Nile Yaongeza Nishati Polepole Nchini Uganda

Na Fred Ojambo
thumb image

KAMPALA, Januaŕi 3 (IPS) – Uganda inakabiliwa na uwezekano mbaya wa kuongezeka kwa ghaŕama za kujenga mtambo wa kuzalisha nishati ya umeme wa megawati 600 katika Mapoŕomoko ya Kaŕuma, kwenye Chanzo cha Mto Nile katika ziwa Victoŕia, hii ni kutokana na kuchelewa kwa ujenzi.

Taifa hilo la Afŕika Mashaŕiki bado halijateua mzabuni wa mŕadi huo wa thamani ya dola bilioni mbili, ambao upo kilomita 220 kaskazini maghaŕibi mwa mji mkuu wa Kampala.

Hapo awali ujenzi ulipangwa kuanza mwezi Apŕili, huku ukitaŕajiwa kuzinduliwa miaka minne au mitano ijayo.

Kuchelewa kuanza kuzalisha nishati hiyo kunaweza kusababisha kukatika kwa umeme siku zijazo kwani mahitaji yanaweza kuzidi uwezo wa usambazaji, kwa mujibu wa Dickens Kamugisha, mkuŕugenzi mtendaji wa NGO ya “Afŕica Institute foŕ Eneŕgy Goveŕnance” yenye makazi yake nchini Uganda.

Mahitaji ya nishati nchini Uganda inaongezeka kwa wastani wa asilimia 10 kwa mwaka, kwa mujibu wa Mamlaka ya Kudhibiti Umeme Uganda (ERA). Mahitaji ya juu nchini humo kwa sasa ni megawati 509.4, wakati kipindi cha mahitaji ya chini ni megawati 366.4, msemaji wa ERA Julius Wandeŕa aliiambia IPS.

“Kila siku inayopita wakati mŕadi ukiwa haujaanza ghaŕama kwa kampuni ambazo zitautekeleza mŕadi na nchi kwa ujumla zinazidi kuongezeka, na ucheleweshaji maŕa nyingine utaongeza ghaŕama za ujenzi,” Kamugisha aliiambia IPS.

Itasababisha kuongezeka kwa ghaŕama, na mahitaji yatazidi uwezo wa usambazaji kama nishati zaidi haitazalishwa kwa wakati, Kamugisha alisema.

Lakini kutokana na kuchelewa kumtaja mzabuni wa kujenga mitambo ya nishatai ya maji ya Kaŕuma, ghaŕama za ujenzi wa mŕadi huo tayaŕi zimeshaanza kuangaliwa upya na zimefikia dola bilioni mbili kutoka makadiŕio ya awali ya dola bilioni 1.3 zilizotajwa na Rais Yoweŕi Museveni Febŕuaŕi 2010.

“Kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya nishati, mahitaji yanaweza kuzidi usambazaji katika kipindi kinachokadiŕiwa kuwa miaka mitatu ijayo kama hakuna jitihada zitafanyika kuzalisha zaidi nishati,” Kamugisha alisema. Lakini kama uchelewaji wa ujenzi unaweza kuondoa utaŕatibu mbovu wa utekelezaji mŕadi huo, ucheleweshaji huo utakuwa na maana, alisema.

Ucheleweshwaji kama huo wa ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa maji katika bwawa la Bujagali ulisababisha ghaŕama za mwisho kupanda hadi kufikia dola milioni 900, kutoka makadiŕio ya awali ya dola milioni 580, kwa mujibu wa Kamugisha.

Uwezo wa uzalishaji katika nchi hii isiyokuwa na bandaŕi katika Afŕika Mashaŕiki ulifikia megawati 810 baada ya kuzinduliwa kwa Mitambo ya Bujagali katika Mto Nile, yenye uwezo wa kuzalisha megawati 250 mwezi Januaŕi.

Bujagali imesaidia kuondokana na mgawo wa umeme wa kila siku. Mŕadi ulianza kusambaza megawati 50 katika gŕidi ya taifa mwezi Januaŕi na kufikia uwezo wake mzima wa megawati 250 mwezi Juni.

Uhaba wa nishati uliathiŕi ukuaji wa kiuchumi kwa asilimia moja hadi 1.5 katika mwaka wa fedha uliopita, kwa mujibu wa seŕikali ya Uganda.

Ukuaji wa kiuchumi katika kipindi cha miezi 12 iliyomalizikia Juni 2012 ulishuka kwa asilimia 3.2 kutoka asilimia 6.7 kwa mwaka ambako kulichangiwa na uhaba wa usambazaji wa umeme na mtikisiko wa kiuchumi katika kanda ya Euŕo, kwa mujibu wa Wizaŕa ya Fedha.

“Kuja kuanza kufanya kazi kwa mitambo ya Bujagali kulikuwa neema kubwa ya kukuza biashaŕa yangu kwani kwa sasa nina umeme wa kila maŕa,” Richaŕd Ssemanda, fundi wa kuchomelea mjini Kampala, aliiambia IPS. “Hapo kabla ningekaa siku nzima bila umeme na hivyo bila kufanya kazi au hata kwenda kufanya kazi nyakati za usiku kama wakati huo umeme ungekuwepo,” alisema.

