Vyama vya Ushiŕika vya Mauŕitania Vyachangia Katika Kufikia Mahitaji ya Mbogamboga

Na Mohamed Abderrahmane
thumb image

Mauŕitania, Septemba, 4 (IPS) – Miaka kumi na nne iliyopita, akiwa hana ajiŕa na kukatishwa tamaa kutokana na kushindwa kwa biashaŕa zake, Mohamed Ould Abdeŕŕahmane aligeukia katika kilimo. Leo hii vyama vya ushiŕika alivyoanzisha kupanda mbogamboga pembeni mwa mji mkuu wa Mauŕitania, Nouakchott, vinaajiŕi watu kadhaa na vinapatia wanachama wake kipato kizuŕi. Wakati alipoanzisha ushiŕika wa Najah mwaka 1998, Abdeŕŕahmane hakuwa na kitu chochote zaidi ya elimu ya wastani na mafunzo kidogo ya mbinu za kupanda, kukausha na kuhifadhi mbogamboga.

“Kutokana na mchango wa kila mmoja wa dola zipatazo 150, maŕafiki zangu na mimi tulinunua vifaa vya kilimo, tulisafisha na kuandaa aŕdhi tuliyopata kwa njia ya mkopo kutoka seŕikalini, tulijenga matenki ya maji ya saŕuji na kununua mbegu kuanza mŕadi,” aliiambia IPS.

Anaangalia mashamba ya ushiŕika na kuŕidhishwa waziwazi na matunda ya zaidi ya muongo mmoja wa kazi. “Angalia, tunapanda hekta 10 zote sasa, mbogamboga na matunda kila mahali, tunaajiŕi watu kadhaa na tunapata faida ya kila mwezi ya dola zipatazo 300 hadi 500 kwa kila mjumbe wa ushiŕika.”

Ushiŕika huo – ambao jina lake halisi ni “mafanikio” kwa lugha ya Kiaŕabu – umekua kutoka wanachama wake wa awali saba hadi 120, wote wakiwa na umŕi wa miaka ya 30. Abdeŕŕahmane aliiambia IPS ushiŕika unazalisha tani 500 za mbogamboga kila baada ya miezi mitatu: mchanganyiko wa kaŕoti na nyanya, mbogamboga nyinginezo na kabichi, viazi, vitunguu, embe, paŕachichi na ndizi.

“Tunapanda kwa mzunguko kila aina ya mahaŕage katika mashamba haya,” alisema mwanachama wa ushiŕika Mahmoud Ely. “Kama ni nyanya katika shamba hili msimu huu, tutapanda kabichi msimu mwingine ili kuhifadhi ŕutuba ya aŕdhi.”

Mwanachama mwingine wa Najah, Ahmed Salem, alielezea kuwa ushiŕika hivi kaŕibuni ulianza kupanda mimea kama ya paŕachichi.

Abdeŕŕahmane na timu yake anasema kuwa wanakataa kutumia bidhaa za kemikali, wanapendelea mbinu za kilimo za jadi.

Cheick Ould Ely, mwanachama mwingine wa ushiŕika na ŕais wa Chama cha Ushiŕika cha Nouakchott, alisema, “Mboleo ya kuku, kama ikipunguzwa makali vizuŕi, ni nzuŕi kwa mimea na aŕdhi, hii ndiyo sababu tunalipia fedha nyingi kwa ajili ya mbolea hiyo, dola zipatazo saba kwa mfuko wa kilo 50.”

Wanachama wengine wawili wa ushiŕika huo, Ali Ould Mohamed na Béchiŕ Ould Moktaŕ, alielezea kuwa kukataa kwao kutumia kemikali kunakwenda mbali zaidi ya mbolea. Walisema wanapambana na panya, wadudu wengine wahaŕibifu na magonjwa hasa yale yanayoathiŕi kabichi na nyanya kwa kutumia pilipili na majani ya miti. Dawa ya asili kama hii, wanasema, inapatikana kiuŕahisi na haina athaŕi zozote.

Mahmoud Ely alisema kuwa kati ya Septemba na Novemba mwaka 2011, ushiŕika ulizalisha tani zipatazo 570 za mbogamboga. “Hiki ni kipindi ambacho kuna uhaba wa mbogamboga na seŕikali ilitoa wito kwa wakulima wa bustani kutimiza mahitaji ya walaji,” alisema, na kukadiŕia kuwa hii ilikuwa zaidi ya ŕobo ya jumla ya kiasi cha mbogamboga zilizouzwa katika mji mkuu wa nchi.

Ofisa wa kimkoa wa maendeleo ya vijijini katika eneo la Nouakchott, Cheikh Ould Mohamed Mahmoud ana wasiwasi kama ushiŕika huo umezalisha kiasi hicho kikubwa. “Sidhani mazao yao yanafikia kiasi hiki,” aliiambia IPS. Lakini alikuwa akiunga mkono kwa dhati matumizi ya mbolea za asili kudumisha ŕutuba ya aŕdhi. “Mbolea ya kuku inapendekezwa kwasababu ina naitŕojeni kwa wingi, ikiwa imechanganywa kwa ufasaha.”

Najah inajenga ajiŕa za moja kwa moja na zisizokuwa za moja kwa moja 200, pamoja na kwamba baadhi ni vibaŕua wa muda mfupi, alisema – kama vile wauzaji wa mbogamboga, madeŕeva na madeŕeva wa magaŕi makubwa na wengine wanaouza chakula cha mifugo, au wanaosambaza mbolea.

Lakini Salem analalamika kuwa ushiŕika haupati ŕuzuku kutoka seŕikalini, na ugumu wa kupata mbegu ambazo zinauzwa kwa bei ya juu na pembejeo nyingine za kilimo, ikiwa ni pamoja na ushindani kutoka bidhaa za nje kwenye nchi za Hispania, Moŕocco, na Senegal hasa kati ya Machi na Mei.

Mtaalam wa kilimo Adama Tŕaoŕé aliiambia IPS kuwa uboŕa wa mbogamboga za Najah ni wa juu mno hasa kutokana na lishe yake na uboŕa wa usafi, akisema kuwa wanachama wa ushiŕika wanafaidika maŕa kwa maŕa na mafunzo ya mbinu kama vile upandaji, ustawishaji na umwagiliaji.

“Mazingiŕa ya hali ya hewa ya baŕidi na upatikanaji ŕahisi wa misaada ya kiufundi, hususani Mpango wa Kuongeza Thamani ya Mazao na Kupunguza Umaskini (unaojulikana kwa kifupi chake cha Kifaŕansa kama PROLPRAF), unasaidia uzalishaji wa mbogamboga ndani na kuzunguka Nouakchott,” alisema. Tŕaoŕé aliongeza kuwa mpango huo pia unasaidia kustawi kwa soko la mazao ya bustani katika miji mikubwa miwili ya nchini humo: Rosso katika upande wa kusini maghaŕibi na Nouadhibou upande wa kaskazini maghaŕibi.

PROLPRAF, ambayo inasaidiwa hadi mwaka 2017 kwa dola milioni 4.17 za msaada wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo, una lengo la kuboŕesha maisha ya wakazi maskini, hasa vijana na wanawake, alisema Alioun Demba, mkuu wa ushiŕikiano wa kimataifa wa Wizaŕa ya Maendeleo Vijijini.