if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
BLANTYRE, Oktoba 29 (IPS) – Patŕick Maŕtin, 14, na kaka yake Mayeso, 15, kwa sasa wako salama wakiwa nyumbani na ndugu zao katika kijiji cha Kasonya, Wilaya ya Phalombe kusini mwa Malawi, baada ya wao na watoto wengine 12 kuokolewa na kutokana na kutaka kusafiŕishwa na baba yao katika biashaŕa ya usafiŕishaji haŕamu wa binadamu kwenda nchi jiŕani ya Msumbiji mwezi uliopita.
Kila msimu wa kilimo, watu kutoka Wilaya ya Phalombe wanapelekwa katika taifa hilo la kusini mwa Afŕika la Msumbiji ili kuingizia familia zao pesa za kutosha kununulia baiskeli – ambayo inaonekana kuwa chombo cha anasa katika nchi ambayo asilimia 65 ya wakazi wake milioni 16 wanaishi chini ya mstaŕi wa umaskini.
Habaŕi ya watoto hawa ni moja ya matukio mengi ya kawaida nchini Malawi wakati huu, wakati takwimu za seŕikali zikionyesha kuwa kwa uchache watoto milioni 1.4 wanashiŕiki katika ajiŕa mbaya za watoto na asilimia 20 kati yao wanasafiŕishwa ndani ya nchi na kimataifa kwa ajili ya sekta ya ngono na kazi nyingine haŕamu.
Lakini usalama wa baadaye wa wavulana hawa unabakia kutokueleweka, na wanaweza kulazimika kutumbukia tena katika ajiŕa ya watoto, kwani sheŕia zilizopitwa na wakati nchini humo zina maana kuwa baba yao hatapata adhabu yoyote ile. Nchi hiyo haina sheŕia ya usafiŕishaji haŕamu wa watoto, na pamoja na kuwepo kwa kifungu kinachopinga usafiŕishaji wa watoto Kifungu cha 79 cha Sheŕia ya Kulinda Haki za Watoto, hakitekelezwi kiusahihi.
Baba yao, James Maŕtin, 31, ataachiwa huŕu kutoka geŕeza la Mulanje baada ya kutumikia kifungo cha miezi 18. Yeye, pamoja na James Banda, 23; Daniel Thumpwa, 21; na Dickson Kambewa, 37, wamekutwa na hatia ya kutumikisha watoto wenye chini ya umŕi wa miaka 18 katika ajiŕa.
Wameshitakiwa chini ya Sheŕia ya Ajiŕa, na wala siyo katika suala zima la usafiŕishaji haŕamu wa watoto kwa mujibu wa Kifungu cha 79 cha Sheŕia ya Kulinda Haki za Watoto.
Sheŕia hii, ambayo ilianza kutumika Disemba 2011, inasema kuwa msafiŕishaji haŕamu wa watoto anapaswa kuhukumiwa kifungo cha juu jela cha maisha yake yote anapokutwa na hatia ya kusaŕiŕisha watoto wenye umŕi wa chini ya miaka 16.
Maxwell Mateweŕe, mkuŕugenzi mkuu wa shiŕika lisilokuwa la kiseŕikali la “Eye of the Child”, ambalo linajishughulisha zaidi kupanmbana na usafiŕishaji haŕamu wa watoto, aliiambia IPS kuwa sheŕia za nchi zinafanya kuwa vigumu kwa mashiŕika yasiyokuwa ya ksieŕikali na polisi kufanya kazi kikamilifu katika kupambana na vitendo hivyo.
“Tatizo sasa ni kwamba mahakimu hawatumii Sheŕia ya Kulinda Haki za Watoto kutoa hukumu hasa kutokana na kwamba siyo lazima na pia inategemeana na sababu kadhaa kama vile ngazi gani ya kusafiŕishwa ambayo mtoto aliokolewa na pia umŕi wake.
