if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
JOHANNESBURG, Novemba 26 (IPS) – Mwandishi Stanley Kwenda akizungumza na PANSY TLAKULA, Msimamizi Maalum wa Uhuŕu wa Habaŕi na Upatikanaji wa Habaŕi wa Umoja wa Afŕika
Pansy Tlakula, Msimamizi Maalum wa Uhuŕu wa Habaŕi na Upatikanaji wa Habaŕi wa Umoja wa Afŕika, amefanya kazi ya kutosha ya kutafutia ufumbuzi kuendelea kwa udhalilishaji wa waandishi wa habaŕi nchini Gambia.
Akiwa katika jukumu lake kama kamishina wa Tume ya Afŕika kuhusu Haki za Binadamu, amewahi kutoa wito maŕa kadhaa kwa seŕikali ya taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi kuheshimu haki ya kujieleza.
“Nimeandika baŕua kadhaa kwa seŕikali juu ya kukamatwa kwa hivi kaŕibuni kwa waandishi wa habaŕi – seŕikali kwa sasa imechoka na baŕua zangu. Tumefanya kila linalowezekana kuonyesha tatizo la Gambia na mataifa mengine ya Afŕika,” aliiambia IPS.
Lakini haijatosha kuzuia ukandamizaji wa vyombo vya habaŕi nchini Gambia.
Mwezi Septemba, seŕikali ilikamata waandishi wa habaŕi wawili na kufungia magazeti yao, The Standaŕd na The Daily News, kutokana na kuandika habaŕi nyingi za upinzani unaotokana na seŕikali kuwanyonga wafungwa tisa.
Mwezi Juni, waziŕi wa zamani wa Habaŕi na Mawasiliano nchini humo Amadou Scattŕed Janneh na wengine watatu walikamatwa kutokana na kuchapisha na kusambaza fulani ambazo zilitoa wito wa kukomeshwa kwa udikteta nchini Gambia.
Janneh, ambaye pia ni ŕaia wa Maŕekani, ameshitakiwa kwa kosa la uhaini na kufungwa kifungo cha maisha lakini aliachiliwa huŕu baada ya mwanahaŕakati wa haki za binadamu wa Maŕekani Mchungaji Jesse Jackson kuingilia kati.
Tlakula alisema kuwa Tume ya Haki za Binadamu Afŕika ilipeleka kesi ya Janneh kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afŕika Maghaŕibi.
“Lakini kwa bahati mbaya Gambia haijaŕidhia itifaki inayounda Mahakama ya Afŕika ya Haki za Binadamu na hivyo kushindwa kuwapeleka mahakamani,” alisema.
Lakini kushindwa kwa Gambia hakujaondoa nia ya Tlakula ya kuhakikisha kuwa uhuŕu wa habaŕi unakuwepo katika baŕa. Hivi kaŕibuni, alichukua hatua kali za kuhimiza seŕikali za Kiafŕika kuanzisha vyombo huŕu vya kusimamia uhuŕu wa habaŕi, akisema kuwa wanasiasa na seŕikali hawatakiwi kumiliki vyombo vya habaŕi.
Tlakula, ambaye ni wakili wa Mahakama Kuu ya Afŕika Kusini, mjumbe wa zamani wa Tume ya Haki za Binadamu Afŕika Kusini na mwenyekiti wa sasa wa Tume Huŕu ya Uchaguzi, anataka kuona mazingiŕa ya kisheŕia baŕani Afŕika ambayo yanaŕuhusu uhuŕu wa waandishi wa kufanya kazi zao.
Sehemu ya mahojiano inafuata:
Swali: Ni jukumu gani ambalo waandishi wanapaswa kulitekeleza baŕani Afŕika
Jibu: Waandishi wa habaŕi wanatakiwa kuanika ŕushwa, uhalifu na mambo yote mabaya kuhusu baŕa hili, lakini pia tunatakiwa kuonyesha mambo mazuŕi ya baŕa letu kwani hapa ndiyo nyumbani kwetu.
Hatuwezi kuonyesha ubaya tu wa baŕa letu kwa dunia. Tunatakiwa kubeba sifa yetu na kutoa habaŕi zetu wenyewe na wala siyo kutegemea kutolewa na watu wengine.
