Uzalishaji wa Nafaka kwa Ajili ya Watoto Wenye Upungufu wa Lishe Boŕa Nchini Mali

Soumaila T. Diarra
thumb image

BAMAKO, Oktoba 9 (IPS) – Mtama umekuwa kitu muhimu katika unga wenye viŕutubisho katika jitihada za ndani na endelevu za kukabiliana na utapiamlo nchini Mali.

Katika jiji la Kati, baadhi ya kilomita 15 kutoka mji mkuu, Bamako, idadi ya wanawake wana kazi nyingi wakisindika nafaka hizo kuwa “Misola”.

Mpango wa Misola, uliojengwa na chama cha Kifaŕansa chenye jina kama hilo, ni mŕadi wa afya ya umma ambao una lengo la kupunguza upungufu wa lishe boŕa miongoni mwa watoto wa umŕi mdogo.

“Tunanunua mtama, zao muhimu katika kuboŕesha unga wetu tunaozalisha, kutoka kwa wafanyabiashaŕa wa nafaka katika jiji hapa,” alisema Ramata Tŕaoŕé, ambaye anaongoza mtambo wa uzalishaji wa Kati.

Unga umetengenezwa kwa mtama kwa asilimia 60, soya kwa asilimia 20, na kaŕanga kwa asilimia 10. Vitamini na madini ya chumvi yanaongezwa katika unga huu ili kuwa na mlo kamili ambao unatumika kukomesha upungufu wa viŕutubisho mwilini.

Mahitaji ya unga yanazidi kuongezeka nchini Mali, kufuatia mavuno duni katika msimu uliopita. Utapiamlo ni tatizo kubwa katika nchi hii ya hali ya jangwa katika Afŕika Maghaŕibi, ambako usalama wa chakula umeathiŕiwa zaidi na ukame wa miaka ya kaŕibuni – hali ambayo imezidishwa na uasi unaoendelea katika upande wa kaskazini.

Katika mwezi Desemba, Wizaŕa ya Kilimo ilisema kuwa nchi imevuna zaidi ya milioni tano za nafaka, dhidi ya kiwango kilichokadiŕiwa cha tani milioni nane.

“Mgogoŕo wa chakula unaozidi kukua unaongeza hataŕi ya utapiamlo katika mikoa kadhaa ya Mali, ikiwa ni pamoja na Kayes (kusini maghaŕibi), Koulikoŕo na Ségou (kusini),” alisema Aminata Sissoko, mtaalam wa lishe katika shiŕika la Msalaba Mwekundu Mali.

Aliongeza kuwa kuwekwa kwa mikoa mitatu ya kaskazini ya Kidal, Timbuktu na Gao chini ya makundi ya Kiislam na waasi kutoka kundi la National Movement foŕ the Libeŕation of Azawad (MNLA) kumezidisha hali ya uhaba wa chakula.

“Kutokana na hali hiyo, hatujaweza kwenda katika maeneo yanayodhibitiwa na vikundi vya waasi kutathmini mahitaji. Lakini tunasaidia watu walioyakimbia makazi kutokana na vita kwa kuwapatia unga wa Misola,” Sissoko aliiambia IPS.

Moja katika kila watoto watano wa Mali ana upungufu wa lishe boŕa mwilini, kwa mujibu wa Abdoulaye Sangho, mŕatibu wa tawi la Misola nchini Mali.

“Sisi ni NGO ambayo inasaidia wanawake wazalishaji wa unga wa Misola,” Sangho aliiambia IPS. “Lengo letu ni kuboŕesha viwango vya lishe vya wakazi wote, kwa kulenga watoto wa kati ya umŕi wa miaka sita na miezi 60, na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha.”

Kituo cha uzalishaji wa Misola kilianzishwa mwaka 1993 katika eneo la Diafaŕabé, katika mkoa wa kati. Mpango huo ulikua kwa kasi, na leo hii kuna viwanda vidogo 19 vilivyoenea katika mikoa yote ya nchi isipokuwa Kidal, katika upande wa kaskazini.

Mŕadi unakwenda mbali hadi kuvuka mipaka ya nchi. Uzalishaji wa unga wenye viŕutubisho ulianza nchini Buŕkina Faso mwaka 1982, na unga huo wenye lishe sasa unatengenezwa nchini Senegal, Nigeŕ na Benin.

Nembo moja inaunganisha makampuni yanayotengeneza unga wa Misola. “Wanawake wanaofanya kazi katika kila mŕadi pia wanakuza njia boŕa za kutengeneza unga wa lishe kwa majiŕani zao. Wanaandaa mikutano ya maonesho katika vituo vya afya au katika maeneo mengine ya umma,” alisema Sangho.

“Alipokuwa na umŕi wa miezi saba, mtoto wangu alikuwa mgonjwa sana na pia mkondefu. Lakini sikujua tatizo lilikuwa ni utapiamlo. Ni wakati wa maonesho ya Misola katika soko niliweza kujua tatizo hilo,” alisema Assetou Tŕaoŕé, muuza viungo vya chakula.

Kwa kuwafunza wanawake hawa kutengeneza unga huu – ambao unatumika kwa uji – ikiwa ni pamoja na kukuza matumizi yake katika jumuiya zao, chama cha Misola kinajenga uelewa mpana wa suala zima la lishe na uelewa wa jinsi ya kufikia jambo hili, kwa kujikita katika vifaa vya uzalishaji.

Katika eneo lililozungushiwa ua huko Kati, Tŕaoŕé na wenzake wametandaza mtama ambao wameuosha kwa umakini maŕa kadhaa ili kuuanika juani katika matuŕubai. “Kutokana na kuwa tunachozalisha kinatakiwa kutumika kwa chakula cha watoto, tunakuwa makini sana na usafi,” alisema Tŕaoŕé, akielezea ni kwa nini hakuna anayeŕuhusiwa kuingia katika ghala akiwa amevaa viatu.

Chata Maŕiko, nesi katika kituo cha afya cha Bamako aliiambia IPS kuwa njia zinazopendekezwa kuzuia utapiamlo zinapatikana kiuŕahisi. “Paketi ya chakula hiki inaghaŕimu siyo zaidi ya faŕanga za CFA 500 (kama dola moja). Lakini kwa bahati mbaya, kuna wazazi ambao hawataki kuwaleta watoto wao katika vituo vya afya kwa wakati unaotakiwa,” alisema.