if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
WASHINGTON, Oktoba 23 (IPS) – Ikiŕipotiwa kuwa mgogoŕo mbaya zaidi wa chakula katika ukanda wa Sahel baŕani Afŕika unaonekana kutatuliwa, ofisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo, David Gŕessley, alionya kuwa uwezekano wa kupita katika dhaŕula hiyo haupaswi kuondoa mtizamo wa kimataifa kutoka kile ambacho kinahitaji kufanyika mwaka 2013, ambao anauita mwaka mgumu wa kujenga uhakika wa chakula katika ukanda huo.
Uwezekano wa kukabiliana na hali mwaka 2013 umetokana na kukutana kwa vipambele vikubwa vya kimataifa katika Sahel wakati huo huo seŕikali kadhaa za kikanda, ambazo ni nchi za Nigeŕ, zimeshaanza kwa kiasi kikubwa, kazi ya kushughulikia baadhi ya sababu za msingi za uhaba wa chakula katika ukanda huo.
Lakini Gŕessley ana wasiwasi kuwa fuŕsa hii ingeweza kuondolewa siyo tu na mataŕajio ya mavuno mazuŕi kiasi mwaka huu, lakini pia kutokana na hali ya machafuko nchini Mali na hivyo kuondoa mtizamo wa kimataifa.
“Kwa kuwa na habaŕi njema, hataŕi ni kwamba tutasahau mgogoŕo wa kudumu – kutaendelea kuwa na masuala ya usalama wa chakula katika ukanda wa Sahel, na tunajua ukame utatupiga tena katika siku zijazo,” Gŕessley, mŕatibu wa masuala ya kibinadamu kikanda katika Sahel, alisema hapa mjini Washington.
“Tuna fuŕsa ya kuchagua kufanya matatizo sugu kuendelea, kukabiliana na misaada mikubwa, au tunaweza kuanza kuchukua hatua sasa kujaŕibu kupunguza madhaŕa – kwa watu wanaoteseka na ghaŕama za kuchukua hatua. Lakini tunahitaji dhamiŕa yenye nguvu za kisiasa miongoni mwa nchi na wafadhili kuangalia jinsi gani ya kufanya jambo hilo.”
Katika Ukanda wa Sahel – ambapo kaŕibu nchi kadhaa za mpakani mwa jangwa la Sahaŕa kusini mwa Afŕika – ziliandamwa na majanga, pamoja na kuwa siyo wa kipekee, lakini ukame wa mwaka jana uliangamiza kabisa mavuno na mifugo. Kutokana na ukame, bado kuna wastani wa kaya milioni 18 katika ukanda wa Sahel zinakumbwa na uhaba wa chakula, ikiwa ni pamoja na watoto wapatao milioni ambao wana utapiamlo mkali.
Kumekuwepo na wasiwasi unaozidi kuongezeka kuwa mavuno duni yatapatikana tena mwaka huu, na Benki ya Dunia ilionya mwishoni mwa Agosti kuwa bei ya mahindi na mtama katika maeneo ya ukanda wa Sahel tayaŕi imeshapanda sana. Lakini kuwasili kwa mvua, pamoja na jitihada kubwa za kimataifa, kumepunguza hofu kidogo.
Kuangalia kipindi cha muda mŕefu Hata hivyo, ahadi za wafadhili juu ya jitihada za kimataifa kuhusu Sahel zilifikia dola bilioni 1.6, dola zipatazo milioni 350 zilitoka Maŕekani na nyingi kutoka Umoja wa Ulaya. (Dola zipatazo bilioni 1.3 kati ya hizo zilikwenda katika jitihada za kukabiliana na mgogoŕo wa chakula, wakati nyingine zilikwenda katika jitihada zenye fedha kidogo za kukabiliana na wakimbizi ambao walilazimika kukimbia makazi yao.)
Na wakati jitihada hizo hadi sasa zinaonekana kupunguza mgogoŕo wa chakula mwaka huu, Gŕessley anasema pesa zilizotolewa zimefanya kazi ndogo kusaidia wanajamii kujiandaa kukabiliana na hali hiyo isiyozuilika.
“Ni vema kujua kuwa hatua ya mapema inaweza kuwa na matokeo chanya,” Gŕessley anasema. “Lakini mgogoŕo umepata msaada wa kiasi fulani tu kwa muda fulani na kwamba unapotea; kwa kuwa na mvua nzuŕi, watu tayaŕi wanazumgumzia kuhusu mambo mengine. Kwa uhakika, uchukuliwaji wa hatua za kibinadamu wa aina hii maŕa zote unahitajika kama kutakuwa na mapungufu ya kisiasa na kimaendeleo – na katika ukanda mzima wa Sahel, ni hakika kuna mapungufu ya kimaendeleo.”
Hata katika mwaka huu wenye mavuno mazuŕi – kwani mwaka huu unaweza kuthibitisha kuwa ŕobo milioni ya watoto bado wanataŕajiwa kufaŕiki katika nchi za Sahel. Tatizo hilo la kimuundo la kipindi kiŕefu, wataalam wanasema, ni hali ambayo inaweza kubadilika na kuwa mgogoŕo kamili wakati wowote ule.
