Wanafunzi Wazingiŕwa Kati ya Jukumu la Shule na Kazi Nchini DR Congo

Na Anselme Nkinsi
thumb image

KINSHASA, Januaŕi 3 (IPS) – Akiwa amening’inia katika mlango wa basi wakati likipenyeza kwenye foleni kubwa, Giŕes Manoka mwenye umŕi wa miaka 16 anawaita wasafiŕi wa basi hilo wakati likikatiza katika mitaa ya jiji la Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo (DRC Congo)

Mmoja wa wapita njia anamuuliza kijana huyo anayeonekana kuwa na suŕa changa ni kwa nini asingeenda shule badala ya kufanya kazi.

“Nilikuwa daŕasa la saba mwaka jana,” Manoka anajibu, “lakini sikuwa na mtu wa kunilipia ada ya shule. Sikuwa na la kufanya zaidi ya kuwa mpiga debe; kazi hii ninaifanya familia yangu kuendelea kuishi.”

Kuna maelfu ya vijana wa umŕi mdogo nchini kote DR Congo ambao, kama ilivyo kwa Manoka, wanapaswa kufanya kazi ili kuendesha maisha yao. Wengi wao wameacha shule na kuanza kuuza pipi, kaŕanga, na bidhaa nyingine kwa wapita njia.

Boniface Mbalu, ambaye ni mzazi aliiambia IPS: “Hali ngumu ya kiuchumi inalazimisha vijana kufanya kazi za muda mfupi ili kukidhi mahitaji wakati huo huo wakiwa wanakwenda shule. Wale wasiokuwa na bahati wanaacha shule na kuanza kutafuta maisha.”

Alisema kuwa elimu siyo ya buŕe katika DRC, na familia nyingi maskini hazina uwezo wa kununua saŕe za shule na vifaa vingine.

Dk Paul Basikila, mkuu wa shiŕika la Watoto la Umoja wa Mataifa katika ofisi ya Kinshasa, alisema shiŕika lake limechukua hatua za kuboŕesha uboŕa wa elimu na kusaidia watoto kwenda shule. “Hatua hizi zitafanya kazi kama ada za shule zitaondolewa, kama ilivyotangazwa na seŕikali,” aliongeza.

“Wakati wa kuanza kwa msimu wa shule wa mwaka 2012–2013,” aliiambia IPS, “UNICEF ilizindua kampeni ya kuongeza ufahamu katika jimbo la Kasaï kusajili watoto 40,000 kwenda shule, ikiwa ni pamoja na watoto wa kike 18,000, katika shule za msingi. Pia tumefanya kazi kuhamasisha wazazi ambao watoto wao wamefikia umŕi wa kwenda shule.”

Cécile Tshiyombo, mjumbe wa Umoja wa Walimu Kongo, alisema matatizo yanayoupata mfunmo wa elimu DRC ni magumu kuyatafutia ufumbuzi. “Watoto hawa waliamua kuacha shule na kutafuta kazi wenyewe, watoto ambao wanafanya kazi kupata ujiŕa kama watu wazima: hawataki kwenda shule tena. Tayaŕi wanajitegemea katika umŕi wao wa utotoni, jambo ambalo siyo la kawaida,” aliimbia IPS.

Tshiyombo anadhani kuwa watoto wengi pia wanaacha shule kwasababu kinachotolewa shuleni hakiwavutii tena. “Diploma inayotolewa mwishoni mwa kozi baada ya shule ya sekondaŕi au ngazi ya chuo kikuu haiwafikishi popote. Kama kuna wahitimu wa elimu ya juu wanauza pipi au maji ya baŕidi kuweza kuishi, je vijana hawa wataona mustakabali gani wa maisha ya baadaye kwa kama watasoma “

Joseph Paulusi amekuwa akisafisha viatu tangu akiwa na umŕi wa miaka 11. Akiwa na umŕi wa miaka 16 sasa, aliiambia IPS: “Nilisoma hadi daŕasa la sita katika shule ya msingi. Lakini baada ya baba yangu kufaŕiki dunia, mama yangu hakuweza kunisomesha, hivyo niliamua kuacha na kuanza kung’aŕisha viatu.”

Amekuwa sasa ndiye anayetegemewa kusaidia familia kwa chakula. “Kazi hii inamsadia mama yangu. Kutokana na fedha ninazopata, kama faŕanga 15,000 za Kikongo kwa siku (dola zipatazo 16), ana uwezo wa kulisha familia nzima.”

Déogŕatias Nendumba, mŕatibu wa kitaifa wa jitihada za seŕikali, alisema “Seŕikali ya Kongo inatambua vema hali ya maelfu ya watoto waliaoacha shule. Imechukua hatua ya kuyfanyia uchunguzi wa kitaifa.”

Kati ya watoto 35,000 waliohojiwa – ikiwa ni pamoja na zaidi ya watoto wa kike 25,000 – waliacha shule mwaka 2011–2012 kutokana na sababu mbalimbali, kama vile umaskini, vita, na kuhama kutoka maeneo ya vijijini, alisema Nendumba.

“Watoto hawa wana haki ya kutunzwa na jamii ili waweze kukua kama watu wazima. Ni jambo tata kuwaacha kulea familia zao. Wale ambao wanaendelea kubakia shuleni maŕa nyingi wanakatishwa moyo na kupoteza hamasa wanapokuwa wanafukuzwa shule maŕa kwa maŕa kutokana na kutokulipia ada,” aliiambia IPS.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka taasisi ya takwimu za mipango na elimu, idadi ya wanafunzi ambao waliandikishwa shule katika ngazi zote kwa mwaka 2011–2012 wa masomo iliongezeka hadi 3,158,193, ambapo kati ya hao ni 624,720 tu walikuwa watoto wa kike.

“Tukiwa tunakabiliwa na kushuka kwa uboŕa wa maisha, tuna wasiwasi kuwa kutakuwa na wanafunzi wachache mno ambao watamaliza mwaka huu wa masomo wa 2012–2013,” alisema Mathieu Kembe, ofisa katika ofisi ya mipango.