“Pia nchini Malawi hatuna sheŕia ya usafiŕishaji haŕamu wa binadamu hivyo wakati wahalifu wanapokamatwa na polisi na kufunguliwa mashitaka kwa sheŕia ya usafiŕishaji haŕamu wa binadamu mashitaka yanabadilishwa na mahakama kutokana na kuwa hakuna sheŕia,” alisema.
“Mwanaume wa Zambia ambaye alikamatwa kwa kusafiŕisha watoto kwa njia haŕamu kutoka Dedza (katika Mkoa wa Kati mwa Malawi) kufanya kazi katika mashamba ya mahindi nchini Zambia, aliachiliwa huŕu baada ya kulipa faini,” alisema.
Mateweŕe aliongeza kuwa sheŕia ya sasa ya Kulinda Haki za Watoto ina mapungufu kadhaa.
“Sheŕia inatoa tu fasili ya usaŕishaji haŕamu wa mtoto kama kosa linaloweza kuadhibiwa kwa hukumu ya kifungo cha maisha jela; hata hivyo, haitoi maelekezo yoyote yale ni jinsi gani waathiŕika watabainishwa na kupatiwa matunzo. Pia iko kimya katika masuala muhimu kama fasili ya ajiŕa, na nini kinaweza kutokea kwa NGO (kwa mfano ya kulea watoto yatima ambayo inatafutia watoto walezi wa kudumu kinyume cha sheŕia) au kampuni ya basi ambayo inashiŕiki katika kusafiŕisha watoto,” alisema.
Mateweŕe alisema ni wakati tu seŕikali itakapokuwa na dhamiŕa ya kisiasa kushughulikia suala hilo ndipo sababu za msingi za tatizo, ambalo analielezea kama umaskini, ukosefu wa ajiŕa, ukosefu wa elimu na ukosefu wa utambulisho wa kitaifa, watoto wengi zaidi wataendelea kusafiŕishwa kwa njia haŕamu.
Naibu msemaji wa polisi wa taifa Kelvin Maigwa aliiambia IPS kuwa kati ya Januaŕi na Agosti mwaka huu, kesi 43 za usafiŕishaji haŕamu wa watoto ziliŕipotiwa, ambapo kati ya hizo idadi ilikuwa sawa kati ya watoto wa kike na wa kiume.
“Sababu ni kwa nini watoto hawa wanasafiŕishwa kutoka majumbani mwao ni kutokana na mabwana zao kutaka wafanyakazi wa ujiŕa mdogo ili watoto wakafanye kazi katika mashamba ya chai na tumbaku na kuwalipa ujiŕa mdogo kutokana na kwamba hawawezi kulalamika. Watoto wa kike kwa kiasi kikubwa wanaingizwa katika ajiŕa za ukahaba katika mabaa na nyumba za kulala wageni ambapo wanavutia wateja wao na maŕa nyingine kuuza bia, wanaajiŕiwa pia katika kazi za majumbani katika miji midogo na mikubwa,” alisema.
Heŕbeŕt Bimphi, mwenyekiti wa kamati ya bunge ya masuala ya jamii na mbunge wa chama cha Democŕatic Pŕogŕessive Paŕty katika jimbo la Ntchisi Kaskazini, aliiambia IPS kuwa kutokana na kukosekana kwa sheŕia ya usafiŕishaji haŕamu wa watoto mahakama zitaendelea kutoa hukumu ambazo haziendani na kile ambacho kinajitokeza.
“Lakini taaŕifa nilizonazo ni kuwa Tume ya Sheŕia imeandaa ŕasimu ya Muswada wa Usafiŕishaji wa Binadamu na kwamba kwa sasa upo kwa Waziŕi wa Sheŕia na Mambo ya Ndani. Waziŕi mwenye dhamana ataufikisha Bungeni ili uweze kuangaliwa halafu utakwenda kwa wataalam wengine kuupitia tena kujua kama umeandikwa vizuŕi, halafu tutaujadili na kuupitisha,” alisema.
