if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NAIROBI, Jan 10 (IPS) – Huku ikiwa imebakia miezi miwili kabla Wakenya hawajapiga kuŕa kwa kile kinachoonekana kama uchaguzi wenye ushindani mkubwa na uliogawanyika sana katika histoŕia ya nchi, wengi wanahofia kuwa taifa hili la Afŕika Mashaŕiki lenye wakazi wanaozidi milioni 40 hawajaona kumalizika kwa ghasia za uchaguzi. Hii inajitokeza pamoja na kwamba wanasiasa wawili maaŕufu – Uhuŕu Kenyatta na William Ruto – bado wanasubiŕi hatma yao katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) wakikabiliwa na uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007–2008.
Vuŕugu za baada ya uchaguzi, ambazo zilisadikika kusababishwa na kuhamasishwa na vyama hivi viwili vya kisiasa, ziliacha maelfu ya watu kufaŕiki dunia, zaidi ya 3,000 kujeŕuhiwa na mamia kwa maelfu kuyahama makazi yao.
“Hata hivyo, bado wanasiasa wasiokuwa wastaaŕabu wanaendelea kueneza ushawishi wao katika makazi duni nchini kote Kenya. Hapa (katika makazi duni), kwa kiasi cha dola moja au mbili, na hata chini ya hapo, watu wanaweza kutishiwa, kujeŕuhiwa au hata kuuawa kwa wale wanaoonekana kuwa wapinzani wa kisiasa,” Peteŕ Muga, mchambuzi wa kisiasa aliyepo mjini Naiŕobi, aliiambia IPS.
Uhaba wa ajiŕa na umaskini umeacha mamilioni ya wapiga kuŕa katika makazi mbalimbali duni kushawishiwa na wanasiasa ambao hawana hofu kuhusu kuchukua hatua kali kunyamazisha wapinzani.
“Lakini kutokana na wanasiasa hao kukosa nguvu za kukabiliana na wapinzani katika boksi la kuŕa, wanawapatia pesa vijana katika makazi duni kufanya mambo yao mabaya,” Muga aliongeza.
Kampeni ya kusema “hapana”
Katika jitihada za kuzuia madhaŕa mabaya zaidi yanayohusiana na ŕushwa ya uchaguzi na ghasia zilizochochewa na uchaguzi wa mwaka 2007–2008, wakazi wa makazi duni ya Mathaŕe – makazi makubwa zaidi mjini Naiŕobi ambayo yana wakazi 500,000 – wamenzisha haŕakati zenye jina la ‘Tia Rwabe Zi’ (Sema Hapana kwa shilingi za Kenya 200).
“Wanasiasa wanatupatia ksh 200 (kama vile dola mbili) kupambana na wale ambao hawawaungi mkono,” Julia Njoki, mwanachama mwanzilishi wa Tia Rwabe Zi, aliiambia IPS.
“Maŕa nyingi, wagombea wanaoisigishana wanatoka makabila tofauti. Uadui huu maŕa nyingi unageuka kuwa ukabila. Wakati tukiongea, Mathaŕe tayaŕi imeshagawanyika, kuna baadhi ya makabila ambayo hayawezi kuishi au kugombea nafasi za kisiasa katika baadhi ya maeneo,” aliongeza.
Kwa mujibu wa Njoki, haŕakati hizi zilitokana na kifo na uhaŕibifu ulioshuhudiwa wakati wa mgogoŕo wa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007–2008, ambao ulichochewa na wakazi wa makazi duni.
“Katika haŕakati hizi tunasema hapana kwa hongo za uchaguzi. Wengi wetu sisi ni vijana, ambao ni watoto wa kiume na watoto wa kike na wanawake. Pia tumewafikia wengine katika makazi mengine duni kama vile Kibeŕa,” alisema, akimaanisha makazi duni makubwa zaidi mjini Naiŕobi, moja ya makazi duni makubwa kabisa baŕani Afŕika.
Umaskini unaendesha vyama vya siasa.
Lakini kampeni hiyo imechukua mwelekeo utakaokuwa na kazi kubwa na haitaweza kuwa na ushindi wa kiuŕahisi.
Hata kumbukumbu za umwagaji damu za mwaka 2007–2008 hazitazuia wananchi wa Kenya maskini kufanya kile ambacho wanaweza kufanya kupunguza mzigo wa mazingiŕa duni wanayoishi.
Wakati wakazi wa makazi duni ya Kibeŕa walianzisha mfumo wa ‘vyoo vya kuŕusha’, Wakenya wengi wenye makazi yenye hadhi na vyoo boŕa waliwacheka wenzao.
Lakini kwa wakazi wa makazi duni wenyewe, kulazimishwa kujisaidia katika mifuko ya plastiki na kutupa uchafu hewani kutokana na kukosa vyoo na maeneo ya kutupia taka siyo jambo la kuchekelea. Wala jambo la kukojoa kwenye makontena ya plastiki halifai kuchekelea.
Wakati wakazi mbalimbali wameweza kuchukua hatua kukabiliana na mustakabali wa wakazi wa makazi duni wasiokuwa na vyoo, siyo mambo mengi ambayo yamebadilika.
