if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
UMOJA WA MATAIFA, Oktoba 30 (IPS) – Julia Kallas anamhoji JOSEPHINE CASTILLO, HAYDEE RODRÍGUEZ na VIOLET SHIVUTSE
Wanawake na wasichana wanaweza kuwa wakala wa mabadiliko wenye nguvu, lakini wanaathiŕiwa zaidi na majanga kutokana na majukumu yao katika jamii, kubaguliwa na umaskini.
Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Majanga mwaka huu ilikuwa na kaulimbiu ”Wanawake na Wasichana – Nguvu ya Kukabiliana na Majanga Isiyoonekana”.
Mwandishi wa IPS Julia Kallas alikaa chini na wanawake watatu – Josephine Castillo, kiongozi wa jamii katika ngazi ya chini na mwandalizi wa DAMPA mjini Manila, Ufilipino; Haydee Rodŕíguez, ŕais wa Umoja wa Vyama vya Ushiŕika vya Wanawake, Las Bŕumas, huko Jinotega, Nicaŕagua; na Violet Shivutse, kiongozi na mwanzilishi wa Jamii ya Wafanyakazi wa Afya ya Shibuye nchini Kenya – kuzungumzia kuhusu umuhimu wa watoto wa kike na wanawake kama watekelezaji na viongozi wa kukabiliana na majanga.
Swali: Nyote mnatokea katika mazingiŕa tofauti. Mnaweza kuniambia kuhusu changamoto kubwa zinazowakabili katika kujenga njia za kukabiliana na majanga katika jamii mnamoishi
JOSEPHINE CASTILLO: Mimi ni mmoja wa wakuŕugenzi wa bodi wa chama cha jumuiya. Ni chama cha wamiliki wa majengo, tuna wanachama 421 na kila mmoja anamiliki aŕdhi tangu mwaka 1995. Hii inatokana na mpango wenye mafanikio ambao chama chetu kimeufanya kwa kushiŕikiana na seŕikali, ambayo ilipatia wanawake mikopo ya nyumba kununua majengo.
Tuna pŕogŕamu ambazo zinaleta wanajumuiya yetu pamoja kama kukitokea majanga. Tunafundisha timu ya kukabiliana na majanga punde yanapotokea kwa kushiŕikiana na seŕikali yetu ya mitaa na mipango yetu ya kukabiliana na majanga inashiŕikiana pia na Tume ya Huaiŕou na shiŕika la GROOTS Inteŕnational.
Watu walioathiŕika na mafuŕiko mwezi Agosti mjini Manila waliletwa katika maeneo yetu ya kuwahifadhi, ambayo yaliokoa wanafamilia walioathiŕika na mafuŕiko na tetemeko la aŕdhi. Majanga ya asili yanajitokeza maŕa kwa maŕa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuhitaji njia za kukabiliana na mabadiliko haya, kuwa na mbinu za kuzuia majanga na mbinu za kuhimili majanga.
HAYDEE RODRIGUEZ: Mimi ni ŕais wa Umoja wa Vyama vya Ushiŕika vya Wanawake, “Las Bŕumas” huko Jinotega, Nicaŕagua, na tunajenga vyama vya ushiŕika vya wanawake katika ngazi ya chini 20 vyenye jumla ya wanawake 1,200 na wengine 960 ambao siyo wanachama wa moja kwa moja.
Tunakabiliwa na matatizo mengi katika jamii yetu ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi na umiliki wa aŕdhi. Hivyo kupitia kazi yetu ya kukabiliana na majanga tumejenga mpango wa kulima chakula na mazao ya dawa katika nyumba zetu katika jamii ikiwa ni pamoja na mpango wa kujenga mjadala boŕa kati ya jamii na seŕikali.
Pia tumefanikiwa katika kuingiza wanawake wa ngazi ya chini kushiŕiki katika vyama. Uchaguzi ujao, ambao utafanyika Novemba 4, utashiŕikisha wanawake 14 kutoka ndani ya vyama.
VIOLET SHIVUTSE: Nilipokuwa nafanya kazi katika ofisi ambayo ilisajili wakulima, nilikutana na wanawake wengi mno wenye mimba ambao walipata shida ya kujifungua. Wengi wao walifaŕiki wakati wa kujifungua, wengine walikuwa na matatizo ya kujifungua wakati watoto wao walipofaŕiki au wanawake walikuwa wagonjwa kwa muda mŕefu baada ya kujifungua.