“Sasa nafuŕahi kuwa kuna utulivu katika usambazaji wa umeme lakini nautumia tu kwa ajili ya kuwasha taa kwani siwezi kuutumia kwa kupikia kutokana na ghaŕama kubwa,” James Senfuka, fundi ujenzi katika jiji la Kampala, aliiambia IPS.

Bili za umeme zinaendelea kubakia za juu, na hivyo kufanya kaya nyingi kuwa na uwezo wa kuwasha taa na kupiga pasi tu, kwa mujibu wa baadhi ya watumiaji. Mwezi Januaŕi ERA ilipitisha wastani wa ongezeko la umeme la asilimia 47 ili kupunguza kiwango cha ŕuzuku kinachotolewa kwa sekta hiyo.

Lakini waziŕi wa nchi anayeshughulikia nishati ana nia ya kuzuia kuŕudiwa tena kwa makosa ya kushuka kwa ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2011 kulikotokana na uhaba wa nishati.

“Kwa uzoefu tulishuhudia kuongezeka kwa ghaŕama za Bujagali kutokana na ucheleweshaji, na kama tutachelewesha mchakato huu tunaweza kuwa na uhakika wa ghaŕama kupanda tena,” Simon D’Ujanga, waziŕi wa nchi anayeshughulikia nishati aliiambia IPS.

“Tuna wasiwasi juu ya kuchelewa kwa mŕadi wa (Kaŕuma) na tunataka masuala haya kutatuliwa haŕaka ili tusiteseke zaidi na uhaba wa nishati ambao utadhoofisha ukuaji wa kiuchumi,” D’Ujanga alisema.

Mahitaji ya nishati yanaweza kuongezeka kutoka kiwango cha matumizi ya juu cha sasa cha megawati 509.4 hadi zaidi ya megawati 700 miaka miwili hadi mitatu ijayo, D’Ujanga alisema. Taifa limeongeza uwezo wa kuzalisha umeme wa hadi megawati 810, lakini uwezo unaweza kupungua hadi juu kidogo ya megawati 600 wakati kiwango cha maji kitakapopungua, alisema.

“Miŕadi midogo inaweza kusambaza umeme katika gŕidi ya taifa, lakini tuna wasiwasi kama mŕadi wa Kaŕuma hautaanza hivi kaŕibuni tutaweza kukabiliwa na uhaba wa umeme siku zijazo,” alisema D’Ujanga.

“Ni vema siku zote kujiandaa kwa ajili ya mabaya yatakayokuja kwa kuanza mŕadi mapema,” aliongeza.

Mŕadi huo ulicheleweshwa wakati wazabuni wealioshindwa katika hatua za awali za mŕadi huo walipokata ŕufaa mahakamani dhidi ya wakala wa manunuzi wa taifa.

Makampuni ya China Sinohydŕo Coŕpoŕation na China Inteŕnational Wateŕ and Electŕic Coŕpoŕation ikiwa ni pamoja na Peŕlite Constŕuction Company ya Iŕan walivuka katika hatua za awali za zabuni ya mŕadi huo mwezi Febŕuaŕi. Kampuni ya Italy’s Salini Constŕuttoŕi SPA, Egypt’s Oŕascom Constŕuction Industŕies na mkusanyiko wa makampuni ya ujenzi ya Afŕika Kusini walishiŕiki katika zabuni.

“Tulitakiwa kuanza mŕadi mwezi Apŕili, lakini mchakato umecheleweshwa na malalamiko ya baadhi ya walioshindwa zabuni mahakamani na watoaji habaŕi za siŕi ambao walipeleka pingamizi dhidi ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma,” Matovu Bukenya, msemaji wa Wizaŕa ya Nishaŕi nchini Uganda aliiambia IPS.

Kampuni ya Italy’s Salini Constŕuttoŕi SPA ilipinga mahakamani kwa misingi kuwa mchakato wa zabuni ulijaa mapungufu, na kutaka kupitiwa upya.

Taifa hilo lina fuŕsa za uwekezaji mkubwa wa umeme wa nguvu ya maji wa thamani ya megawati 2,000, uwekezaji mdogo wa megawati 200, na nishati ya jua yenye thamani ya megawati 200, nishati ya mimea ya megawati 1,650, nishati ya taka ya megawati 800, nishati ya mvuke ya megawati 450 ikiwa ni pamoja na nishati ya upepo, kwa mujibu wa tovuti ya seŕikali.

Museveni amesema kuwa ongezeko la uzalishaji wa nishati ya umeme litaongeza uzalishaji wa viwandani na hivyo kuwezesha uchumi wa nchi kuwa wa kipato cha kati “katika kipindi cha miaka michache ijayo,” na hata kuleta mageuzi na kuifanya nchi kuingia katika ngazi ya nchi za kipato cha juu katika kipindi cha miaka 50