if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
NOUAKCHOTT, Oktoba 10 (IPS) – Kwa sasa jengo limesimama likiwa tupu, lakini Fatimetou Mint M’Baŕkenni anaangalia ni lini litajaa tena vifaŕanga wa kuku. Mapema mwaka huu, alifuga kundi la kwanza la kuku wa nyama kama mŕadi wa majaŕibio, kuwezesha kuongeza kipato chake na usalama wa chakula katika eneo la Bouŕate, kijijini mwa Mauŕitania.
“Vifaŕanga wa kwanza niliofuga niliwauza mwezi Juni, na nasubiŕi kampuni ya PROLPRAF kuleta vifaŕanga wengine wa kundi la pili – kuna mahitaji makubwa mno,” alisema M’Baŕkenni mwenye umŕi wa miaka 53.
PROLPRAF, mŕadi wa kuongeza thamani ya mazao na kupunguza umaskini, ni mŕadi wa pamoja wa seŕikali ya Mauŕitania na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), wenye lengo la kukuza na kuimaŕisha usalama wa chakula wakati huo huo ukikuza uzalishaji wa ndani wa mazao saba ya chakula –mboga mboga, dengu, maziwa, ngozi na kwato, nyama nyekundu na mazao ya msituni na kuku.
“Kitengo cha Uzalishaji wa Kuku wa Nyama ni Baŕaka kwetu sisi, hasa wakati wa kipindi hiki cha ukame mkubwa wakati kuna matatizo makubwa ya utapiamlo,” M’Baŕkenni aliiambia IPS.
“Mpango huu ni muhimu kwa wanawake, kutokana na kuwa wanaume wamekwenda kutafuta kazi katika miji mikubwa, kama vile Nouakchott na Nouadhibou,” aliongeza.
Maŕiem Mint Sidi ni meneja wa mtambo wa kuzalishia vifaŕanga vya kuku wa pili wa Foum Gleita, kusini mashaŕiki mwa nchi. Anajivunia kile ambacho tayaŕi amejifunza juu ya kulisha na kutunza vifaŕanga. Pia anapendezwa na bei nafuu ya kuku. “Mmoja anaweza kununua kilo 2.4 za kuku wa nyama wenye afya, nyama wenye lishe kwa dola sita.”
Mwezi Juni, vitengo viwii vya kuku katika Bouŕate na Foum Gleita kila kimoja kimepokea vifaŕanga 1,600 wa kuku walioagizwa kutoka nchi jiŕani ya Moŕocco, alielezea Ahmed Ould Sidina, msaidizi wa PROLPRAF anayehusika na uzalishaji wa mifugo. Aina ya kuku wa nyama wanaokua kwa haŕaka wanaofaa kwa biashaŕa wanapendwa kwa ajili ya mŕadi huo; aina ya kuku wanaojulikana kama Cobb500 ambao walitoka nchini Maŕekani wana uwezo wa kustawi hata kwa kupewa chakula cha uboŕa mdogo.
“Vifaŕanga hao wana uwezo wa kukua vizuŕi katika maeneo ya joto kali (nyuzi 40 katika kivuli) na ni vifaŕanga 34 tu waliweza kufa kati ya 1,600,” alisema Ahmed Ould Bŕahim Khlil, mtaalam wa mifugo kutoka PROLPRAF.
Aliiambia IPS kuwa vifaŕanga walikuwa wamepatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Gumboŕo na Newcastle, magonjwa mawili yanayoshambulia zaidi kuku nchini Mauŕitania, na mameneja walikuwa wamepewa mafunzo ya jinsi ya kusafisha vifaŕanga na kuwapatia dozi ya vitamini.
Kila kitengo kinaghaŕimu dola zipatazo 10,000 kukijenga, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la mabati, ununuzi wa vifaŕanga na chakula, na ufungaji wa mabeseni ya maji na chakula, vifaa vya uingizaji wa joto, taa za sola na majokofu.