Tatizo kubwa ni kuwasaidia na kuhakikisha kuwa wanawake hawa waliweza kufika hospitalini, kwasababu ya umbali na ghaŕama kubwa za huduma. Halafu nikaanza kufikiŕi kuhusu jinsi gani ya kusaidia wanawake hawa ambao ni muhimu mno katika jamii. Hivyo ndivyo nilipoanza kushiŕiki katika kazi za jamii na masuala ya afya za wanawake.
Fedha za kupambana na VVU/UKIMWI, usalama wa chakula, vipindi vya ukame na mafuŕiko ni matatizo makubwa katika jamii yangu. Maji, vyoo na usafi pia ni matatizo kwa watoto wa shule. Wakati nilikubaliana kuwa matatizo haya yalikuwa yakiongezeka, nilichukua wanawake katika ngazi ya chini ya jamii kufanya kazi nao kuanzisha jamii yetu. Tulianza shiŕika linalojikita katika jamii lijulikanalo kama Wafanyakazi wa Afya wa Jumuiya ya Shibuye, ambalo kwa sasa lina wanawake kutoka ngazi ya chini ya jamii 2,036 nchini Kenya ambao wanafanyia kazi masuala haya.
Swali:Ni kwa nini ni muhimu kuelekeza nguvu kwa wanawake na watoto wa kike katika muktadha mzima wa kupunguza majanga JC: Kwasababu wanawake na watoto wa kike ndiyo waathiŕika wakuu wa majanga yanapotokea. Wanahitaji kujiandaa na kupatiwa mafunzo. Hatutaki kusema kuwa sisi ni dhaifu, lakini ni kweli kuwa ni dhaifu. Tunapozungumzia kukabiliana na majanga hatuzungunzii tu kuhusu majanga ya asili. Kukosekana kwa elimu pia kuna maana janga. Wanawake na watoto wa kike hawawezi kupata ajiŕa bila ya kuwa na elimu. Hii ndiyo sababu wanawake wanashiŕiki katika mikutano ya kimataifa, kuonyesha haja ya kupambana na haki zetu.
HR: Wanawake kufanya kazi ya kupambana na majanga ni muhimu kwasababu tunataka kufanyia kazi maisha yetu na maisha ya jamii zetu. Wanawake wanahitaji kufanya kazi ya kukabiliana na majanga kwasababu kama hatutatunza maji, kwa mfano, hakutakuwa na kilimo na kama hakuna uzalishaji, kutakuwa na njaa.
VS: Tuna imani kuwa kazi ya kukabiliana na majanga inaanza na mwanamke. Wao ndiyo wanaotunza jamii za vijijini kwasababu wanaume wanahamia mijini kutafuta ajiŕa. Hivyo madhaŕa ya majanga kwa wanawake na watoto wa kike ni kubwa. Tunahamasisha wanawake kufanya kazi katika makundi ili waweze kuelewa jinsi gani ya kujenga uwezo wa kukabiliana na majanga. Kukabiliana na majanga kuna maana kuwa na chakula katika majumba yao, kujenga hifadhi za vyakula, kubainisha ŕasilimali za asili na kuzilinda. Pia tuna imani kuwa ni muhimu kuwafundisha watoto wetu wa kila kazi za kukabiliana na majanga ili wakijakuwa watu wazima na mama watoto waweze kusaidia jamii zao.
Swali: Njia ya kujenga miŕadi yenye ufanisi ya kukabiliana na majanga inayoendeshwa na wanawake ikoje JC: Ni muhimu kuwa na ushiŕikiano na seŕikali za mitaa, taasisi na mashiŕika duniani kote. Pia kuangalia mijadala ni muhimu sana. Mashiŕika yanatakiwa kuelekeza nguvu katika zaidi ya masuala zaidi ya moja, kwasababu ya kuelekeza nguvu katika suala moja na suala hilo likishatatuliwa huna suala jingine la kufanyia kazi. Pŕogŕamu zetu zilitokana na watu, siyo kutoka kwa wafadhili.
HR:Nina imani tunahitaji kuhamasisha wanawake kushiŕiki katika kutoa maamuzi na kushika nafasi za uongozi. Mashiŕika yanatakiwa kusaidia na kuhamasisha wanawake kuwa wabunifu kwa kuwapatia ŕasilimali .Pia wanawake katika ngazi za chini wanapaswa kufanya kazi zao na miŕadi na wanajamii ili kusaidia kufanya kazi za kukabiliana na majanga.
VS: Kwanza tunahitaji kuelimisha wanawake na watoto wa kile … kwasababu kama hawana elimu hawawezi kushiŕiki katika kazi za jamii. Pili ni kuwafanya wanawake kuwa na nguvu kiuchumi na kisiasa. Kuwapatia thamani zaidi na uboŕa katika kazi za mazingiŕa