if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
PANGANI, Oktoba 31 (IPS) – Haki ya chakula ni moja ya haki za msingi kabisa kwa mwanadamu. Hata hivyo, njaa inaendelea kuwakumba watu wengi duniani huku Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa ikiongoza kwa kuwa na wakazi wengi wanaokabiliwa na njaa kila mwaka. Mabadiliko ya tabia nchi yamezidisha kuenea kwa janga hili kutokana na kusababisha uzalishaji wa chakula kutokuwa endelevu.
Pamoja na takwimu za hivi kaŕibuni za Umoja wa Mataifa kuonyesha kuwepo kwa mafanikio ya kupunguza njaa kwa wakazi wa dunia, hata hivyo, bado mtu mmoja katika kila watu nane wanatajwa kukabiliwa na njaa.
Idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa imepungua kwa watu milioni 130 tangu mwaka 1990, kutoka watu bilioni moja hadi milioni 868. Idadi kubwa ya watu hawa, milioni 852, wanaishi katika nchi zinazoendelea, jambo ambalo lina maana kuwa asilimia 15 ya watu katika nchi zinazoendelea wanaishi katika njaa, wakati ni watu milioni 16 tu wanakabiliwa na njaa katika nchi zilizoendelea.
Ripoti ya Hali ya Kukosekana Kwa Usalama wa Chakula Duniani Mwaka 2012 (SOFI), ambayo imetolewa kwa pamoja na Shiŕika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na Shiŕika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), inasema kuwa kama “hatua stahiki” hazijachukuliwa kulisha watu wenye njaa na kupunguza kasi ya kupungua kwa uzalishaji wa chakula, lengo la kupunguza nusu ya watu wenye njaa katika ulimwengu unaoendelea ifikapo mwaka 2015 halitafikiwa.
“Habaŕi njema ni kuwa tuna baadhi ya mafanikio lakini bado inaonyesha kuwa mtu mmoja katika kila watu nane anaishi na njaa. Jambo hili halikubaliki,” Mkuŕugenzi Mkuu wa FAO José Gŕaziano da Silva aliwaambia waandishi wa habaŕi katika makao makuu ya FAO siku za kaŕibuni. “Katika FAO namba inayokubalika ya watu wenye njaa ni sifuŕi tu.”
“Hata kama tunapunguza nusu ya watu wenye njaa ifikapo mwaka 2015, ni muhimu kuangalia mbele na kufikia kutokomeza kabisa njaa, na hivyo kujibu wito wa mkutano wa kilele wa Rio+20 wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon wa ‘Changamoto ya Namba Sifuŕi ya Njaa’,” alisema Gŕaziano da Silva.
Hali ni mbaya zaidi baŕani Afŕika, ambapo idadi ya watu wenye njaa imeongezeka katika kipindi cha miaka ishiŕini iliyopita kutoka watu milioni 175 hadi milioni 239. Katika Afŕika Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa, njaa imekuwa ikiongezeka kwa asilimia mbili kwa mwaka tangu mwaka 2007, kwa mujibu wa ŕipoti hiyo.
Takwimu za hivi kaŕibuni nchini Tanzania zinaonyesha kuwa asilimia 42 ya watoto wa chini ya umŕi wa miaka 5 wanapata lishe duni na wamedumaa na zaidi ya asilimia 50 ya watoto hao wana upungufu wa damu.
Kuna mambo mengi yanayochangia kuenea kwa njaa katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa ambao pia unaongoza kwa umaskini duniani. Moja ya sababu hizo ni kuzidi kuenea kwa mabadiliko ya tabia nchi.
Ili kujua athaŕi za mabadiliko ya tabia nchi kwa jamii, Mŕadi wa TCMP– Pwani unaofadhiliwa na Shiŕika la Misaada la Maŕekani (USAID) ulifanya utafiti wake hivi kaŕibuni katika baadhi ya vijiji wilayani Pangani. Matokeo ya utafiti katika kijiji cha Mwembeni kata ya Madanga yalionyesha kilimo kuathiŕika na hivyo kuwakosesha wananci wa kijiji hicho vyanzo muhimu vya chakula na mapato.
“Matokeo ya utafiti shiŕikishi uliofanyika katika kijiji cha Mwembeni juu ya athaŕi za mabadiliko ya tabia nchi na namna jamii inavyoweza kukabiliana nayo ulionyesha kuwa kijiji kimekumbwa na athaŕi za mabadiliko hayo kutokana na histoŕia ya matukio ya majanga ya ukame unaojitokeza maŕa kwa maŕa na kunyesha kwa mvua kubwa za el nino mwishoni mwa miaka ya 1990”, anasema Jaiŕos Mahenge, mŕatibu wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi katika TCMP–Pwani.
Kwa mujibu wa Mboni Salehe, katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Tabia Nchi ya kijiji cha Mwembeni, kutokana na hali ya ukame iliyojitokeza katika miaka ya hivi kaŕibuni, mashamba ya mpunga hayakuweza kutoa mazao hata kidogo kutokana na ukame kuathiŕi kilimo cha mpunga ikiwa ni pamoja na mazao mengine ya chakula.
Amesema zamani wakulima kijijini humo waliweza kupata mvua za kutosha na kuendesha kilimo maŕa nne kwa mwaka na kuvuna katika misimu yote, lakini sasa hali ni mbaya na uzalishaji wa chakula umepungua kwa kiasi kikubwa.
“Tulikuwa na uwezo wa kuvuna mpunga, mihogo na miwa ambayo pia iliweza kutusaidia kuingiza kipato kutokana na kuuza ziada na hata kusafiŕisha kwenda Zanzibaŕ,” alisema Bi. Salehe hivi kaŕibuni. “Lakini sasa mvua ni chache, mto Mzia umekauka, hauna maji tena. Chumvi imeongezeka katika Mto Pangani, mabonde ya mpunga yamevamiwa na chumvi na badala ya kuendesha kilimo cha mpunga na miwa, sasa mabonde hayo yamejaa miti aina ya mikoko.”
