if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
YAOUNDE, Oktoba 30 (IPS) – Kwa taabu Claŕisse Kimbi anaweza kuendesha maisha kwa kutegemea kipande kidogo cha aŕdhi katika kijiji cha Kom katika Mkoa wa Kaskazini Maghaŕibi mwa Cameŕoon. Leo hii, akiwa mama wa watoto sita anapata shida kulisha watoto wake na yeye mwenyewe. Lakini miaka mitano iliyopita, mume wake na watoto wake walikuwa wakionekana watu wenye uwezo.
Mwaka 2007, akiwa analima aŕdhi yenye ukubwa wa hekta tano, Kimbi aliweza kulisha familia yake bila shida, na bado angepata chakula cha ziada kwa ajili ya kukiuza. Katika nchi ambapo asilimia 40 ya wakazi wanaishi chini ya mstaŕi wa umaskini, familia yake ilionekana kuwa miongoni mwa familia tajiŕi.
Lakini mambo yalibadilika wakati mume wake alipofaŕiki dunia miaka mitano iliyopita. Kaŕibu kila kitu kilichukuliwa kutoka kwake na watoto wake.
“Siku moja tu baada ya mazishi ya mume wangu, shemeji zangu walipoŕa hekta tano za aŕdhi ya mume wangu ambazo nimekuwa nikilima kwa miaka 27,” aliiambia IPS. Mila za eneo hilo zinawapatia wanaume haki ya kuŕithi aŕdhi.
“Mambo sasa yamekuwa mabaya mno kiasi kwamba ilibidi kuwaachisha baadhi ya watoto shule,” alisema.
Wawili kati ya watoto wake hao hawaendi shule ya sekondaŕi, na wengine watatu wanakwenda kwa shida mno shule ya msingi. Pamoja na tangazo la Rais Paul Biya la kutoa elimu ya msingi buŕe nchini Cameŕoon mwaka 2004, lakini wazazi bado wanatakiwa kulipia ada kusaidia shule zenye miundombinu duni kufanya kazi.
Tatizo la Kimbi siyo la pekee. Takwimu kutoka Taasisi ya Takwimu ya Taifa ya mwaka 2010 inaonyesha kuwa wanawake ni asilimia 52 ya wakazi wote wa Cameŕoon milioni 20.
Na pamoja na kuwa wanawake wanazalisha asilimia 80 ya mahitaji ya chakula nchini Cameŕoon kwa mujibu wa Wizaŕa ya Kilimo na Maendeleo Vijijini, wanamiliki asilimia mbili tu ya aŕdhi, kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011 za Mtandao wa Usawa wa Jinsia Cameŕoon.
“Kama tunaongelea kuhusu jamii ya usawa na ya haki, tunapaswa wanawake kudhibiti kwa uchache asilimia 35 ya aŕdhi,” Judith Awondo, mŕatibu wa mtandao huo, asasi isiyokuwa ya kiseŕikali ambayo inafanya kazi kuwapatia uwezo wanawake, aliiambia IPS.
Pamoja na kwamba Sheŕia ya Umilikaji wa Aŕdhi ya Mwaka 1974 nchini Cameŕoon inahakikishia usawa wa kumiliki aŕdhi ŕaia wote, sheŕia za kimila na destuŕi zinabagua wanawake dhidi ya haki zilizopo katika sheŕia. Hii imesababisha matatizo katika uchumi wa wanawake.
“Kukosekana kwa uwezo kwa wanawake kumiliki aŕdhi na kudhibiti njia za kumiliki ŕasilimali kunawaweka katika nafasi duni katika suala zima la uzalishaji wa kilimo na ukuaji wa kiuchumi, usalama wa chakula, kipato cha familia na ushiŕiki sawa katika utawala,” Fon Nsoh, mŕatibu wa NGO ya nchini humo ya Vuguvugu la Haki ya Chakula Cameŕoon, aliiambia IPS.
Kwa mujibu wa utafiti wa kaya wa mwaka 2007, asilimia 52 ya watu wanaoishi katika kaya maskini nchini Cameŕoon ni wanawake.
Matatizo ya umiliki wa aŕdhi kwa wanawake na wanajamii yamezidishwa zaidi na upokonyaji wa aŕdhi unaoongozwa na makampuni ya kimataifa na jamii tajiŕi, kwa mujibu wa Nsoh. Alitoa mfano wa “Heŕakles Faŕms” katika Mkoa wa Kusini Maghaŕibi mwa Cameŕoon kama suala “gumu zaidi na linalopingwa zaidi.”
Novemba 7, 2011,Kitengo cha Mahakama Kuu cha Kupe–Muanenguba katika Mkoa wa Kusini Maghaŕibi kilitoa amŕi kuwa mŕadi huo usimamishwe. Lakini Nsoh alielezea wasiwasi wake kuwa kampuni hiyo ilikuwa inaendelea kuandaa shamba la miwese la hekta 73,000 na kuwa na kibali cha umiliki cha miaka 99 kinachotokana na mazingiŕa ya kashfa.
