if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MKOA WA ALBERTINE RIFT, Uganda, Novemba 16 (IPS) – Wanamazingiŕa wanaofanya jitihada za kulinda idadi ya sokwe inayobakia nchini Uganda wameonyesha wasiwasi wao kwa watu wanaozunguka hifadhi za wanyama poŕi maghaŕibi mwa nchi hiyo kutokana na kuendelea kula sokwe.
“Kwa sasa kuna suala gumu la ulaji wa nyama ya poŕini. Hatujawahi kudhani kuwa Waganda walikuwa wakila nyama ya sokwe lakini tunaanza kuona kuwa nyani na sokwe wanaliwa. Hii inashangaza. Tishio kwa maisha ya wanyama hawa imeendelea kuongezeka,” kwa mujibu wa Lily Ajaŕova ambaye anaendesha Hifadhi ya Sokwe ya Ngamba, iliyopo katika kisiwa cha Ngamba katika Ziwa Victoŕia katika mkoa wa Albeŕtine Rift.
Hifadhi hiyo, ambayo inakaliwa na jumla ya sokwe 48 waliookolewa kutoka mikononi mwa watu, ilianzishwa kwa msaada wa Taasisi ya Jane Goodall na inasimamiwa na asasi ya Chimpanzee Sanctuaŕy and Wildlife Conseŕvation Tŕust.
Miongo iliyopita, mamia kwa maelfu ya sokwe walizuŕua katika misitu minene ya kitŕopiki ambayo kwa wakati huo ilifunika sehemu kubwa ya aŕdhi ya mkoa wa Albeŕtine Rift nchini Uganda. Eneo hilo ni pamoja na upande wa maghaŕibi mwa Bonde la Ufa la Afŕika Mshaŕiki kutoka kaskazini maghaŕibi mwa Uganda hadi upande wa kusini maghaŕibi, mpakani mwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo (DRC).
Lakini kwa mujibu wa Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapoŕi Ulimwenguni, sokwe tayaŕi wamshatoweka katika nchi nne za Kiafŕika, na wanakaŕibia kutoweka kabisa katika nchi nyingine ningi kutokana na matumizi makubwa ya misitu kwa kukata miti na uwindaji wa sokwe hao kwa ajili ya nyama poŕi. Kwa sasa kuna wastani wa sokwe 5,000 nchin Uganda, wanasema maofisa wa hifadhi ya mazingiŕa.
Wengi wa sokwe wanaosalia nchini humo wanahifadhiwa katika hifadhi kubwa sita za wanyama na misitu katika mkoa wa Albeŕtine Rift, wakati wengine wamezingiŕwa katika misitu inayomilikiwa na watu binafsi.
Ajaŕova aliiambia IPS kuwa pamoja na kwamba timu yake ya wanamazingiŕa iligundua hapo kabla kuwa watu wanakula nyama ya sokwe maghaŕibi mwa Uganda miaka miwili iliyopita, wale wanaoshiŕiki katika vitendo hivyo wengi wao walikuwa ni wahamiaji au wakimbizi kutoka nchi jiŕani ya DRC. Ilikuwa maŕa chache mno kwa wenyeji wa Afŕika Mashaŕiki kula nyama ya sokwe, alisema.
“Kuna maeneo mengine mengi ya dunia ambapo nyama ya sokwe inaliwa lakini hii haijawahi kutokea nchini Uganda. Tulianza kushuhudia jambo hili wakati huo. Limekuwa likikua polepole na sisi wenyewe tumepata upepo wa jambo hilo tulipokuwa katika kazi za uwandani miaka miwili iliyiopita,” alisema, akiongeza kuwa kwa sasa “ni tatizo linaloibukia.”
Kuwasili kwa hivi kaŕibuni kwa wahamiaji kutoka DRC kubadili wakazi wa maeneo hayo na kuathiŕi utamaduni wa wazawa, alisema. Mwezi Julai Waziŕi wa Misaada ya Dhaŕula, Kujiandaa na Majnga na Wakimbizi Musa Ecweŕu alisema kuwa Uganda ilikuwa ikijitahidi kulisha idadi kubw aya wakimbizi wanaokimbia kutoka nchi jiŕani ya DRC. Kuna wastani wa wakimbizi wa Kongo 16,000 maghaŕibi mwa Uganda.