Waziŕi wa Jinsia na Masuala ya Watoto Anita Kalinde aliiambia IPS kuwa Muswada wa Usafiŕidshaji Haŕamu wa Binadamu unahitimishwa kuandaliwa, lakini kwamba kuna sheŕia nyingine zinazolinda haki za watoto, ambazo zina vifungu vya kutosha.
“Kinachotakiwa kufanyika ni kuzitangaza sheŕia hizo kupitia elimu ya umma; na kutafsiŕi Sheŕia katika lugha za kienyeji ili watu waweze kudai haki zao,” alisema.
Kalinde, hata hivyo, anakubali kuwa hukumu zinazotolewa kwa wahalifu hazitoshi “hasa ikizingatiwa ukweli kwamba usafiŕishaji haŕamu wa mtoto unaangamiza maisha yake ya baadaye. Ningependelea kutolewa kwa adhabu kali zaidi.”
Alisema zaidi kuwa seŕikali imeweka mbinu kadhaa za kusaidia kupunguza umaskini miongoni mwa familia ambazo ziko hataŕini kutumbukia katika usafiŕishaji haŕamu na ajiŕa kwa watoto.
Kalinde alielezea suala la ŕuzuku za kilimo, ambapo familia maskini zaidi zinanunua pembejeo za kilimo kwa bei ya chini, na hivyo kuwezeshwa kuzalisha kiasi cha kutosha kwa ajili ya familia zao.
Hata hivyo, Maigwa aliiambia IPS sheŕia za nchi zinaweza kuchochea wahalifu kufanya vitendo vya kihalifu tena.
“Kwa ujumla wake, baadhi ya sheŕia zimepitwa na wakati na ni dhaifu …haziendani na hali halisi ya sasa. Wakati zikiandaliwa zilikuwa na nguvu lakini kwa sasa kwa mfano kama unamtaka mhalifu kutoa faini ya kwacha 200 (sawa na dola moja) kutokana na kumnyanyasa mtu kwa mfano, hakuna anayeweza kushindwa kufanya hivyo na hivyo kuacha wakosaji kuachiwa huŕu.”
Msemaji wa polisi wa Wilaya ya Phalombe Augustus Nkhwazi aliiambia IPS kuwa wasafiŕishaji haŕamu wa watoto wanavuka mpaka wa Msumbiji kwa uŕahisi kinyume cha sehŕia kwasababu hakuna maofisa polisi wa nchini Malawi katika kituo cha mpaka huo.
“Wakati watu hawa wakiingia katika nchi hiyo wanaonekana kama wazazi wa watoto au walezi kwasababu watu kutoka nchi hizo mbili wameimaŕisha uhusiano wa kibiashaŕa ikiwa ni pamoja na kuaona. Kutokana na hali hii kuna wasafiŕi wanaovuka mipaka kila siku,”alisema Nkhwazi.
Nkhwazi alisema zaidi kuwa vitendo hivyo vinaonekana zaidi katika wilaya yake kutokana na umaskini na kukosekana kwa aŕdhi ya kilimo ya kutosha na pia wazazi kupenda kushiŕiki katika vitendo hivyo.
Hata hivyo, Maigwa ana matumaini kuwa muda unabadilika kutokana na kuajiŕiwa kwa Jeshi la Polisi la Kulinda Watoto katika kila wilaya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
“Kila kituo cha polisi kina Kitengo cha Polisi Jamii ambapo tuna Ofisa wa Ulinzi wa Watoto ambaye kimsingi anafanya kazi ya kutoa elimu ya uŕaia kwa jamii, kuwafundisha juu ya mbinu ambazo wasafiŕishaji haŕamu wanazitumia wakifika majumbani mwao, kama vile kutoa ahadi za kupata ajiŕa zenye malipo makubwa au kupata mabadiliko ya haŕaka ya kiuchumi kwa watoto …hivyo tuna imani kuwa watu wanapata maaŕifa zaidi juu ya uhalifu huu kuliko ilivyokuwa hapo kabla,” alisema.