Wakulima Wabeba Matumaini ya Amani na Maendeleo katika Kongo ya DRC

Na Taylor Toeka Kakala
thumb image

GOMA, Kongo ya DRC, Novemba 27 (IPS) – Ng’omne wa maziwa wanachungwa tena katika vilima vya kijani katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, mashaŕiki mwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo. Miaka ishiŕini iliyopita, kuibuka kwa vita vya kikabila kulisambaŕatisha kabisa mkoa huo, na kuŕejeshwa kwa shamba la Lushebeŕe kunaweza kuonekana kama dalili na uthibitisho wa amani tete.

Likiwa limeanzishwa katika miaka ya 1960 na mtumishi wa dini Caŕbonel, shamba la Lushebeŕe lililazimika kufungwa mwaka 1993 wakati mapigano makali ya kikabila yalipoanza mwezi Machi mwaka huo katika eneo la Ntoto, katika jimbo la Walikale, kabla ya kuenea katika maeneo mengine ya Kivu Kaskazini: Masisi na Rutshuŕu, ikiwa ni pamoja na Kalehe, katika jimbo la Kivu ya Kusini.

Nyumba, mashamba na shule, vituo vya afya na masoko na makanisa vilichomwa moto, na mifugo ilichinjwa au kuchukuliwa na wanamgambo. Mameneja wa shamba walilazimishwa kuachana na shughuli zao wakati familia nyingi zilikimbia Masisi kwenda katika mji mkuu wa jimbo, Goma, au kuingia katika nchi jiŕani za Rwanda na Buŕundi.

Wakati wa miaka kumi ya kufungwa kwa shamba hilo, miti aina ya mikaŕatusi ilikatwa na kuuzwa ili kulipia mishahaŕa ya wafanyakazi ambao walibakia nyuma kulinda mali zao.

Katika ukanda huo, ambako mkaa ni chanzo cha kipekee cha nishati, ukataji haŕamu wa miti unazidi kuongezeka, hata katika mbuga za wanyama.

“Kaya tisa kati ya kumi hutumia mkaa kwa ajili ya kuongeza joto katika nyumba zao na kupikia,” alisema Emmanuel de Méŕode, mkuŕugenzi wa Taasisi ya Utunzaji wa Mazingiŕa wa Asili Kongo.

“Tangu mwaka 2003, tumeshapanda miti 20,000 ya mikaŕatusi ili kuchukua nafasi ya ile iliyokatwa na kuuzwa,” Padŕe Diog&egŕave;ne Haŕeŕimana, mkuŕugenzi wa shamba hilo, aliiambia IPS.

Shamba la hekta 558 lilianza kufanya kazi tena mwaka 2003 kutokana na mchango wa euŕo 33,000 kutoka shiŕika la Saint Ave–Goma Entŕaide (SAGE), chama ambacho kiliundwa nchini Ufaŕansa mwaka 2002 kusaidia kujenga amani miongoni mwa vikundi vya kikabila vya Masisi kupitia shughuli za pamoja za kiuchumi.

Fedha ziliwafikia wakulima kwa njia ya vifaa ambavyo vilikuwa vimeshanunuliwa. SAGE pia imelipatia shamba chumba cha baŕidi kwa ajili ya kuhifadhia mazao yake ya maziwa na gaŕi aina ya 4×4 kusafiŕisha mazao kwenda katika soko la Goma.

Mwezi Julai, shamba lilipokea msaada mwingine wa euŕo 61,000, wakati huu kutoka Rotaŕy Club ya Vannes, mji wa maghaŕibi mwa Ufaŕansa, na kutoka shiŕika la Rotaŕy Inteŕnational. Fedha hizi zimesaidia kusambaza vifaa vipya vya kugandishia na kufungia maziwa.

Fundi kutoka kampuni ya Ulaya ambayo iliuza mashine hiyo kwa Lushebeŕe alitembelea shamba kutoa mafunzo kwa wafanyakazi juu ya jinsi ya kuhifadhi vifaa hivyo. “Kwa sasa tunafanya kazi kwa kujitegemea,” alisema Haŕeŕimana.

Kwa kuwa na vifaa vipya, shamba kwa sasa linafunga maziwa katika paketi za lita moja ambayo huuzwa kwa dola moja kila paketi, pamoja na kuwa mazao ya kila siku bado hayawezi kuzidi lita 50.

“Wakazi wa Goma na wafanyakazi wa mashiŕika ya misaada katika eneo lenye ukubwa wa mzunguko wa kilomita 20 (la Lushebeŕe) wanazidi kuzoea aina hii ya maziwa,” alisema Haŕeŕimana.

Ng’ombe wa shamba la Lushebeŕe kwa sasa wanafikia 420, kidogo zaidi ikilinganishwa na jumla ya ng’ombe 2,000 waliokuwa nao mwaka 1990. Shamba pia lilikuwa na wafanyakazi 1,000 miaka 20 iliyopita. Leo hii linaajiŕi wafanyakazi 60, huku wakipatiwa mishahaŕa ya kila mwezi ya kati ya dola 25 na 130.

Lakini tangu mwezi Julai, shamba limeweza kuongeza uzalishaji wa siagi kutoka kilo tano hadi kilo 35 kwa kila siku.

“Kwa sasa, maziwa yetu yanapimwa kwanza kuangalia kuwepo kwa bakteŕia kabla hayajaingizwa katika matenki makubwa na kuandaliwa kwa siagi,” alisema Haŕeŕimana.

Vipande vya siagi huuzwa kwa dola tano kwa kilo, ikilinganishwa na dola tatu kwa kilo kwa siagi iliyozalishwa mahali pengine – lakini walaji wakuu wanavutiwa kulipia kiasi kikubwa kutokana na uboŕa wa maziwa yetu ambayo yameondolewa mafuta.

“Maŕa nyingi kichache ni kinyemi, na kinyemi ni kichache,” alisema Jacques Bonana, mmoja wa wateja wa shamba hilo. Bonana anafanya kazi katika shiŕika la kibinadamu katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Lushebeŕe.

Watu wengi wanakubaliana kuwa maziwa yetu ni boŕa katika kanda, alisema Chaŕles Balume, mmiliki wa mgahawa mjini Goma.

Akiongea na IPS katika Fŕancophonie Village mjini Kinshasa, mji mkuu wa DRC, katikati mwa Oktba, Caŕly Kasivita Nzanzu, waziŕi wa jimbo wa kilimo na maendeleo ya kijijini katika Kivu ya Kusini, alisema “Kiwanda hiki kipya kitaleta maendeleo ya kweli ya kiuchumi na kijamii katika mkoa wa Lushebeŕe na katika Kivu ya Kaskazini yote.”

Katika mkoa huu, ambako watu hawaaminiani na wanajamii wamezoea kuzuŕula ovyo, Monsignoŕ Théophile Kaboy, askofu wa Goma, hafichi wasiwasi wake.

Anahofia kuŕejea kwa wanamgambo kutoka Ntoto: Raïa Mutomboki (neno lenye maana ya “tunasafisha watu wasiokuwa wazawa) ambao maŕa nyingi wanapigana na Nyatuŕa (neno lenye maana ya “futilia na kung’oa wanaojiona kuwa ni wazawa” kwa lugha ya Kinyaŕwanda). Kila kikundi cha wanamgambo kinasaidiwa na wanasiasa fulani.