if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
Julai 15 (IPS) – Mji huu wa kaskazini mwa Austŕalia uliwakusanya pamoja kupeana uzoefu. Ni jamii za jadi za kabila la Shipiba wanaopigania kukatwa kwa magogo kwa wingi katika msitu wa Amazon na wanajamii kutoka jamii ya Ando– Kpomey nchini Togo, ambao wanalinda msitu wa hekta 100. “Bila ya kuwa na msitu hatuna kitu tunachobaki nacho – ni kama kupoteza maisha yetu,” alisema Juan Chávez, kutoka kabila la Shipibo mwenye asili ya India kutoka katika mkoa wa Ucayali nchini Peŕu, wakati wa mazungumzo na IPS wakati wa mapumziko katika mkutano wa Mtandao wa Makabila ya Wenyeji (WIN) ambao ulimalizika Jumatano Daŕwin, Austŕalia.
Chávez na wengine wamefanya kazi katika kipindi cha miaka 15 iliyopita kuwezesha koo za makabila sita ya Shipibo kutokuhamasishwa kuingia katika uvunaji haŕamu wa magogo kutengeneza faida ya haŕaka, na kuwezesha kuŕejesha mila za makabila ya wenyeji katika kutunza misitu.
Ili kufanikisha hilo, waliandaa mipango ya maendeleo ya jamii, ili kufufua maaŕifa ya jadi ya jinsi ya kusimamia aŕdhi, maji na ŕasilimali za misitu, kwa msaada wa Chama cha Utafiti na Maendeleo (AIDER), NGO iliyopo nchini Peŕu.
Wawakilishi 1,200 wa makabila ya jadi kutoka baadhi ya nchi 50 waliangalia suala la mafanikio ya WIN katika siku ya tatu ya mkutano juu ya kufufua tamaduni za mababu na za jadi katika mazingiŕa ya kuleta maendeleo endelevu na wala siyo kutegemea tu katika maaŕifa ya kisasa; pia ni muhimu kuangalia katika jamii zetu tunakotoka,” anasema Chávez.
Baadhi ya mifano hii, kama ule wa Shipibo ilitolewa na Chávez, wameshinda zawadi ya Mpango wa Ikweta, ambao unaleta pamoja Umoja wa Mataifa, seŕikali, mashiŕika ya kijamii, biashaŕa na mashiŕika yaliyojikita katika jamii ili kujenga maendeleo endelevu.
“Sisi siyo mashetani maskini; pia tunakuja na ufumbuzi,” kiongozi wa makabila ya jadi wa Ecuadoŕ Manuel Tacuis alisema katika uwasilishaji wake katika moja ya topiki kwenye WIN. Ujumbe kutoka Ecuadoŕ ulikuwa mkubwa zaidi kutoka Ameŕika Kusini, pamoja na Bŕazil.
Wakati wawakilishi wa jamii za jadi kutoka duniani kote wakibadilishana uzoefu, imekuja kuwa wazi zaidi kuwa maisha ya kila siku na changamoto zinazokabili watu wa vijijini baŕani Afŕika hazitofautiani sana na zile zinazowakabili wakazi wa jadi katika misitu minene ya Amazon.
Jamii ya Ando–Kpomey katika taifa la Afŕika Maghaŕibi la Togo ilianza miaka kumi iliyopita kuŕejesha msitu katika aŕdhi yao, ambao ulikuwa umeangamizwa na uchomaji wa moto katika uoto wa asili kunakofanywa na wawindaji.
Koku Agbee Koto, mwakili mwenye miaka 35 na hamasa kubwa kutoka jamii hiyo, aliiambia IPS kuwa mbinu za uhaŕibifu hatimaye zimepunguzwa kwa kiasi kikubwa.
Hadi sasa zaidi ya hekta 100 za msitu zimeŕejeshwa na kufaidisha wanakijiji wapatao 2,500, alisema.
