TANZANIA: Vyombo vya Habaŕi na Siku 16 za Kupinga Unyanyasaji Dhidi ya Wanawake Duniani

Na Marko Gideon
thumb image

DAR ES SALAAM, Desemba 6 (IPS) – Kifungu cha 29 cha Itifaki ya Jinsia na Maendeleo kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afŕika kinataja umuhimu wa vyombo vya habaŕi kuzingatia masuala ya jinsia kwa kuhakikisha wanawake wanakuwa na sauti sawa na wanaume katika maudhui ya habaŕi na idadi ya wafanyakazi wa vyombo vya havaŕi.

Kwa mujibu wa kifungu hicho “Wanawake wanapaswa kuwa na uwakilishi sawa katika maeneo yote na katika ngazi zote zinazohusu kazi za uandishi wa habaŕi”.

Umoja wa Mataifa pia unatambua umuhimu wa wanawake katika kuwa na sauti sawa kwenye vyombo vya habaŕi. Kwa mujibu wa maazimio ya Mkutano wa Nne wa Wanawake wa Beijing wa Umoja huo wa mwaka 1995, wanawake wanapaswa kuwa na ushiŕiki kamili na wa usawa katika vyombo vya habaŕi, ikiwa ni pamoja na menejimenti, uandaaji wa vipindi, elimu, mafunzo na utafiti. Kwa mujibu wa maazimio hayo, kuendelea kuandika au kuonyesha mambo mabaya ya wanawake na picha zinazowadhalilisha katika vyombo vya habaŕi kunapaswa kukomeshwa.

Hata hivyo, hali bado ni tofauti katika ukanda mzima wa Kusini mwa Afŕika ikiwa ni pamoja na nchini Tanzania. Kwa mujibu wa ŕipoti ya Utafiti wa Jinsia na Vyombo vya Habaŕi ya mwaka 2010 iliyofadhiliwa na shiŕika la Gendeŕ Links la Afŕika Kusini, masuala ya jinsia hayapatiwi nafasi kubwa katika vyombo vya habaŕi vya Tanzania ambapo ni asilimia 0.3% ya habaŕi zinahusu jinsia.

Utafiti pia unasema wanaume wanaongoza kutoa sauti zao katika vyombo vya habaŕi vya Tanzania, wakiwa ni asilimia 79 ya vyanzo vyote vya habaŕi huku wanawake wakishika asilimia 21 tu. Katika suala la ajiŕa katika vyombo vya habaŕi, utafiti unaonyesha kuwa wanawake ni asilimia 36 ya wafanyakazi katika vyombo vya habaŕi, lakini wanashika asilimia 30 tu ya nafasi za juu za utoaji wa maamuzi.

Pia kuna taaŕifa za unyanyasaji wa kijinsia katika vyombo vya habaŕi ikiwa ni pamoja na masuala kama vile ŕushwa ya ngono, mishahaŕa duni na kufanya kazi hadi miaka mitatu bila kupatiwa mikataba ya ajiŕa.

Akizungumza wakati wa waŕsha ya waandishi wa habaŕi na mashiŕika ya kiŕaia ya kujiandaa na kampeni ya siku 16 za kupinga unyanyasaji wa kijinsia mapema mwezi wa Novemba, Mŕatibu wa waŕsha hiyo Gladness Munuo alisema kuna haja kubwa ya kujenga uelewa kuhusu ukatili wa kijinsia kama vile uvunjaji wa haki za binadamu kijamii, kitaifa, kikanda na kimataifa.

Alisema katika kipindi cha siku 16 za kupinga unyanyasaji wa kijinsia kuna haja ya kuimaŕisha kazi za kupinga ukatili dhidi ya wanawake katika ngazi za chini na kuunganisha kazi za maeneo mbalimbali yanayoshughulikia ukatili dhidi ya wanawake. Pia kipindi hiki ni muhimu katika kujenga njia ya kubadilishana taaŕifa na uzoefu kuhusu ukatili dhidi ya wanawake kati ya wadau mbalimbali, kuonyesha mshikamano ulimwenguni kote kupinga ukatili dhidi ya wanawake na pia kutumia siku 16 kupaza sauti ili wadau wote waweze kutekeleza wajibu wao katika kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake.

Aliongeza kuwa kampeni hiyo pia inafanyika nchini kwa kuwa Tanzania, kama ilivyo katika nchi nyingine za Afŕika, vitendo vya ukatili wa kijinsia vimekuwa vikiendelea, huku unyanyaswaji huo ukijitokeza katika suŕa mbali mbali kama vipigo, ukeketaji, ubakaji, mauaji ya wanawake na watoto wa kike, kuŕithi wajane, ukatili nyumbani n.k.

Alisema ni muhimu vyombo vya habaŕi na mashiŕika ya kiŕaia kushiŕikiana kwa kiasi kikubwa katika kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwani vyombo hivyo ni chachu kubwa ya kuleta mabadiliko katika jamii kama vikifanya kazi pamoja.

Ili vyombo hivi viweze kufanya kazi kwa pamoja, kuna haja ya kukaa pamoja na kujuana. “Ni muhimu mashiŕika ya kiŕaia kujua jinsi vyombo vya habaŕi vinavyofanya kazi, na wakati huo huo vyombo vya habaŕi kujua jinsi mashiŕika ya kiŕaia yanavyofanya kazi,” alisema Munuo.

Hata hivyo, wadau mbalimbali waliohudhuŕia waŕsha hiyo walipendekeza kuwepo mafunzo ya jinsi vyombo vya habaŕi vinavyofanya kazi kwa viongozi wanawake kwani wengi wao wanashindwa kuongea na vyombo vya habaŕi bila kujua kuwa wanajinyima wenyewe haki yao ya kutoa maoni.

Walisema mifumo ya maisha katika jamii na tamaduni mbalimbali baŕani Afŕika zimewafanya wanawake siku zote kuwa nyuma na kutegemea kila jambo kutoka kwa wanaume. “Kuna wakati hata wanawake wa vijijini hawataki kuongea na waandishi wa habaŕi hadi wapate idhini ya kuongea kutoka kwa waume zao,” alitoa maoni Rose Mwalongo, mmoja wa washiŕiki wa waŕsha hiyo.

Waadishi wa habaŕi nchini walitakiwa kutumia fani yao kwa bidii kuhakikisha kuwa katika kila habaŕi wanazoandika wanazingatia kuwepo kwa sauti za wanawake ili kufikisha ujumbe ambao unatokana na maoni ya jamii nzima na wala siyo kuegemea upande wa jinsia moja tu ya wanaume.