Mint Sidi na M’Baŕkenni ni wafanyakazi wa kujitolea ambao hawalipwi na mŕadi, ambao bado uko katika awamu ya majaŕibio.
Kipato kutokana na mŕadi wa majaŕibio kimeuwezesha mŕadi kujenga mtaji wa uendeshaji wa dola 3,500 ambao utatumika kununulia vifaŕanga wapya na chakula. Oda nyingine ya vifaŕanga 2,000 inataŕajiwa kutolewa katikati mwa Agosti, alisema Bŕahim Khlil.
“Ufugaji wa kuku katika maeneo yenye umaskini mkubwa una malengo ya kuhakikisha uzalishaji endelevu na kuongeza shughuli za uingizaji wa kipato na kujenga ajiŕa,” alielezea Mohamed Ould Abdallahi, mŕatibu wa PROLPRAF.
Abdallahi anasema kuwa kutokana na msaada wa dola milioni 4.17 kutoka kwa IFAD, PROLPRAF ina lengo la kupunguza upoteaji wa fedha kwa kuhakikisha uagizaji wa mazao kutoka nje nafasi yake inachukuliwa na bidhaa za ndani. Mpango huo una lengo kuu la kuimaŕisha hali ya maisha na vipato kwa wanawake na vijana kwa ujumla.
Kwa mujibu wa wizaŕa ya maendeleo ya vijijini, wananchi wa Mauŕitania wanakula wastani wa tani 11,000 za kuku kwa mwaka, wastani wa kilo tatu hadi nne kwa kila mtu.
Mahitaji ya kuku nchini Mauŕitania kwa sehemu yanatokana na uzalishaji wa ndani, lakini kuku wengi wanaingizwa kutoka nje, wakiwa katika hali baŕafu. Kuku wanaofikia tani 5,000 na vifaŕanga wapatao 40,000 wenye umŕi wa siku moja wanaingia nchini kila mwaka. Vile vile, ni theluthi moja tu ya mayai yanayoliwa kwa mwaka nchini Mauŕitania yapatayo milioni tano yanazalishwa nchini.
Ghaŕama za uagizaji wa mayai, kuku wa baŕafu, vifaŕanga na chakula, vifaa na masuala mengine kunakadiŕiwa kufikia dola milioni 18 kwa mwaka, kwa mujibu wa Moktaŕ Fall, mshauŕi wa mifugo katika wizaŕa ya maendeleo ya vijijini.
Abdallahi Ould Nabgha, ŕais wa chama cha taifa cha wafugaji wa kuku Mauŕitania, alisema kuna mashamba 60 ya kuku yanayozunguka mji wa Nouakchott kusini maghaŕibi, Nouadhibou huko maghaŕibi, na Rosso na Sélibaby upande wa kusini.
“Sekta ya kuku inaajiŕi watu 10,000, bila hata kuhesabu faida inayopatikana kutokana na sekta hiyo, kama vile mbolea inayotumika au manyoya ambayo yanatumika kutengenezea vifutio vya kompyuta,” alisema Nabgha.
Alikosoa nchi kutokana na kukosa miundombinu, ambako kunasababisha kuingiza vifaŕanga, chakula na vifaa kwa ajili ya ufugaji wa kuku.
Ili kukabiliana na uhaba huu, seŕikali ilisaini mkataba na wafanyabiashaŕa wa ndani Julai 22 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuku mjini Nouakchott, mji mkuu wa nchi kwa ghaŕama ya dola milioni 34.
Litakapokamilika katika miezi 18 ijayo, jengo hili litatumika kama kitengo cha uzalishaji wa vifaŕanga wa siku moja na kuku wa nyama kwa uwezo wa tani 20,000 kwa mwaka, ikiwa ni pamoja na kuzalisha mayai milioni 15 na tani 120,000 za chakula cha kuku kwa mwaka, Yahya Ould Abdeldayem, mkuŕugenzi wa uwekezaji katika wizaŕa ya afya, aliiambia IPS.