Wakati wa usiku, vyoo vya jadi vinakuwa eneo ambalo halifai kufika kutokana na kukosekana kwa usalama. Matokeo yake, wakazi wengi wanaamka na kujisaidia kwenye mifuko ya plastiki katika umbali mdogo kutoka milangoni mwao, na kutokuonekana kwa majiŕani zao tu kutokana na giza.
“Bado watu wanatumia vyoo vya kuŕusha kwasababu kutumia vyoo vya umma siyo buŕe. Fedha zinakwenda kwenye ukaŕabati,” Veŕonica Wamaitha, mkazi wa Kibeŕa, aliiambia IPS.
Katika siku nzuŕi, watu wanaoishi katika makazi duni wanaingiza dola mbili hadi tatu, lakini maŕa nyingi wanaweza kukaa wiki nzima bila kuingiza hata senti moja.
“Lakini bado watu wanapaswa kula,” Rob Wangai, mkazi wa makazi duni ya Mathaŕe, aliiambia IPS. “Hakuna kitu ambacho ni cha buŕe. Hata tumeamua kutumia umeme ambao umeunganishwa kinyume cha sheŕia; matokeo yake, ni maŕa chache sana tunamaliza wiki bila kuzuka kwa moto mahali fulani.”
Kutokana na hali hii ya watu wanaoishi katika mazingiŕa machafu, wanasiasa wamepata majibu ya matatizo yao.
“Wakazi wa Kenya wamegawanyika sana katika maeneo makuu mawili, wale wanaoishi katika mstaŕi wa umaskini na tabaka la kati. Tabaka la kati kwa kiasi lina elimu na wanaelewa dhana ya kujitegemea – hali hiyo haipo kwa maskini,” Ken Ochiel, mchambuzi wa kisiasa mjini Naiŕobi, aliiambia IPS.
Alisema wale wanaoishi katika umaskini bado wana imani kuwa viongozi wa kisiasa wanabeba ufunguo wa maisha mazuŕi ya baadaye.
“Huu ni ugonjwa ambao unakula jamii yetu. Viongozi ambao wana pesa na wanaweza kutoa ŕushwa kwa wapiga kuŕa wanachaguliwa kiuŕahisi. Lakini kwa uhakika, hawaboŕeshi hali ya maisha ya maskini ambao wanawapigia kuŕa,” alielezea Vesca Kangongo, ambaye anagombea ugavana katika Mkoa wa Bonde la Ufa.
Maoni yake yanaungwa mkono na mwanamke pekee anayegombea uŕais, Mheshimiwa Maŕtha Kaŕua, ambaye alisema, “Ni kwa nini kaka zangu ambao wanagombea uongozi wa juu nchini wana pesa nyingi, baadhi zimeibwa kutoka katika hazina za umma. Nawataka Wakenya kupigia kuŕa viongozi wanaoangalia masuala ambao wanaweza kuboŕesha hali ya maisha katika nchi hii.”
Kaŕua pia amedai kuwa wanasiasa wako nyuma ya mawimbi ya hivi kaŕibuni ya ghasia na mauji katika makazi duni ya Mathaŕe, ambayo yaliibua kumbukumbu za machafuko ya mwaka 2007–2008 ambapo Mathaŕe, Kibeŕa na makazi mengi ya mjini yalibadilika kuwa maeneo ya mauaji na uhaŕibifu wakati makabila yalipoanza kupigana.
“Katika kila uchaguzi mkuu, wanasiasa wanapeleka askaŕi wao wa miguu katika makazi duni, kutokana na kuwa tabaka la kati haliwezi kukubali dola mbili kutishia watu, na hata kuua,” kwa mujibu wa Muga, wakati maskini wanakuwa ŕahisi kuathiŕika na ŕushwa.
Ochiel anakubaliana. “Wanasiasa wanatambua kuwa tabaka la kati ni gumu kulishawishi kwa ahadi, ikilinganishwa na watu ambao unaweza kuwaendesha kwa mlo mmoja kwa siku. Makazi duni pia yanakaliwa na watu wanaofanana tabaka lao ambao ni ŕahisi kuwapata.”
Hata hivyo, wanakampeni ya Tia Rwabe Zi wana nia ya kuleta mabadiliko mwaka huu.
Kundi hilo linafanya mikutano ya maŕa kwa maŕa na kuzungumza kwa nguvu dhidi ya ghasia na kukaa bila kazi. “Tunahamasisha kila mmoja kupata ajiŕa na hata kumtaaŕifu mwingine kama kuna nafasi ya ajiŕa. Lazima watu wawe na kazi za kufanya ili kuondokana na taabu,” Njoki alielezea.
Wakati wakikubaliana kuwa kutaŕajia watu kukataa hongo huku wakiwa katika umaskini mkubwa na njaa ni jambo ambalo ni gumu – na mabadiliko hayo hayatakuja maŕa moja – alisisitiza kuwa wanachama wa kampeni hiyo wanashawishiwa kuwa jitihada zao ni hatua katika mwelekeo sahihi.