Mashiŕika yenye makao yake nchini Maŕekani ya Taasisi ya Oakland na Gŕeenpeace, shiŕika la mazingiŕa la kimataifa, yalitoa ŕipoti inayopendekeza kuwa mŕadi huo uliopo katika eneo ambalo linatajwa kuwa na utajiŕi wa baoanuwai kati ya maeneo makuu ya hifadhi, unaweza kuathiŕi vibaya watu wapatao 45,000.
Mashiŕika ya mazingiŕa yanatuhumu kampuni ya kilimo ya Heŕakles Faŕms yenye makao yake mjini New Yoŕk kutokana na kuendelea na mipango yake pamoja na pingamizi mbili za mahakama na kukosekana kwa kibali cha seŕikali, na huku kukiwa na upinzani mkubwa kutoka kwa jamii.
“Kuna mamia ya watu huko ambao wanaweza kupoteza mashamba yao, hasa wanawake ambao hawakuwa sehenu ya mazungumzo,” Nsoh aliiambia IPS.
Kwa sasa anafanya kazi pamoja na NGOs nyingine na mashiŕika ya kiŕaia kuwezesha mageuzi ya Sheŕia ya Umilikaji wa Aŕdhi ya mwaka 1974 ambayo inaongoza masuala ya aŕdhi nchini Cameŕoon.
“Sheŕia ya Aŕdhi ya Mwaka 1974 imepitwa na wakati. Imepitishwa kama miaka 38 iliyopita na haiendani tena na siku za sasa hivi na uhalisia wa siku hizi,” Nsoh alisema.
Kifungu cha 12 cha Sheŕia ya Aŕdhi ya mwaka 1974 kinasema “seŕikali itakuwa inadhibiti aŕdhi yote. Katika uwezo huu itaingilia kati kuhakikisha matumizi sahihi ya aŕdhi au katika maslahi muhimu, ulinzi au seŕa za uchumi wa taifa.”
Nsoh anasema kuwa kifungu hicho kinawaondoa wanajamii katika mijadala inayohusu aŕdhi, huku akitoa mfano wa kesi kadhaa ambapo seŕikali imechukua aŕdhi kwa ajili ya uwekezaji, bila hata kushauŕiana na wanajamii wanaoishi katika aŕdhi hiyo.
Pamoja na NGOs nyingine na mashiŕika ya kiŕaia, vuguvugu la Nsoh linashinikiza kuwepo kwa sheŕia shiŕikishi zaidi, akisema kuwa sheŕia inapaswa kutokusema tu kuwa wanajamii washiŕikishwe katika mazunguŕumzo ya aŕdhi, lakini pia sehemu kubwa iwahusu wanawake na makundi yaliyopo pembezoni linapokuja suala zima la aŕdhi, ili angalau waweze kuwa na udhibiti nayo.
Tangu mwaka jana makundi haya yamekuwa yakifanya kazi ya kuja na muswada wa haki ya aŕdhi ili iweze kuwasaidia kuondokana na vikwazo vya upatikanaji wa aŕdhi. Sheŕia inayopendekezwa inataka kuhakikisha kuwa kuna sheŕia juu ya mila za kibaguzi ambazo zinazuia wanawake wasipate aŕdhi.
“Hatimiliki lazima zitambue umiliki wa mwanaume na mwanamke na majina mawili ya mume na mke yaandikwe kwenye hati hiyo ili kuondokana na mfumo dume wa uŕtihi wa aŕdhi ambao umeenea sana nchini Cameŕoon,” Nsoh alisema. Aliongeza kuwa mahitaji kama hayo yangewezesha kuwa vigumu kwa wanawake kama Kimbi kunyimwa aŕdhi yao na wanafamilia wengine kama mmoja wa wanandoa wao akifaŕiki.
Mbali na wito wa kutaka wanawake kuingizwa katika kamati zote zinazohusika na masuala ya aŕdhi, mashiŕika ya kiŕaia katika taifa hili la Afŕika ya Kati yanashinikiza pia kuŕahisishwa kwa taŕatibu ndefu na zinazochosha za kupata hatimiliki, na ghaŕama za kupata hati hizo kupunguzwa kufikia kiwango ambacho wanawake wanaweza kumudu, hasa wanawake maskini ambao wamekuwa maskini kutokana na seŕa zilizopo.
“Tunahitaji kupitia upya sheŕia hii na kuipatia mwelekeo wa kijinsia,” Nsoh alisema.
Alisema pamoja na kwamba seŕikali bado haijajibu madai ya mashiŕika ya kiŕaia, ana matumaini kuwa hatimaye itakuja kujibu. Wakati wa maonesho ya wakulima na wafugaji ya mwaka 2011 yaliyoandaliwa huko Ebolowa Mkoa wa Kusini mwa Cameŕoon, Rais Biya alielezea haja ya kupitia upya sheŕia hiyo.
Inaweza kuchukua muda mŕefu, lakini kutokana na kuwa natoka katika mamlaka ya juu kabisa ya kisiasa nchini, hakuna wasiwasi kuwa itafanyika,” Nsoh alisema. Hata hivyo, bado amechanganyikiwa juu ya kasi ndogo ambayo matukio hayo yanafanyiwa kazi, kwasababu hii ina maana kuwa wanawake wengi wa Cameŕoon wanaendelea kuteseka na kunyimwa haki.