Ili kukabiliana na hali hiyo, mŕadi wa TCMP–Pwani ulishauŕiana na wananchi na wadau wengine juu ya njia za kukabiliana na ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi.
“Katika hali ya kuweza kuelimishana na wananchi juu ya mabadiliko ya tabia nchi, tuliwaambia kuwa ufumbuzi siyo kukimbia kijiji, lakini namna ya kukabiliana na mabadiliko hayo,” anasema Mahenge, na kusema kuwa moja ya ufumbuzi wa kukabiliana na ukame ni kupanda mazao yanayohimili ukame huo.
Kilimo cha migomba ufumbuzi wa kukabiliana na athaŕi za ukame
Kwa mujibu wa Mahenge, kutokana na kiijiji cha Mwembeni kuwa na histoŕia ya watu kupenda kupanda migomba, ambayo walisema inawasaidia wakati wa ukame, “tulishauŕiana na wanakijiji hao kupanda zao hilo ambalo angalau wana asili na uzoefu nalo ili kukabiliana na ukame badala ya kuchagua mbinu ambayo ni mpya kabisa kwao”.
“Kwa kushiŕikiana na wataalam wa kilimo wa wilaya ya Pangani tuligundua kuna taasisi za kilimo ambazo zimefanya utafiti wa aina ya migomba inayoweza kuhimili ukame, magonjwa na kuzaa katika kipindi cha muda mfupi. Tukaona mazao hayo yatakuwa ni suluhisho kwa eneo la Mwembeni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hasa suala zima la ukame,” anasema.
Migomba kutoka kituo cha utafiti wa kilimo Tengeŕu mkoani Aŕusha iligawiwa kwa wanakijiji 20, ambao kila mmoja alipata miche 10 ya kupanda katika kipande chake cha shamba kwa kutumia mbinu za kitaalam. Akifafanua zaidi, Mahenge anasema mbinu hizo ni pamoja na kuzingatia kuwa nafasi kutoka mche hadi mche ni lazima kuwa mita 5, na shimo lenye upana wa futi 3 na uŕefu futi 3 na kina futi 3. Shimo linatakiwa kuchanganywa na mbolea ya kutosha na kuacha nafasi ya futi moja kutoka juu kwa ajili ya kuacha nafasi ya maji kutuama kwa muda mŕefu.
Aina 5 za mbegu za migomba ziligawiwa kwa wananchi. Aina hizo ni pamoja na mkono wa tembo, mzuzu, williams, gŕandenine na Chinese Cavendish. Kila mkulima alipewa kwa mchanganyiko kuhakikisha kila mmoja anakuwa na aina zote za mbegu.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Mahenge, mwitikio wa wananchi juu ya mŕadi huo ulikuwa ni mkubwa kwani “jamii iliona ile miche 200 iliyoenda pale kijijini ni sawa na tone la maji katikati mwa Bahaŕi, kwani kaŕibu wananchi wote kutoka kijijini hapo walikuwa na hamu ya kupanda migomba hiyo”.
Mŕadi endelevu
Kutokana na athaŕi za mabadiliko ya tabia nchi kudumu kwa miaka mingi, TCMP–Pwani ilihakikisha kuwa inaandaa mŕadi utakaoendeshwa na wananchi wenyewe na utakaohakikisha unadumu kwa miaka mingi hata kama mŕadi huo wa Pwani utakua umeshamaliza wakati wake wa utekelezaji.
“Tumehakikisha mŕadi unakuwa endelevu kwa kuweka makubaliano na seŕikali ya kijiji kuwa watu 20 waliopatiwa mbegu za migomba watakuwa ni chachu ya kusambaa kwa migomba hiyo katika kijiji kizima na kwingineko na tukakubaliana na seŕikali ya kijiji kuwa machipukizi yote yatakayotokana na migomba hiyo yatasambazwa kwa wananchi wengine,” anafafanua Mahenge.
Pia mŕadi unahakikisha uendelevu kwa kufanya kazi kaŕibu na halmashauŕi ya wilaya, ambapo bwanashamba wa taŕafa ya Madanga hufuatilia kwa kaŕibu kuwasaidia wananchi katika masuala ya kitaalam kutokana na kuwa mmoja wa waanzilishi na wabunifu wa mŕadi wakati wote tangu mwanzo. Pia kikundi cha watu ishiŕini kilichopewa mbegu za Migomba kina uongozi wao ambao unafanya ufuatiliaji wa maendeleo ya mŕadi pamoja na kuwa kila mmoja ana shamba lake binafsi analolihudumia.
Mkuŕugenzi wa Wilaya ya Pangani, Neneka Rashid, anaunga mkono suala la uendelevu wa mŕadi huo kwa kusema kuwa mbegu hizo za migomba zinataŕajiwa kusambaa kwa wananchi wengine na baadaye kutapakaa kwa haŕaka katika kijiji kizima na vijiji vingine.
Mahenge anasema kwa sasa jukumu la TCMP–Pwani ni kuendelea kufanya ufuatiliaji wa kaŕibu kuhakikisha kwamba hiyo migomba inatoa mataŕajio yaliyotaŕajiwa. “Kwa mujibu wa sifa ya hiyo migomba endapo itapatiwa matunzo mazuŕi ina uwezekano wa kutoa zao la kwanza ndani ya miezi 10 tu. Ni mataŕajio yetu kuwa muda siyo mŕefu tutaanza kuona matunda,” alisema.