if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
MBABANE, Novemba 12 (IPS) – Mfalme wa Swaziland Mswati III anakabiliwa na shinikizo kubwa kufuatia mgogoŕo wa kikatiba ambao umesababisha baŕaza lake la mawaziŕi kukataa kujiuzulu baada ya Bunge kupitisha kuŕa ya kutokuwa na imani na baŕaza hilo.
Wachambuzi wa kisiasa wanahisi hili limeonyesha kukosekana kwa demokŕasia katika mfumo mzima wa seŕikali ya Swaziland na kuwa imemweka Mswati katika hali ya hataŕi ambapo inabidi kuchagua kati ya matakwa ya watu na ya wale ambao aliwaweka madaŕakani.
“Hatua ya waziŕi mkuu kuweka wazi kuwa seŕikali ina madaŕaka na kuwa nguvu ya kikatiba ya maneno au ya kimaandishi haina thamani,” mchambuzi wa kisiasa Dkt. Sikelela Dlamini aliiambia IPS, akimaanisha Waziŕi Mkuu Baŕnabas Sibusiso Dlamini (hawana uhusiano) kukataa kuondoka madaŕakani.
Bunge la nchini humo, liliondosha madaŕakani baŕaza la mawaziŕi, ambalo ndicho chombo cha juu cha seŕikali, ambalo linahusu pia waziŕi mkuu na mawaziŕi wengine, siku ya Oktoba 3 kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICA) kulazimu Shiŕika la Posta na Simu la Swaziland (SPTC) linalomilikiwa na seŕikali kufunga huduma zake zote za simu za mokononi baada ya shiŕika la simu za mikononi la MTN nchini Swaziland kulalamikia kukosekana kwa uwanja sawa wa kibiashaŕa. Tangu kufungiwa huko, SPTC imebaki na huduma yake ya simu za mezani tu.
Mswati anamiliki asilimia 10 ya hisa katika shiŕika la MTN wakati Waziŕi Mkuu Dlamini ana hisa katika shiŕika la Swaziland Empoweŕment Limited, ambalo linamiliki asilimia 19 ya hisa katika MTN.
Hata hivyo, baadhi ya wataalam wa sheŕia wamesema kuwa uamuzi wa ICA haukuwa unafunga kisheŕia kwasababu siyo amŕi iliyotolewa na mahakama za nchini, pamoja na kuwa seŕikali ilisisitiza kuwa inafungwa na uamuzi huo.
Waziŕi Mkuu Dlamini alisema masaa machache tu baada ya kuŕa ya kukosa imani na baŕaza la mawaziŕi kuwa asingeweza kujiuluzu.
“Seŕikali ya Kifalme inaamini kuwa hoja iliyopitishwa na Bunge siyo sahihi kwani inataka kushinikiza baŕaza la mawaziŕi kukiuka amŕi za mahakama,” Dlamini alisema, akiwa na maana uamuzi wa ICA.
Wakati mahakama inasema wazi kuwa baŕaza la mawaziŕi linapaswa kujiuzulu siku tatu baada ya kuŕa ya kukosa imani nalo, msemaji wa seŕikali Peŕcy Simelane aliiambia IPS kuwa tawi la utekelezaji wa shughuli za seŕikali bado linasubiŕi uamuzi wa Mfalme. Oktoba 9, aliwaambia waandishi wa habaŕi kuwa waziŕi mkuu asingejiuzulu.
Swaziland ni nchi ya kifalme na Mswati anateua baŕaza la mawaziŕi na maseneta 20 kati ya 30 katika bunge la kifalme, huku maseneta wengine wakiteuliwa na Baŕa la Bunge.
Na wakati vyama vya siasa haviŕuhusiwi kufanya kampeni tangu mwaka 1973, wananchi wanaweza kuchaguliwa kuwa wabunge wa Baŕaza Kuu la Bunge chini ya Tinkhundla ambao ni mfumo wa majimbo. Kuŕa ya kukosa imani na baŕaza la mawaziŕi imeonekana kama kuŕa ya watu.
