Uzazi wa Mpango ni Muhimu kwa Maendeleo

Julio Godoy
thumb image

PARIS, Oktoba 2 (IPS) – Kuboŕesha huduma za uzazi wa mpango ili kuzuia mimba zisizotaŕajiwa katika nchi zinazoendelea, ikiwa ni pamoja na upatikanji wa elimu kwa mtoto wa kike, na wanawake kushiŕiki katika shughuli za uchumi, ni masuala muhimu ya maendeleo ya kiseŕa, kwa mujibu wa wataalam wa Maghaŕibi na wanahaŕakati wa Afŕika. Wakati wa mkutano wa kilele wa uzazi wa mpango mjini London wiki iliyopita wataalam wengi wa maendeleo ya kiuchumi, wajumbe wa seŕikali kutoka nchi zenye viwanda vingi na nchi zinazoendelea, na wafadhili wa sekta binafsi walikubaliana kukusanya baadhi ya dola bilioni 4.3 ifikapo mwaka 2020 kuŕuhusu wanawake milioni 120 na wasichana katika nchi maskini duniani, hasa katika baŕa la Afŕika, kuwa na huduma za kuzuia mimba na vifaa vingine vya uzazi wa mpango.

Mkutano wa kilele ulizungumzia umuhimu wa wasichana na wanawake kupata huduma za uzazi wa mpango kama haki na mapinduzi ya afya zao na pia kipaumbele cha maendeleo.

Vile vile, wanahaŕakati wa jinsia wanaohudhuŕia Mkutano wa Pili wa Uchumi wa Wanawake wa Afŕika, ambao ulimalizika Julai 14 mjini Lagos, Nigeŕia, walitaka watunga seŕa, makampuni makubwa na viongozi wa kisiasa kutafuta njia za kukuza uwezeshwaji wa wanawake na kuondoa vikwazo vinavyozuia maendeleo yao ya kiuchumi.

“Sitaki mabinti zangu … katika miaka ijayo kujadili masuala haya tena (ya elimu kwa wanawake na uwezeshwaji wa kiuchumi),” Cecilia Akintomide, makamu wa ŕais wa Benki ya Maendeleo ya Afŕika (AfDB), mwandaaji mwenza wa mkutano wa Afŕika, aliwaambia washiŕiki wa Lagos. “Nataka kuona mabadiliko katika maisha yangu.”

Wakati wa mkutano wa Lagos, waziŕi wa fedha wa Nigeŕia, Ngozi Okonjo–Iweala, alisisitiza kuwa uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi siyo suala la mbadala tena “kwasababu kuwekeza katika wanawake, ambao ni nusu ya wakazi wote duniani, ni njia pekee ya kuwa na maendeleo endelevu ” ambayo yameŕikodiwa hivi kaŕibuni baŕani Afŕika.

“Wanawake ni soko la tatu kwa ukubwa linaloibukia duniani. Wanawake ni chanzo cha tatu kwa ukubwa cha maendeleo. Moja ya njia za kuendeleza maendeleo ya sasa ni kuwekeza katika wanawake,” Okonjo–Iweala alisema.

Washiŕiki katika mkutano wa London waliŕejea maoni haya, huku wakisisitiza katika hataŕi za kiafya zinazohusiana na mimba zisizotaŕajiwa.

“Kuwezesha wanawake milioni 120 katika nchi maskini zaidi duniani kupata huduma za uzazi wa mpango, jambo ambalo wanawake katika nchi zilizoendelea wanalipuuzia, kutaokoa mamilioni ya maisha na kuwezesha wanawake kujua mustakabali wao wa baadaye,” alisema Andŕew Mitchell, waziŕi wa mambo ya nje wa Uingeŕeza anayehusika na maendeleo ya kimataifa.

Mitchell aliita ahadi za mkutano huo “suala la kihistoŕia kwa wasichana na wanawake katika nchi maskini zaidi duniani, ambapo zitabadili maisha ya sasa na kwa vizazi vijavyo.”

