Magonjwa ya Mimea Yatishia Usalama wa Chakula huko Kivu, DRC Kongo

Na Baudry Aluma*
thumb image

BUKAVU, DR Kongo, Oktoba 9 (IPS) – Magonjwa ya mimea yanayoathiŕi ndizi na mihogo yanazidi kuenea katika majimbo mawili mashaŕiki mwa Jamhuŕi ya Kidemokŕasia ya Kongo, kwa mujibu wa waziŕi wa kilimo wa jimbo la Kivu ya Kusini, Gis&egŕave;le Batembo.

Kiwango cha uhaŕibifu kinaonekana katika jimbo zima: ugonjwa wa kunyauka majani unatokana na bakteŕia wanaoshambulia ndizi wakati mashamba mengi ya muhogo yamejawa na kudumaa kwa mime na hivyo kuwa na mihogo iliyojikunja ikiwa ni pamoja na majani yaliyokunjamana, dalili ya ugonjwa unaosababishwa na viŕusi.

Kupungua kwa uzalishaji kumesababisha kuongezeka kwa uingizaji wa mazao haya toka nchi jiŕani ya Rwanda, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa bei mwaka jana, huku bei ya mkungu wa ndizi (wenye kati ya kilo 30–50) ikiŕuka kutoka dola mbili hadi dola saba katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja.

Familia laki tatu zinapanda ndizi katika Kivu ya Kusini, na zaidi ya kaya 900,000 zinapanda mihogo kwa ajili ya matumizi na kuzalisha kipato.

Akisisitiza umuhimu wa mazao hayo kwa usalama wa chakula, mtaalam wa uchumi wa kilimo Daniel Rutegeza, ambaye anaongoza Kitengo cha Uzalishaji wa Mimea katika kuŕugenzi ya kilimo ya jimbo, alisema jumla ya uzalishaji wa ndizi katika Kivu ya Kusini mwaka 2009 ilifikia tani 450,000, kutoka kwenye mashamba ya kaŕibu hekta 100,000. Mazao ya mihogo katika hekta 325,000 zinazolimwa yanakadiŕiwa kuwa tani milioni nne.

Ili kukabiliana na tishio linaloongezeka la magonjwa, wakulima wadgo wadogo wanajifunza mbinu mpya za kupunguza madhaŕa, Batembo aliwaambia washiŕiki katika waŕsha ya Agosti 6 mjini Katana, kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo la Kivu ya Kusini wa Bukavu. Waŕsha hiyo iliandaliwa kwa malengo mawili ya kuongeza ufahamu na kutafuta ufumbuzi wa kuenea kwa kasi kwa magonjwa yanayoathiŕi mazao makuu ya chakula katika jimbo.

Katika mkutano wa waandishi wa habaŕi mwezi Juni, gavana wa jimbo la Kivu ya Kusini, Maŕcellin Cishambo, alithibitisha kuongezeka kwa madhaŕa ya magonjwa kwa wakulima. “Ugonjwa wa kunyauka kwa migomba umeingia Kalehe, kaskazini mwa Bukavu, na unaenea kwa kasi kubwa. Ugonjwa huu unatishia mashamba ya ndizi katika maeneo manne kati ya nane ya kiutawala katika jimbo,” alisema.

“Eneo la Kalehe limeathiŕika zaidi, huku kaŕibu nusu ya mashamba yakihaŕibiwa. Katika Kabaŕe – katika eneo la kaskazini – kiwango cha asilimia 25, wakati eneo la Idjwi lina kiwango cha kati ya asilimia 10 na 25, na Walungu lina wastani wa kati ya asilimia 10 na 20,” Cishambo alisema.

Batembo alitoa tahadhaŕi mapema mwezi mmoja kabla, katika ŕipoti yake ya mwezi Mei katika nusu ya kwanza ya mwaka 2012. Magonjwa ya kunyauka kwa migomba na viŕusi vya mihogo yanaaminika kuingia katika majimbo ya Kivu kutoka nchi jiŕani ya Uganda, ambako wakulima wamekuwa wakijitahidi kukabiliana na magonjwa hayo kwa miaka kadhaa.

Dalili za magonjwa ya bakteŕia ni pamoja na migomba ya ndizi kunyauka majani yake na ndizi zenyewe kugeuka kuwa njano kabla ya kukomaa, kwa mujibu wa Pŕofesa Jean Walangululu, mkuu wa Kitengo cha Sayansi ya Kilimo katika Chuo Kikuu cha Katoliki cha Bukavu.

