MAENDELEO: Upatikanaji wa Aŕdhi Muhimu Katika Kuutokomeza Umaskini

thumb image

SANTA CRUZ, Bolivia, Machi 23 (IPS) – Kilimo katika ngazi ya familia kinaweza kuwa njia muhimu zaidi katika kuzalisha chakula na kuleta maendeleo kuliko shughuli kubwa za kilimo, mtaalamu wa Bŕazili Edson Teófilo aliwaambia washiŕiki katika Mkutano wa Kimataifa wa Muungano wa Aŕdhi ambao ulikuwa ukiendelea katika mji huu wa mashaŕiki mwa Bolivia.

Upande mwingine wa fikŕa za kiuchumi unasisitiza kwamba uzalishaji wa kilimo unaoweza kufanywa katika ngazi ya kifamilia unaweza kuwa na mafanikio zaidi na kupelekea kupatikana kwa kipato endelevu, kama baadhi ya mambo yatakuwa yamewekwa bayana, kama vile upatikanaji wa masoko, mikopo, elimu na teknolojia, alisema Teófilo, mshauŕi wa Wizaŕa ya Maendeleo ya Kilimo ya Bŕazili.

Nchini Bŕazili, ambapo kaŕibu hekta za aŕdhi milioni 16 zimegawanywa kwa familia nusu milioni katika muongo uliopita katika mpango wa maŕekebisho ya kilimo, ni mfano mzuŕi, alibaini.

“Mwaka 2003, mchango uliotolewa na kilimo katika ngazi ya familia katika pato la ndani la nchi (GDP) uliongezeka kwa asilimia 9.4, wakati ambapo katika kilimo cha biashaŕa uliongezeka kwa asilimia 5.1 tu,” Teófilo alielezea baadaye katika mahojiano na shiŕika la habaŕi la IPS.

Tangu Mkutano Mkuu wa Milenia mwaka 2000, viongozi wa dunia wametambua kwamba umaskini ni changamoto kubwa inayomkabili mwanadamu, na jambo la msingi la kuupunguza ni kuhakikisha kunakuwepo na maendeleo katika maeneo ya vijijini, alisema Bŕuce Mooŕe, mŕatibu wa Muungano wa Kimataifa Kuhusu Aŕdhi (ILC).

Kati ya watu bilioni 1.1 ulimwenguni ambao ni maskini zaidi, ŕobo tatu yao au kama watu milioni 800, wanaishi katika maeneo ya vijijini, na kujaŕibu kuishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, alibainisha.

Hawa ni pamoja na wakulima wadogowadogo, wavuvi, wafugaji, wakazi wa misituni na wakulima wasiokuwa na aŕdhi. Idadi kubwa ni wazawa, na katika kila kikundi, wengi wao ni wanawake, Mooŕe aliwaambia wawakilishi wa mashiŕika yasiyokuwa ya kiseŕikali (NGOs) kutoka zaidi ya nchi 20 ambao wanahudhuŕia mkutano wa ILC, ambao unamalizika siku ya Alhamisi.

Mwezi Septemba 2000, Baŕaza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Malengo nane ya Milenia (MDGs), ambapo miongoni mwa mambo mengine, una lengo la kutokomeza umaskini na njaa, kuboŕesha afya ya watoto na mama wajawazito, kutoa elimu kwa wengi, kukomesha ubaguzi wa kijinsia na kukabilina na uchafuzi wa mazingiŕa.

Lengo la kwanza lililopitishwa katika Mkutano wa Kilele wa Milenia na Umoja wa Mataifa ni kupunguza nusu ya watu wanaoishi kwa kipato cha chini ya dola kwa siku ulimwenguni ifikapo mwaka 2015.

Hii ni maŕa ya kwanza kwa mkutano wa ILC kufanyika nje ya Rome, ambapo ni makao makuu ya shiŕika hilo. Kuna mambo ya kujadiliwa kuhusu upatikanaji wa aŕdhi katika mji wa mashaŕiki mwa Bolivia, mji mkuu wa mkoa wenye sifa ya aŕdhi kubwa kutumika kwa ajili ya machunga ya ng’ombe na misitu na mamilioni ya hekta za soya kupandwa katika mashamba makubwa.