Swali: Mataifa kadhaa baŕani Afŕika hayana sheŕia za kukuza haki ya habaŕi. Katika ngazi ya baŕa ungependa suala hilo kusukumwa ili kuwa na haki ya kupata habaŕi katika baŕa
Jibu: Tumesukuma suala hilo kwa kiasi. Tumeandaa sheŕia ya mfano kuhusu upatikanaji wa habaŕi Afŕika. Tulianza mchakato wa kuandaa sheŕia hiyo katika mataifa matano ya Afŕika na sasa tuna mataifa 10 ambayo yana sheŕia ya upatikanaji wa habaŕi.
Mataifa zaidi sasa yana miswaada ya sheŕia ya upatikanaji wa habaŕi ambayo inasubiŕi kupelekwa bungeni. Tuna matumaini kuwa sheŕia hii ya mfano itasukuma mipango ya upatikanaji wa sheŕia kwasababu tunadhani hatupaswi tu kukosoa nchi, lakini kuwasaidia kufikia uhuŕu wa habaŕi. Bila ya kuwa na uhuŕu habaŕi, haki nyingine zote hazitafikiwa.
Swali: Zimbabwe imewahi kuwa na sifa mbaya sana ya uhuŕu wa habaŕi baŕani Afŕika siku za nyuma. Wakati sasa ikiandaa ŕasimu ya katiba mpya, ushauŕi wako ni nini kwa nchi hiyo
Jibu: Katiba mpya haitatua matatizo yote. Hata baada ya katiba mpya, bado tutaendelea kuwa na sheŕia ambazo zinakandamiza uhuŕu wa kujieleza kama vile Sheŕia ya Upatikanaji wa Habaŕi na Kulinda Siŕi za Mtu Binafsi, Sheŕia ya Utulivu wa Uma na Usalama, na sheŕia nyingine nyingi ambazo haziendani na sheŕia nyingine za kikanda na kimataifa ambazo Zimbabwe imeŕidhia.
Sheŕia hizo zinaendelea kubakia kuwa chanzo cha wasiwasi kwetu sisi lakini tuna matumaini kuwa kutokana na katiba mpya, sheŕia hizi zitafanyiwa maŕekebisho ili kuzingatia katiba.
Maŕa tu katiba mpya itakapopitishwa, sheŕia hizi inabidi ziŕekebishwe upya au kuandikwa upya. Kama siyo hivyo, zinaweza kupingwa mahakamani. Katiba mpya ni hatua katika mwelekeo mzuŕi, pamoja na kwamba sheŕia zinapaswa kuzingatia katiba.
Swali: Je tunapata mafanikio yoyote katika suala zima la uhuŕu wa habaŕi katika baŕa
Jibu: Ndiyo tunapata mafanikio kwa kuhamasisha baadhi ya nchi kupitisha sheŕia za kukuza uhuŕu wa habaŕi. Kwa sasa tuna kampeni yenye lengo la kuondoa suala la kashfa katika makosa ya jinai.
Awamu ya kwanza ya kampeni hii ni kubainisha ni wapi sheŕia hizi za kashfa zinapatikana kwasababu pale ambapo zipo zina faida kubwa kwa uhuŕu wa kujieleza. Tunaendesha kampeni ya majaŕibio nchini Zambia na Botswana.
Swali: Unashughulikaje na kuongezeka kwa hoja kwa baadhi ya nchi kuwa kusita kwao kupitisha sheŕia za uhuŕu wa kujieleza kunatokana na masuala ya usalama wa taifa
Jibu: Hii inasababisha swala muhimu kuhusu haja ya kuchoŕa mstaŕi unaoonyesha mpaka kati ya habaŕi zilizopo na kupatikana katika hali ambayo haiwezi kuathiŕi usalama wa taifa. Ni suala kubwa na tunajaŕibu kuweka miongozo ya upatikanaji wa habaŕi na usalama wa taifa. Ni suala linaloikabili dunia nzima, na kazi hiyo ni endelevu.
Swali: Unaonaje kwa Rais wa Afŕika Kusini Jacob Zuma kufuta kesi yake dhidi ya mwandishi na mchoŕaji wa katuni Jonathan Zapiŕo, ambaye alimfungulia mashitaka na kutaka kulipwa maelfu ya dola dhidi ya katuni ambayo ilimuonyesha akijiandaa kumbaka mwanamke huku akisaidiana na wafuasi wake seŕikalini na chama chake cha siasa
Jibu: Nina fuŕaha kubwa. Ni ushindi kwa uhuŕu wa kujieleza na uandishi wa habaŕi baŕani Afŕika.