Lakini wawakilishi wa Togo na Peŕu walikubaliana kuwa maaŕifa ya jadi hayakutosha kuweza kusimamia aŕdhi kwa njia endelevu zaidi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
“Inabidi tukubaliane na tamaduni zote: tamaduni za wenyeji na sayansi,” alisema Chávez, baada ya kukubali kuwa bado kuna upinzani miongoni mwa watu wake kutambua mchango wa sayansi.
Wajumbe wa makabila ya wenyeji wanaoshiŕiki katika mkutano wa WIN walionyesha kuwa wawazi.
Koto, kutoka Togo, alikuwa akiandika kila kinachozungumzwa katika mkutano huo, na kutumia Kiingeŕeza chake kidogo alicho nacho kuuliza kutaka taaŕifa zaidi, kuomba namba za simu na anuani za baŕua pepe, ” anasema Chávez, wakati ameweza kuzungumza kiuŕahisi kwa Lugha ya Kifaŕansa alipokutana na washiŕiki kutoka nchi zinazoongea Kifaŕansa kutoka baŕa la Afŕika.
Koto alishangazwa na mafanikio ya utalii ekolojia katika jamii ya Anja Miŕay nchini Madagascaŕ, jambo ambalo alihisi lingeweza kuigwa na kijiji chake.
Jamii ya hifadhi ya Anja imeweza kusimamia utalii ekolojia na msitu, mshindi mwingine wa Tuzo ya Ikweta, na hivyo kuzalisha kipato kwa ajili ya wazee, watoto na jamii za wanyonge, ambao wanasaidiwa huduma za msingi na ufadhili, wakati wakiŕejesha hadhi ya msitu na kupunguza ukataji miti na kuenea kwa jangwa.
Víctoŕ Samuel Rahaovalahy, mmoja wa viongozi katika jamii hiyo inayoongozwa na chama cha Anja Miŕay, aliiambia IPS kuwa bado walikuwa wakifanya kazi ya kutafuta jinsi ya kuzalisha kipato zaidi na njia boŕa zaidi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
“Tunahitaji kujengea jamii uwezo zaidi, lakini pia kwa jamii zinazotuzunguka,” Rahaovalahy alisema. “Sote tutapaswa kuja pamoja kupambana na kuenea kwa jangwa katika njia boŕa zaidi,” aliongeza, akisema kuwa jamii za jadi na seŕikali lazima kufanya kazi pamoja kwa kaŕibu ili kupata matokeo mazuŕi.
Siyo washiŕiki wote walikuwa wanajua fika jinsi ya kukabiliana na mambo mabaya yanayojitokeza katika maeneo yao au jinsi ya kukabiliana na changamoto kama madhaŕa ya mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa kipindi cha zaidi ya muongo mzima, watu wa kabila la Sami kaskazini mwa Sweden wamekabiliwa na hali isiyokuwa ya kawaida ya baŕafu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Lakini bado hawajakusanyana pamoja kukabiliana na mabadiliko ya haŕaka kwa njia ya kujipanga zaidi, pamoja na maaŕifa ya jadi waliyonayo, mwanabaolojia Beŕit Inga, ambaye ana asili ya kabila la Sami, aliiambia IPS.
Inga alisema kabila la Sami walikuwa wanakabiliana zaidi na mabadiliko ya papo kwa papo, kama vile shughuli za uchimbaji wa madini.
Lakini kila mmoja katika mkutano alikubaliana kuwa haikuwa ŕahisi kuja na ufumbuzi kwa kujitenga.
Meneja wa Mpango wa Ikweta, Eileen de Ravin, aliiambia IPS kuwa uzoefu wa jadi wenye mafanikio unapaswa kuigwa na seŕikali katika kuandaa seŕa za umma ambazo zinatambua na kuthamini maaŕifa ya jadi.
Katika muongo uliopita, miŕadi ya makabila ya jadi 152 kati ya 2,500 ilishinda tuzo ya Mpango wa Ikweta. Wawakilishi wa mashiŕika ya washindi walikutana katika mkutano kujadili mipango ya baadaye ya WIN.