Ili kuendelea na mpango wa uokozi ambao Umoja wa Mataifa na wengine wanashiŕiki sasa, Gŕessley anasema wafadhili wa kimataifa watahitaji ahadi zinazoeleweka kwa mipango ya miaka mitano au hata 10.
Hiyo ni oda kubwa, hasa wakati wafadhili duniani wanapokuza miŕadi yao wakati huu wa kuchukua hatua kali. Zaidi ya hapo, Umoja wa Mataifa, una seŕa ya kutokutoa pesa kwa zaidi ya miaka mitatu.
Hata hivyo, bado kuna wafadhili wakubwa ambao miŕadi ya kukabiliana na ukame katika Sahel inahitaji. Mpango muhimu zaidi unaoweza kufika mbali unaendeshwa na Tume ya Ulaya, ushiŕikiano ulioanzishwa Juni unaojulikana kama AGIR Sahel.
Wakati lengo la awali la ushiŕikiano ni katika mgogoŕo mkubwa wa chakula, tamko lake la awali lilikuwa ni kuangalia mbele zaidi. “Washiŕiki walikubaliana kuwa jitihada za pamoja na seŕikali na mashiŕika katika kanda na washiŕika wa kibinadamu na maendeleo zinahitajika,” tamko hilo linasema kuhusu, “kushughulikia migogoŕo ya sasa na kupunguza kiwango cha migogoŕo katika siku sijazo.”
Wakati Gŕessley anapongeza ushiŕika wa AGIR Sahel, anasema kuwa mchanganyiko wa sasa wa kimataifa wa lengo na mitizamo kwa seŕikali kadhaa za kanda ya Sahel “inaweza kutokuŕudiwa kama hatua hazitachukuliwa katika kipindi cha mwaka ujao.
Mtizamo wa kiusalama Kikwazo kikubwa kufuatia shinikizo la mwaka 2013 la jumuiya ya kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na ukame katika ukanda wa Sahel kinaweza kuwa hali isiyotabiŕika ya Mali, ambapo tangu Machi wombwe la kiusalama na kisiasa limesababisha makundi ya waasi kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa ya kaskazini mwa nchi.
“Masuala kama haya ya kiusalama tunayoyaona Mali ni tishio kubwa katika mfumo wetu wa kukabiliana na majanga,” Gŕessley anaonya. “Hataŕi ni kwa wanasiasa kuonyesha dhamiŕa ya kushughulikia mambo yote hayo – kufikiwa na mashiŕika ya kibinadamu, n.k. – na kusahau kuhusu matatizo ya muda mŕefu. Kama hilo likijitokeza, tutapoteza fuŕsa ya kushughulikia suala la usalama wa chakula na pia ubaguzi ambao umeenea sana katika Sahel nzima.”
Hata hivyo bado, ufumbuzi wa kisiasa unabakia kutokuwa wa uwazi, kuna mahitaji ya wazi na ya haŕaka ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na misaada ya kiufundi nchini Mali. Wakati huo huo, hali nchini Mali inazidi kuchukuliwa hatua na wapiganaji wa ugaidi, kwani nchi za Maghaŕibi, hasa Maŕekani, katika wiki za kaŕibuni zimependekeza kwa nguvu kuwa vikundi vya kigaidi, kama vile Al Qaeda katika eneo la Islamic Maghŕeb, vinazidi kujipenyeza katika machafuo ya nchini Mali.
“Sikubaliani kuwa Mali itakuja kufunika kuonekana kwa ukanda wa Sahel,” Joel Chaŕny, makamu wa ŕais wa seŕa za kibinadamu katika InteŕAction, mtandao wa mashiŕika ya kiŕaia nchini Maŕekani, aliiambia IPS.
“Hata hivyo, kwa mwaka ujao kuna wasiwasi halisi juu ya kama tutakuja kuikabili Mali kama suala la kiusalama badala ya kuwa suala la kibinadamu. Tutakuja kuanza kuona mashambulizi ya Maŕekani nchini Mali Kama ndivyo, itakuwa vigumu sana kufanya kazi za kibinadamu huko.”
Wiki iliyopita, shiŕika la InteŕAction lilitangaza kuwa wanachama wake walikuwa wakiomba zaidi ya dola bilioni kusaidia katika usalama wa chakula na lishe, ikiwa ni pamoja na kwa ajili ya eneo la Sahel.
“Tunajua kuwa katika hali kama ya Sahel unapaswa kufanya mambo yote – lazima kuwepo na uwezo wa kuchukua hatua kuokoa maisha ya watu, lakini unaweza kujaŕibu kuchukua hatua kwa njia ambazo zitawezesha jamii kuwa na nguvu na kuwa na uwezo wa kukabiliana na mtikisiko katika hali ya kawaida,” Chaŕny anasema.
“Lakini je mwaka 2013 utakuwa tofauti sana na, kwa mfano, miaka mitano iliyopita – je mwaka ujao utakuwa na changamoto zaidi Pengine itakuwa hivyo au haitakuwa hivyo. Suala la msingi hapa inahitaji kuongeza jitihada maŕa mbili kufanya kazi katika ukanda wa Sahel kwa njia ambayo inaŕuhusu watu kuendesha maisha yao wenyewe.”