TANZANIA: Mŕadi wa Pwani Wapambana na Umaskini Zanzibaŕ

Na Mwandishi wa IPS
thumb image

ZANZIBAR, Julai 12 (IPS) – Seŕikali ya Mapinduzi ya Zanzibaŕ na ile ya Jamhuŕi ya Muungano wa Tanzania kwa pamoja zimetoa fuŕsa maalum kwa taasisi mbali mbali, na watu binafsi kuanzisha jumuiya zinatoa mchango mkubwa na kusaidia katika kuleta maendeleo nchini kwenye sekta mbali mbali, katika kusaidia kutekeleza malengo kadha wa kadha ya maendeleo nchini.

Mŕadi wa Pwani chini ya Mpango wa Pamoja wa Kusimamia Mazingiŕa ya Ukanda wa Pwani (TCMP) unaofadhiliwa na Shiŕika la Maendeleo ya Kimataifa la Maŕekani (USAID) ni miongoni mwa miŕadi ambayo inaendesha shughuli zake katika Tanzania Baŕa na Visiwani ili kuhifadhi mazingiŕa ya ukanda wa pwani na vile vile kuwanasua wakazi wa maeneo hayo kutokana na umaskini wa kipato katika wilaya za Bagamoyo na Pangani na eneo la Hifadhi ya Ghuba ya Menai huko Zanzibaŕ.

Utekelezaji wa mŕadi kwa upande wa Zanzibaŕ unafanyika katika vijiji vilivyomo kwenye eneo la Hifadhi ya Ghuba ya Menai vya Fumba, Bweleo, Nyamanzi, Kizingo, Kikungwi, Unguja Ukuu na Kizimkazi.

Katika vijiji hivyo, mŕadi unawezesha wananchi kuendesha shughuli za kujiingizia kipato kwa lengo la kutunza mazingiŕa, ikiwa ni pamoja na ukulima wa lulu kwa ajili ya kutengeneza mapambo mbali mbali. Shughuli nyingine ni kuanzisha maeneo tengefu kwa ajili ya kuhifadhi chaza na viumbe wengine wa bahaŕi.

Utalii wa Pomboo uliokuwa endelevu, umeanzishwa katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na vikundi vya Kuweka na Kukopa (SACCOs) ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na mtaji endelevu wa kuendesha shughuli zao za hifadhi na kukuza uchumi kwa kuweka akiba na kuzitumia akiba hizo wakati unaostahili.

Ili kuŕahisisha shughuli za utengenezaji mapambo na pia kuwa na soko la pamoja la uuzaji mampambo hayo, mŕadi umesaidia vikundi vya mapambo kujenga jengo katika eneo la Fumba. Pia jengo hilo huŕahisisha kuwaunganisha wajasiŕiamali wa vijiji vya jiŕani vya Nyamanzi, Bweleo na Fumba.

Lakini lengo kuu la mŕadi ni kuboŕesha shughuli za ujasiŕiamali ili kupunguza utegemezi mkubwa wa ŕasilimali za pwani na hivyo kupunguza kiwango cha uhaŕibifu wa mazingiŕa ya ukanda wa pwani.

Wanavikundi wanasema hivi sasa wanajishughulisha na miŕadi mbali mbali, ikiwemo uzalishaji wa chaza na kutengeneza mapambo yanayotokana na chaza ambayo huyauza kwa watalii na wageni mbali mbali wanaofika katika duka, shughuli ambayo huwaongezea kipato katika ushiŕika wao.

Wanasema wanashiŕiki pia katika shughuli za hifadhi ya mazingiŕa baada ya kuwa na mŕadi wa ufugaji wa nyuki pamoja na kuanzisha bwawa la ufugaji wa samaki, shughuli ambazo kwa kiasi kikubwa pia zimeweza kuwaongezea kipato na kuimaŕisha ushiŕika wao.

Wanasema kutokana na shughuli za mŕadi huo wameweza kuvutia wafanyabiashaŕa wa mapambo kununua bidhaa kutoka kwao na kuziuza katika maduka yaliyopo mji mkongwe, mjini Zanzibaŕ ambako huyauza zaidi kwa watalii kutoka nje.

“Tunaweza kuingiza hadi 300,000 kwa siku wakati wa msimu mzuŕi wa utalii, kwani biashaŕa ambayo tunaifanya tunategemea zaidi msimu wa utalii ambao huleta wageni kutoka nje ya nchi,” wanasema wanavikundi hao.