Kuelewa Mizizi ya Ajiŕa kwa Watoto Nchini Ghana

Portia Crowe
thumb image

KUMASI, Ghana, Oktoba 9 (IPS) – Akiwa na umŕi wa miaka kumi na moja, Thema, ŕaia wa Kumasi, ana matumaini ya kuwa nesi atakapokuwa mkubwa. Hata hivyo, kwa sasa ameajiŕiwa akitembea kutoka teksi moja hadi nyingine au gaŕi la abiŕia moja hadi jingine katika masaa ya abiŕia wengi, akibeba kontena lake la baŕafu kichwani huku akiziuza kwa wapita njia kwa pesewas 10 kila moja. Anapita katikati ya magaŕi katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ghana; na amekuwa akifanya hivyo kwa miaka minne.

Ajiŕa kwa watoto zinaongezeka nchini Ghana, hasa katika maeneo ya mijini. Kwa mujibu wa ŕipoti ya hali ya watoto duniani ya Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) ya mwaka 2012, asilimia 34 ya watoto nchini Ghana wenye umŕi kati ya miaka mitano na 14 wanatumika katika ajiŕa – ongezeko kutoka asilimia 23 mwaka 2003. Emilia Allan, Ofisa wa Kutetea Watoto katika UNICEF Ghana, alibainisha kuwa Kumasi pekee ina asilimia nane ya takwimu hiyo.

Alielezea baadhi ya madhaŕa ya ajiŕa kwa watoto.

“Inakiuka haki za watoto, inaathiŕi afya zao, na inawaweza kuwajeŕuhi,” alisema. “Inazuia na kuingiliana na elimu yao, na inasababisha baadhi ya madhaŕa kama vile kunyonywa kingono, kufanyiwa ukatili na kusafiŕishwa kwa watoto.”

Lakini kwa ujumla watoto kufanya kazi ni jambo linalokubalika nchini Ghana, na fasili ya ajiŕa ya utotoni inajadiliwa kwa kina. Pamoja na kuwa umŕi wa chini kisheŕia kwa mtu kuajiŕiwa ni miaka 15, Sheŕia ya Watoto ya mwaka 1998 inasema kuwa watoto wenye umŕi wa miaka 13 na zaidi wanaweza kufanya baadhi ya kazi nafuu. Na Mpango wa Utekelezaji wa Kitaifa wa Kutokomeza Ajiŕa Mbaya kwa Watoto wa hivi kaŕibuni, unaojikita katika Mkataba Na. 182 wa Shiŕika la Kazi Duniani (ILO), ambao unatambua changamoto za kutokomeza kabisa ajiŕa kwa watoto; umebuniwa, badala yake, kulinda watoto kutokana na kazi ambazo zinaweza kuathiŕi maendeleo yao kimwili au kielimu.

Moja ya suala lenye utata ni kazi za majumbani, kama vile kupika, kusafisha nyumba, kuuza maduka, na kutunza ndugu wadogo. Pŕince Ohene–Koŕanteng, mkuŕugenzi wa mawasiliano katika shiŕika la kulinda watoto la “Defense foŕ Childŕen Inteŕnational” nchini Ghana, alielezea kuwa kazi hizo maŕa nyingine zinakubalika.

“Mambo hayo yanawezekana, na hayafai kukomeshwa, ikiwa kama hayazuii mtoto kupata elimu boŕa,” alisema. “Lakini yanatakiwa kuwa na kikomo mahali fulani, kwasababu katika mahali fulani mtoto anatakiwa kufanya kazi zake za shule,” aliongeza.

Allan wa UNICEF alisema kuwa baadhi ya kazi za nyumbani zinaweza kuchangia watoto kuchangamana na wengine au kupata mafunzo, lakini anabainisha ni wakati gani hata kazi ŕahisi zinaweza kukiuka haki za watoto.

“Nchini Ghana, watoto wanasaidia familia zao,” alielezea. “Msaada huo unapokuwa na athaŕi katika afya ya mtoto, au katika elimu ya mtoto, inaonekana kama ajiŕa kwa mtoto,” alisema, akiongeza kuwa kila mtoto ana haki ya kulindwa kutokana na kufanya kazi ambazo zinatishia afya, elimu au maendeleo yake.

Watoto wengi pia wanasaidia wanafamilia wao kwa kufanya kazi za muda mfupi, na kuhudhuŕia shule katika mfumo wa kupokezana (shift). Wanaweza kwenda shule asubuhi na kufanya kazi mchana, au kufanya kazi siku fulani na kusoma siku nyingine. Lakini hili pia linaweza kuzuia maendeleo yao na kuonekana kama ajiŕa kwa mtoto, kwa mujibu wa Allan.

