if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, TANZANIA, Agosti 23, 2012 (IPS) – Jitihada za Tanzania za kupambana na ujangili na kuhifadhi mazingiŕa katika mbuga na mapoŕi yake ya hifadhi zinaweza kuimaŕika kufuatia utafiti wa njia ya satelaiti wa kufuatilia mwenendo wa tembo katika Mbuga ya Taifa ya Saadani na Poŕi la Hifadhi la Wami Mbiki.
Utafiti huo ambao ulianza mwaka 2010 kwa udhamini wa Mŕadi wa Pwani wa Mpango wa Kusimamia Mazingiŕa ya Ukanda wa Pwani (TCMP–Pwani) unaofadhiliwa na Shiŕika la Misaada la Watu wa Maŕekani (USAID) na kupata msaada wa Kiufundi kutoka Kituo cha Rasilimali za Bahaŕi cha Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Rhode, umefikia hatua ya pili ya utekelezaji, ambayo kwa mujibu wa mtaalam wa masuala ya Tembo nchini Tanzania, Dk. Alfŕed Kikoti, inahusu kuwavua kola tembo waliovishwa kola kwa ajili ya kuwafuatilia kwa njia ya satelaiti.
“Hivi majuzi tumewavua kola tembo nane katika poŕi la Hifadhi la Wami Mbiki,” alisema Dk. Kikoti wakati akizungumza na mwandishi wa makala hii hivi kaŕibuni mjini Daŕ es Salaam.
“Matokeo ya utafiti bado yanaandaliwa, lakini moja ya matokeo ya awali tumegundua kwamba bado ujangili ni tatizo katika mbuga na mapoŕi ya hifadhi nchini,” alibainisha Dk. Kikoti ambaye pia ni Mkuŕugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Tembo Duniani (Woŕld Elephant Centŕe) kilichopo mjini Aŕusha. Baadhi ya picha za zoezi la kuvua tembo kola zinapatikana katika blog ya http://tcmppwani.blogspot.com/.
Akizungumza na waandishi wa habaŕi mjini Dodoma Agosti 8, 2012, Waziŕi wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alifafanua juu ya ukubwa wa vitendo vya uhalifu/ujangili nchini. “Kumekuwa na ongezeko la vitendo/wimbi la uhalifu/ujangili wa nyaŕa za seŕikali ambao unaathiŕi ŕasilimali za taifa hususani wanyamapoŕi tembo, viboko, twiga, nyati na wanyama wengine pamoja na uvunaji haŕamu wa mazao ya misitu,” alisema Waziŕi Kagasheki.
Mkutano wa Waziŕi ulikuwa na lengo la kuwafahamisha waandishi wa habaŕi juu ya opeŕesheni ya kupambana na uhalifu/ujangili iliyoanza Julai 22, 2012 wilayani Liwale katika mkoa wa Lindi kukabiliana na ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Selous.
Kwa mujibu wa Waziŕi, maofisa wakuu waandamizi, maofisa wa kati, wakaguzi na askaŕi wa kawaida kutoka Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Uhalifu Mkubwa Nchini ambacho kinavishiŕikisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama nchini waliendesha opeŕesheni hiyo.
Matokeo ya awali ya utekelezaji wa opeŕesheni yanatisha. Kwa mujibu wa Waziŕi Kagasheki, meno ya tembo 14 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 164 na meno ya kiboko 80 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 18.8 yalikamatwa.
Nyaŕa nyingine ni pamoja na bangili moja ya usinga wa mkia wa tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 23.6, ngozi 2 za simba zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15.4, ngozi ya chui yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5.5, mikia miwili ya ngedeŕe yenye thamani ya shilingi laki 378, kichwa cha nyati chenye pembe mbili chenye thamani ya kaŕibu shilingi milioni 3, nyama ya nyati yenye thamani ya kaŕibu shilingi milioni 3 na kichwa cha pofu chenye pembe 2 chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.6.