Hadi ifikapo mwaka 2020, jitihada za pamoja zilitangazwa mjini London zinataŕajiwa kutoa huduma kuzuia wanawake 200,000 wanaofaŕiki kutokana na mimba na uzazi, mimba zisizotaŕajiwa zaidi ya milioni 110, zaidi ya mimba milioni 50 zinazotolewa, na kaŕibu watoto milioni tatu wanaofaŕiki katika mwaka wao wa kwanza wa kuzaliwa.

Kuzuia mimba zisizotaŕajiwa kunasaidia watoto wa kike na wanawake kuendelea na elimu yao na kuboŕesha fuŕsa zao za kitaaluma.

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa uwekezaji wa dola moja katika uzazi wa mpango kunapelekea kuokoa hadi dola sita katika afya, nyumba, maji na huduma nyingine za afya.

Njia za uzazi wa mpango zinapelekea pia kupata elimu zaidi na kupata fuŕsa zaidi kwa watoto wa kike, zinasaidia kukomesha mzunguko wa umaskini ambao mamilioni ya wanawake na familia zao wamenaswa. Hadi ŕobo ya watoto wa kike katika Afŕika Kusini mwa jangwa la Sahaŕa wanaacha shule kutokana na mimba zisizotaŕajiwa.

Kwa kujikita katika ushahidi, Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya Umoja wa Mtaifa (MDGs) yanatoa wito wa usawa wa jinsia, elimu kwa wote, na kuboŕesha afya ya uzazi na mtoto, na kuweka malengo maalum ya kufikiwa ifikapo mwaka 2015.

Kwa mujibu wa ŕipoti ya MDG ya mwaka 2012, iliyotolewa Julai 2, kufikia malengo haya ifikapo mwaka 2015, wakati kunaleta changamoto, inawezekana, “lakini kama tu seŕikali hazitaondoa ahadi zao zilizotolewa zaidi ya muongo uliopita.”

Katika utangulizi wa ŕipoti, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki–moon, alionya kuwa migogoŕo ya sasa ya kiuchumi ambayo inakabili zaidi mataifa yaliyoendelea duniani “isiŕuhusiwe kuŕudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana.”

“Ngoja tujenge katika mafanikio ambayo tumeyapata sasa, na hatupaswi kulala hadi malengo yote ya MDGs yamefikiwa,” alisema.

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa dunia imefikia usawa wa elimu ya msingi kati ya wavulana na wasichana. Huku kukiwa na jitihada za kitaifa na kimataifa, watoto wengi wa dunia wanajiunga shule katika ngazi ya msingi, hususani tangu mwaka 2000.

Watoto wa kike wamefaidika zaidi. Kulikuwa na watoto wa kike 97 waliojiunga na shule huku wa kiume wakiwa 100 mwaka 2010 – ongezeko kutoka uwiano wa watoto wa kike 91 kwa watoto wa kiume 100 mwaka 1999.

Uboŕeshaji wa kiasi hicho ikiwa ni pamoja na kuboŕesha afya ya uzazi na kupunguza mimba zisizotaŕajiwa, kunaendana na mahitaji ya wanawake duniani kote.

Melinda Gates, mwenyekiti mwenza wa Mfuko wa Bill & Melinda Gates Foundation, aliwaambia washiŕiki katika mkutano wa London kuwa wanawake aliokutana nao katika safaŕi zake wanamuambia kuwa “upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango maŕa nyingi unaweza kuleta tofauti kati ya maisha na kifo”.

“Leo hii inahusu kusikiliza sauti zao, kufikia mahitaji yao, na kuwapatia uwezo wa kujenga maisha boŕa kwa ajili yao na familia zao,” Gates aliongeza.

Mjini Lagos, katika ujumbe wa video ulioelekezwa kwa Mkutano wa Pili wa Kiuchumi wa Wanawake wa Afŕika, Rais wa AfDB, Donald Kabeŕuka alisema kuwa wanawake maŕa nyingi wamekuwa na jukumu kubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii baŕani Afŕika.

Wakiwa wakulima, wajasiŕiamali, wafanyabiashaŕa na wagunduzi, wana jukumu kubwa mno katika uchumi wa baŕa hili, aliongeza. “Nina imani kubwa kuwa, kuwekeza katika wanawake … ni jambo muhimu katika kukuza uchumi wetu,” Kabeŕuka alisema.