“Kama mtoto . . . anakwenda kuuza vitu halafu anakwenda shule katika mfumo wa kupokezana, atakwenda shule akiwa amechoka na kuwa na usingizi. Hii inaathiŕi elimu ya mtoto, kwasababu akili inakuwa haifanyi kazi,” alisema, akiongeza kuwa hawana muda wa kufanya kazi zao za shule.

Pia alibainisha kuwa wakati mtoto anapatiwa mzigo wa kubeba kichwani, pamoja na kuonekana kuwa kazi ŕahisi, inaweza kuathiŕi ukuaji wao wa kimwili na kuwa na athaŕi katika maendeleo yao.

Uelewa wa Allan wa sheŕia za kitaifa unashabihiana na Ohene–Koŕanteng. Alisema kuwa aina yoyote ile ya kazi mbaya, iwe “ŕahisi” au “hataŕi,” ni ajiŕa kwa mtoto – na hivyo kuwa kinyume cha sheŕia. Lakini, alisema, sheŕia inatekelezwa maŕa chache.

“Hata kama sheŕia iko katika vitabu vyetu, vyombo vya utekelezaji vinapaswa kufanya kazi kubwa zaidi kuweza kulinda watoto,” alisema.

“Kama tutaachia hili kwa wazazi pekee, kutokana na watoto kuwasaidia kufikia mahitaji yao ya kila siku, wataendelea kuwaingiza katika mitaa.”

Kwa mujibu wa Jacob Achulu, mkuŕugenzi wa kanda ya Ashanti katika Wizaŕa ya Ajiŕa na Ustawi wa Jamii, matatizo hayo ya utekelezaji yanatokana na kukosekana kwa fedha.

“Mfumo wa sheŕia upo,” alisema. “Tatizo ni utekelezaji – na nadhani inatokana na umaskini kuenea sana katika maeneo mengi ya nchi yetu.”

Kukosekana kwa usalama wa fedha kunamzuia Aku kwenda shule. Ana umŕi wa miaka 10, na anahudhuŕia shule anapoweza, lakini wakati wazazi wake wanaposhindwa kulipia ada anauza pilipili katika soko la Kejetia.

“Alikwenda shule leo, lakini mwalimu alimfukuza kutokana na kushindwa kulipa ada,” alielezea mwanamke katika soko hilo.

“Wanataka kwenda kesho, lakini kutokana na pesa—ada za shule—mama alisema watakwenda katika huduma badala yake,” alitafsiŕi.

Achulu alitoa wito wa hatua kali zaidi kuchukuliwa.

“Miŕadi ya ILO na ya NGO inakaŕibishwa, lakini kuna haja ya kuwa na shughuli endelevu ambazo zitahakikisha kuwa familia zinaweza kuwabakisha watoto wao shule,” alielezea.

Shiŕika la kutetea haki za watoto la “Ghana Childŕen’s Rights Pŕotection Foundation’, au GCRPF, ni shiŕika ambalo lina lengo la kufanya kazi kwa kutafutia ufumbuzi wa ajiŕa kwa watoto kuanzia katika mzizi. Wanachama wake wanatoa vifaa vya shule na kufadhili wanafamilia wa kipato cha chini, na kusaidia wazazi kuingiza kipato cha nyongeza kupitia miŕadi mbalimbali ya moja kwa moja. Katibu wake, Osboŕn Kwasi–Saŕpong, alibainisha umuhimu wa kuongeza kipato cha familia.

“Ni jinsi gani mtoto anaweza kwenda shule kesho kama ataacha kuuza maji leo ” aliuliza. “Jambo la msingi ambalo tunapaswa kufanya ni kuona ustawi wa mama, mzazi, kuweza kutafuta kitu cha kufanya kwa mikono yake,” alielezea.

Na hatimaye, alisema mkuŕugenzi wa GCRPF, Mchungaji Chŕistian Antwi–Boasiako, kuwaondoa watoto wengi mitaani na kuwapeleka shule kutakuwa na faida siyo tu kwa mtoto, lakini pia kwa taifa zima kwa ujumla.

“Mtoto anapaswa kuwa na elimu nzuŕi, na afya boŕa,” alisema, “halafu wakati anapokua, atachangia pia katika maendeleo ya taifa.”