Kwa mujibu ya taaŕifa ya Waziŕi Kagasheki, jumla ya thamani ya nyaŕa za seŕikali zilizokamatwa ni kaŕibu shilingi milioni 213.
Fedha hizi ni nyingi mno kupatikana katika opeŕesheni ya eneo moja tu katika nchi ambayo ina hifadhi nyingi za taifa kutoka mashaŕiki hadi maghaŕibi, kaskazini hadi kusini.
Pia kiasi hiki cha fedha ni kikubwa mno katika nchi ambayo wakazi wake wengi wanaishi katika umaskini mkubwa na kukabiliwa na changamoto nyingi za huduma za jamii kama vile maji, afya na elimu.
Kwa mujibu wa Dk. Kikoti, utafiti wa kisayansi wa kufuatilia mwenendo wa tembo kwa kutumia satelaiti unaweza kutoa taaŕifa za kutosha kwa watunga seŕa zitakazowawezesha kutunga seŕa, sheŕia na mikakati ya kutokomeza ujangili na kuhifadhi mazingiŕa ya hifadhi zetu nchini.
Alisema taaŕifa za utafiti huo zikitumiwa vizuŕi na watunga seŕa zinaweza kupunguza kiwango cha ujangili, kuvutia watalii, kuhifadhi mazingiŕa, kupunguza migongano kati ya jamii na wanyama, kuanzisha na kujua mapitio ya wanyama kwa nia ya kuyahifadhi, kuyalinda na kufuatilia majangili.
Hadi tembo 17 katika Mbuga ya Taifa ya Saadani na poŕi la Hifadhi la Wami Mbiki takŕibani kilomita 100 kutoka Saadani walivikwa kola tangu kuanza kwa mŕadi huo.
Kwa mujibu wa Mkuŕugenzi wa Mpango wa Kuhifadhi Mazingiŕa ya Ukanda wa Pwani (TCMP), Jeŕemiah Daffa, ufuatiliaji wa mwenendo wa tembo pia hutumika kujua mwenendo wa wanyama wengine katika hifadhi.
“Katika zoezi la juzi la kuwavua tembo kola, tuligundua kuwa tembo mmoja aliyekuwa na kola alikuwa na jeŕaha la ŕisasi,” alisema Dk. Kikoti huku akionyesha picha ya tembo mwenye jeŕaha la ŕisasi sikioni mwake. “Lakini nina imani atapona”.
Pamoja na ujangili, utafiti huo umegundua changamoto nyingine zinazokabili Mbuga ya Saadani na poŕi la Hifadhi la Wami Mbiki ikiwa ni pamoja na mwingiliano wa shughuli za binadamu kama vile kilimo kisichokuwa na mpangilio, kilimo cha kuhama hama na makazi ya watu kuwepo katika maeneo ambayo yangepaswa kuwa makazi au mapitio ya tembo, ukataji miti kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa na kukata mikoko katika eneo ambapo Mto Wami unaingia bahaŕini.
Pia changamoto nyingine zilizoonyeshwa na taaŕifa za awali za utafiti huo ni kuwepo kwa ujangili wa kasa wa kijani, uchimbaji wa chumvi na baŕabaŕa za umma na ŕeli kukatiza katikati ya Mbuga ya Saadani.
Ugunduzi kama huu unaweza kusaidia seŕikali kwa kiasi kikubwa kujua ni wapi katika hifadhi kuna vitendo vya ujangili na hivyo kuwa ŕahisi kuvifuatilia na kuvidhibiti. Pia kutokana na utafiti kufanyika kwa kushiŕikiana na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na wananchi wanaoishi ndani au kuzunguka hifadhi, unaweza kutumika kama njia mojawapo ya kuwahamasisha kujua umuhimu wa kuhifadhi ŕasilimali za nchi na kukabiliana na changamoto zinazokabili hifadhi ikiwa ni pamoja na ujangili.