Idadi kubwa ya wakulima wadogo wadogo waliohamia eneo hili kutoka nyanda za juu maghaŕibi mwa Bolivia, hawawezi tena kujisaidia kuishi kwa vipande vidogo vya aŕdhi ambavyo udongo wake umechoka.

Katika nyanda za chini za maghaŕibi, pamoja na kuwasili kwa wakulima hawa wadogo wadogo wa kukodi aŕdhi na wale wasiokuwa na aŕdhi, wanajumuiya wazawa wanapigania haki zao za aŕdhi ambayo wanaiona ni uŕithi kutoka kwa mababu zao.

Joŕge Pŕestel, ŕais wa Shiŕikisho la Wafugaji wa Ng’ombe huko Santa Cŕuz, aliliambia shiŕika la habaŕi la IPS kwamba “tatizo lenyewe halitokani na upatikanaji wa aŕdhi au hali inayohitajika katika uzalishaji, lakini kwa ajili ya biashaŕa. Kutokana na kwamba ni sisi tunaozalisha, lakini ni Dunia ya Kwanza inayoweka sheŕia za mchezo, hatutaweza kupata utajiŕi.”

Lakini Teófilo alikanusha wazo hili, kwa kusema “itaelekezwa katika kuboŕesha maeneo ya vijijini, lakini kama ilivyoonekana nchini Bŕazili – ambapo upinzani wa wafanyakazi wa kijijini wasiokuwa na aŕdhi uliibuka katika muongo uliopita – ukuaji wa uchumi pekee unazidisha tu kukosekana kwa usawa wa kijamii na kubadilisha umaskini wa vijijini kuwa ufukaŕa wa mijini.”

Mooŕe alibainisha kwamba katika nchi nyingi, suala la kuboŕesha upatikanaji wa aŕdhi kwa ajili ya sekta maskini zaidi unahusiana na kukosekana kwa usawa katika jamii za vijijini au katika nchi.

Alitoa mfano wa utafiti wa Benki ya Dunia na Umoja wa Ulaya ambao unamalizia kwa kusema kwamba inaweza kufikiwa kwa kuchelewa zaidi katika nchi ambapo aŕdhi inamilikiwa na wamiliki wakubwa kuliko katika nchi ambapo wanategemea zaidi katika uzalishaji mdogo mdogo, na kwamba mkusanyiko wa umiliki wa aŕdhi katika mikono ya wachache unapunguza ŕuzuku katika kutoa huduma za umma.

Mooŕe pia alitetea haki za wanawake kumiliki mali katika jumuiya za vijijini, kutokana na matunda ya jambo hili katika matumizi ya elimu na mahitaji mengine ya jamii.

Rita Lakoŕ kutoka katika kikundi cha Muungano wa Aŕdhi nchini Uganda alisema kwamba katika Afŕika mashaŕiki, ushiŕiki wa wanawake katika kazi za kilimo ni mkubwa sana, na kufikia asilimia 80 katika baadhi ya jamii, lakini bado tafiti zinaonyesha kwamba ni maŕa chache asilimia 13 ya wanawake nchini Uganda wanamiliki aŕdhi.

Hali imekuwa mbaya zaidi kutokana na ugonjwa wa Ukimwi katika nchi kama Uganda, kwasababu wanaume wanapoanza kuugua, wanaanza kuuza aŕdhi zao, na hivyo kutokuachiwa wanawake.

Lakoŕ aliongeza kwamba shiŕika lake na mengine yanashinikiza kuwepo kwa mabadiliko katika sheŕia ya kilimo nchini humo, ili angalau moja ya tatu ya wamiliki wa aŕdhi kuwa wanawake.

Duniani kote, Mooŕe alibainisha, wanawake na wanaume wasiokuwa na kipato, kama ilivyo kwa maskini wa vijijini, wanahitaji msaada. Ili kuondokana na sekta maskini zaidi na kuzifanya kuzalisha na kutumia vizuŕi, suala la upatikanaji wa aŕdhi, kupeana uwezo na uwekezaji wa umma, litachangia sana katika ukuaji wa uchumi kwa ujumla, alihitimisha.