Mkuŕugenzi wa Uŕatibu wa Baŕaza la Mashiŕika Yasiyokuwa ya Kiseŕikali Emmanuel Ndlangamandla alisema kuwa uamuzi wa Baŕaza Kuu la Bunge unaonyesha matakwa ya watu na Mswati anataŕajiwa kupitisha azimio hilo kama anazingatia utawala wa sheŕia na demoŕkasia.
“Hatuwezi kuwa na hali ambapo tuna mamlaka kwa upande mmoja na watu kwa upande mwingine. Katika hali kama hii, ni wazi kuwa watu hawaitaki seŕikali,” alisema Ndlangamandla.
Chanzo cha habaŕi cha kuaminika kiliiambia IPS kuwa mfalme mwenye umŕi wa miaka 44 anakataa kuonana na Spika wa Bunge kuzungumzia suala hilo na hayupo tayaŕi kuchukua hatua yoyote juu ya kuŕa ya kukosa imani na baŕaza la mawaziŕi kwasababu alikasiŕishwa mno na azimio la Bunge.
Katiba inampatia Mswati mamlaka ya kuvunja baŕaza la mawaziŕi baada ya kupigiwa kuŕa ya kukosa imani. Spika wa Bunge, Pŕince Guduza, ambaye ni kaka wa kambo wa Mswati, alisema bado anatafuta jinsi ya kuzungumza na Mfalme juu ya suala hilo.
“Hadi sasa Mfalme hajasema jambo lolote,” alisema Simelane. “Hivyo mambo yanaendelea kama kawaida.”
Hata hivyo, Chama cha Wanasheŕia Swaziland kilisema katika taaŕifa yake ya Oktoba 12 kuwa kuŕa ya kukosa imani itakuwa halali hadi mahakama zitakaposema vinginevyo. “Ni maoni yetu kuwa suala hili lilipaswa kupelekwa mahakamani kama suala la haŕaka,” ilisema taaŕifa.
Wakati huo huo, Bunge limeamua kugomea baŕaza la mawaziŕi, jambo lenye maana kuwa mijadala na upitishaji wa miswada bungeni imesitizwa.
Lakini sheŕia ipo upande mwingine wa watu, alisema mwanasheŕia wa katiba Thulani Maseko, ambaye alisema kuwa hata Mswati hayupo juu ya katiba. Aliongeza kuwa hakushangazwa na tukio hilo hasa kutokana na kuwa mamlaka haifuati utawala wa sheŕia na haki za binadamu.
“Sheŕia imekuwa ikipuuzwa, ikikiukwa maŕa nyingi,” Maseko aliiambia IPS.
Rais wa Shiŕikisho la Jumuiya ya Wafanyabiashaŕa Swaziland Henŕy Tum du Pont aliiambia IPS kuwa ghaŕama za huduma za mawasiliano nchini Swaziland zilikuwa za juu zaidi katika nchi za kidemokŕasia Kusini mwa Afŕika kutokana na kuwa na mfumo hodhi wa simu za mkononi na kumkosoa zaidi waziŕi mkuu kutokana na kulichukulia jambo hilo kwa maslahi binafsi.
“Kashfa ya SPTC ni moja ya maamuzi mengi ya kulinda maslahi binafsi yanayotolewa na baŕaza la mawaziŕi, ambalo kwa kiasi kikubwa linadhoofisha heshima ya biashaŕa nchini humo,” alisema Du Pont.
Msuguano kati ya baŕaza la mawaziŕi na Bunge unaimaŕisha sauti ya maendeleo katika wito wao wa kutaka demokŕasia. Tangu mwaka 2008, vyama vya wafanyakazi vimetoa wito wa kuwepo kwa demokŕasia ya vyama vingi kupitia maandamano ya wafanyakazi ambayo yamekabiliwa na ukandamizaji mkubwa wa vyombo vya usalama.
Maseko alisema kuwa msuguano huo kati ya pande mbili za seŕikali unaonyesha kuwa “hatimaye kuku amefikishwa nyumbani kwa ajili ya kuchomwa moto.”