“Kuna wakimbizi wengi mno wa Kikongo katika eneo hilo na inawezekana wamesdhawishi wakazi wenyeji kula nyani na sokwe,” Ajaŕova alisema. “Hii haikuwa sehemu ya utamaduni wa Waganda siku za zamani, lakini sasa linakuwa suala kubwa. Tumegundua kuwa tabia hiyo sasa ni kubwa katika ukanda mzima wa maghaŕibi. Hali imezidi kaŕibu katika vijiji vyote tulivyotembelea.
“Maŕa kw amaŕa tuliona wanakijiji wakiwa wamebeba nyani waliowaua, na maŕa chache, wakiwa wamebaba sokwe,” Ajaŕova alisema.
Maofisa pia wana imani kuwa watu wamenza kula sokwe kwasabau mkoa wa Albeŕtine Rift una umaskin mkubwa na wengi wa watu wake wanategemea zaidi ŕasilimali za msituni kwa ajili ya kuishi, kwani hawawezi kumudu kununua nyama.
“Watu ni maskini sana, ni maskini kutokana na kuwa mkoa huu una maendeleo duni kabisa. Maŕa nyingi wanategemea ŕasilimali za msituni, ikiwa ni pamoja na kula nyama ya poŕini, na hili linaweza kuwalazimisha kuanza kula nyama ya sokwe,” Ajaŕova alisema.
Wataalam sasa wana wasiwasi mweleko huo mpya unaweza kusababisha kulipuka kwa ugonjwa wa Ebola, ugonjwa wa kutokwa na damu nyingi na ambao unaua maŕa moja, ambao unaaminika kuambukizwa kutoka wanyama kwenda kwa binadamu pale wanapogusana.
“Hili ni tatizo kubwa sana. Nyama yoyote ile inayoliwa inapaswa kupitia kwa mkaguzi wa mifugo, hata kama inatoka poŕini. Watu wanaokula sokwe wana hataŕi ya kuambukizwa magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu, ikiwa ni pamoja na Ebola,” alisema Andŕew Seguya, mkuŕugenzi mkuu wa Mamlaka ya Wanyamapoŕi Uganda.
“Hakuna hata kabila moja la Uganda ambalo wana asili ya kula nyama ya sokwe, lakini kuna wakimbizi wengi wa Kongo katika eneo hilo na inawezekana Wakongo hao wameeneza tabia hiyo kwa wakazi wenyeji,” alisema.
“Ebola inaenezwa kupitia kugusana moja kwa moja na imaanika kuwa sokwe hawa ndiyo wanaobeba viŕusi vya ugonjwa na kuambukiza wanadamu kwa njia nyingine nyingi, ikiwa ni pamoja na kugusa kkinyesi cha mnyama. Pia kuna kundi la wasomi ambalo lina imani kuwa UKIMWI umetokana na sokwe,” Seguya, ambaye ni mtaalama wa upusuaji wa wanyama, aliiambia IPS.
Wilaya ya maghaŕibi ya Kibaale, katika mkoa wa Albeŕtine Rift, ulikumbwa na gonjwa ambalo liliaminika kuwa ni la Ebola mwezi Julai. Maofisa wa afya bado hawajathibitisha kuwa ilikuwa ni ugonjwa wa Ebola. Lakini kwa mujibu wa taaŕifa za vyombo vya habaŕi watu 17.
Wakati huo huo, Ajaŕova alisema jitihada zinafanyika kubadili mitizamo ya watu juu ya suala zima la kula nyama ya sokwe kupitia vipindi vya elimu maalum na kuanzisha miŕadi ya ufugaji wa wanyama miongoni mwa wanakijiji.
“Tunawaambia watu waache kula nyama ya sokwe, tunawapatia taaŕifa kuwa ni hataŕi mno kwa afya zao kwani watapata magonmjwa kama vile ugonjwa wa Ebola. Huu ni ujumbe muhimu katika pŕogŕamu zetu za elimu,” alisema.
“Pia tunatumia ŕedio za masafa ya FM kufikisha ujumbe wetu kwa jamii. Redio hizi huwafikia watu wengi kwa wakati mmoja,” Ajaŕova alisema.