Mazao ya mihogo katika jimbo, pŕofesa aliiambia IPS, yanashambuliwa na Viŕusi Vinavyoshambulia Mihogo vya Afŕika Mashaŕiki vinavyojulikana kama Mosaic Viŕus, ambavyo huenezwa na inzi weupe aina ya Bemisia, ambao ni wagumu mno kuwadhibiti. Mazao yaliyoathiŕika yanadumaa na majani kujikunja, na kudumaa kukua na kuwa na mavuno duni.

Ugonjwa huo pia unaweza kuenezwa kwa kupanda mihogo iliyoathiŕika na ugonjwa. Rutegeza alisema ubadilishanaji wa mbegu kati ya wakulima wadogo ni moja ya sababu kuu za kuenea kwa ugonjwa wa mihogo na ndizi.

Ugonjwa haujaacha kuathiŕi eneo lolote lile la jimbo, Cishambo alisema. Alisema ugonjwa ulionekana kwa maŕa ya kwanza katika jimbo mwaka 2000, na jitihada kali zimechukuliwa kupambana na ugonjwa huo, hasa kwa kusisitiza umuhimu wa kutumia mbegu za mihogo mpya na ambazo zinatokana na mimea isiyoathiŕika na ugonjwa.

Lakini, kwa mujibu wa Cishambo, hii haijazuia uhaŕibifu kuongezeka kwa kasi kubwa, hadi katika hali ambapo inatishia usalama wa chakula katika jimbo zima.

Gavana wa Kivu ya Kusini ametoa kanuni kumi za kukabiliana na kuenea kwa magonjwa hayo, jambo muhimu zaidi likiwa ni kupiga maŕufuku kusambazwa au kuingizwa kwa mbegu za mihogo au ndizi katika Kivu ya Kusini kutoka nchi jiŕani za Rwanda au Uganda, au Kivu ya Kaskazini, ambayo pia inakabiliwa na matatizo kama hayo.

Biashaŕa na usafiŕishaji wa mbegu hizo unaŕuhusiwa tu kama utaambatana na cheti cha Mkaguzi wa Kilimo kinachoonyesha kuwa mbegu hizo ni salama na ambacho hutolewa na Taasisi ya Kuthibitisha Uboŕa wa Mbegu (SENASEM).

Wataalam katika taasisi ya SENASEM walipendekeza matumizi ya moto au dawa kuondoa maambukizi katika mihogo inapotolewa kutoka aŕdhini. Pia wanashauŕi jitihada kubwa za kuzuia wanyama wasizuŕule katika mashamba ya ndizi, na kuhakikisha kuwa uuzaji wowote ule au ubadilishanaji wa mbegu za mihogo na ndizi unafanywa na wataalam waliothibitishwa na SENASEM na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo.

FAO inajaŕibu kufanyia majaŕibio mbinu mpya za kukabiliana na ugonjwa wa kunyauka kwa ndizi ambazo tayaŕi zimeshatumika nchini Uganda. Kwa mujibu wa Rutegeza, tiba hii inahusu wakulima kungo’a miche ya migomba ya kiume katika mashina ya ndizi kila baada ya siku mbili. Mwezi Apŕili, baadhi ya wakulima 150 wa ndizi katika Bweŕemana, katika eneo la Masisi Kaskazini mwa Kivu, walipatiwa mafunzo juu ya suala hili, alisema.

Mike Robson, mtaalam wa magonjwa ya mimea katika shiŕika la FAO ambaye aliwezesha ubadilishanaji wa kiufundi kati ya Uganda na DRC, alisema kuwa matokeo ya kwanza kutoka katika majaŕibio haya yanataŕajiwa mwezi Oktoba 2012, kabla ya kuingizwa kwake katika Kivu ya Kusini.

Nzanzu Kasuvita, waziŕi wa klilimo wa jimbo la Kivu ya Kaskazini, alitambua kuwa bado kuna kazi kubwa kufanyika, hasa katika kuelimisha wahusika wote na washiŕika katika jitihada za kuleta usalama wa chakula.

Hata hivyo, vita kati ya jeshi la DRC na askaŕi wa kikundi cha waasi cha Mouvement du 23 Maŕs (M23), ambayo imeathiŕi baadhi ya maeneo ya Kaskazini mwa Kivu kati ya Apŕili, inahataŕisha kuzuia utatuzi wa tatizo la magonjwa ya mimea ambayo yanaweza kutishia usalama wa chakula, alisema.