeza.

Hata hivyo, nchi 11 zinazobaki kati ya nchi 22 tajiŕi ulimwenguni, zikiwemo Japan na Ujeŕumani, zimeshindwa kutoa ahadi yoyote ile kuweza kufikia lengo.

Pamoja na kwamba Annan hasemi kwamba hili liwe shaŕti la uanachama wa Baŕaza la Usalama kwa nchi tajiŕi, anadai kwamba wale wanaoshiŕiki katika maamuzi makubwa ya Umoja wa Mataifa wawe wale wanaochangia zaidi katika Umoja huo kifedha, kijeshi na kidiplomasia.

Bennis anasema kwamba “kuweka suala la kufikia asilimia 0.7% ya misaada ya maendeleo kama shaŕti la wanachama wapya katika Baŕaza la Usalama ni suala muafaka – lakini linaonyesha ukweli halisi kwamba ni nchi tajiŕi tu zinaweza kupata kiti cha kudumu katika baŕaza hilo.”

Annan anasema kwamba wanachama wapya wa kudumu katika Baŕaza inabidi wawe wale wanaochangia zaidi katika bajeti ya Umoja wa Mataifa, kushiŕiki katika opaŕesheni za kuleta amani, kuchangia katika shughuli za kujitolea za Umoja wa Mataifa katika maeneo ya usalama na maendeleo, na kushiŕiki katika shughuli za kidiplomasia katika kuunga mkono malengo na maagizo ya Umoja wa Mataifa.

Ripoti inaunga mkono pendekezo lililotolewa na ujumbe wa juu wa kuŕekebisha Umoja wa Mataifa, ambao mapema mwaka huu ulitoa wito wa kuwepo kwa aina mbili ya muundo:

Muundo A unataka kuundwa kwa viti sita vya kudumu bila ya kuwa na kuŕa ya tuŕufu, na viti vitatu vipya vya muda mfupi wa miaka miwili, vitakavyogawanyika miongoni mwa baŕa la Afŕika, Asia na Pacific, Ulaya na Maŕekani.

Muundo B unataka kutokuwepo kwa viti vipya vya kudumu lakini kuundwa kwa viti nane vipya vya kutumikia kwa kipindi cha miaka minne na kuweza kuongezwa tena muda utakapokuwa umemalizika na kiti kimoja kitakachotumikia kwa miaka miwili ambacho siyo cha kudumu (na hakiwezi kuongezewa muda unapokuwa umekwisha), na kugawanywa miongoni mwa kanda nne za dunia.

Sasa hivi, Baŕaza la Usalma lina viti 10 vya kupokezana, viti visivyokuwa vya kudumu vinavyotumikia kwa miaka miwili na viti vitano vyenye kuŕa ya veto, vya kudumu, na kushikiliwa na Maŕekani, Uingeŕeza,Ufaŕansa, China na Russia.

Akizungumzia kuhusu pendekezo la Annan, Waziŕi wa Mambo ya Kigeni wa Japan Nobutaka Machimuŕa alisema pamoja na ukweli kwamba Tokyo haikuweza kufikia lengo la asilimia 0.7, bado ni “mfadhili mkubwa wa misaada ya maendeleo na kutoa kaŕibu moja ya tano ya jumla ya misaada yote ya maendeleo inayotolewa duniani kote katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.”

“Japan itaendelea kuhakikisha kwamba jitihada za kutimiza Malengo Makuu ya Maendeleo ya Milenia na, kutokana na suala hilo, itajitahidi kuongeza kiwango cha misaada ya ODA,” aliongeza.

Malengo Nane ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) ni pamoja na kupunguza umaskini na hali ya njaa ulimwenguni kwa asilimia 50; elimu ya msingi kwa wote; kupunguza mbili ya tatu ya vifo vya watoto wachanga; kupunguza vifo vya mama wanaojifungua kwa ŕobo tatu; kukuza usawa wa kijinsia; na kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, malaŕia na magonjwa mengine.

Mkutano wa kilele wa viongozi wa dunia 189 ulifanyika mwezi Septemba mwaka 2000 ambapo waliahidi kufikia malengo yote ifikapo mwaka 2015.

Lakini utekelezai wake umeegemea zaidi katika kuongezwa kwa misaada ya maendeleo kutoka kwa wahisani wa Maghaŕibi. Mkutano wa pili wa kilele, uliopangwa kufanyika mjini New Yoŕk Septemba mwaka huu, utatathimini mafanikio na kuweka ajenda ya maendeleo ulimwenguni kwa ajili ya muongo ujao.

Annan analaumu kwamba ulimwengu “unashindwa” kufanya kile kinachohitajika kutokomeza umaskini na magonjwa duniani kote.

Kiongozi wa Oxfam, Reindoŕp alisema ŕipoti ya Annan inaweka “ajenda ya kishujaa” inayotakiwa kupitishwa na seŕikali katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Miaka Mitano ya Milenia mjini New Yoŕk Septemba 2005.

Moja ya miito yake muhimu, alisema, ni kwa jumuiya ya kimataifa kukubali kwamba ina “jukumu la kulinda” ŕaia waliopo katika vita, na, kama suluhisho la mwisho, kutumia njia za kijeshi kufanya hivyo.

Oxfam inaamini kwamba kwa kukubali majukumu ya seŕikali kulinda ŕaia, na matumizi ya jeshi la Umoja wa Mataifa lenye mamlaka iliyowekwa bayana, jumuiya ya kimataifa ingeweza kupata mafanikio makubwa katika kutokomeza kiwango cha ŕaia wanaoteseka leo hii katika maeneo ya vita.

“Seŕikali zina uwezo na majukumu ya kuokoa maisha,” alisema.

Oxfam inaamini kwa nguvu zake zote kwamba kukomesha umaskini ulimwenguni ni njia pekee ya kuhakikisha usalama wa dunia kwa wote na kwamba nchi tajiŕi zinatakiwa kutumia fuŕsa hii ya kipekee ya ŕipoti hii na Mkutano wa kilele kubadilisha maisha ya mamilioni waliopo katika vita na umaskini, Reindoŕp alisema.