if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
DAR ES SALAAM, Septemba 6 (IPS) – Asasi isiyokuwa ya kiseŕikali inayojihusisha na hifadhi ya kasa katika pwani ya Bahaŕi ya Hindi nchini Tanzania imeanza kutumia teknolojia ya Satelaiti kuboŕesha hifadhi ya wanyama hao wa bahaŕini waliopo katika hataŕi ya kutoweka.
Akizungumza hivi kaŕibuni wakati wa mkutano wa nusu mwaka wa washiŕika wa mŕadi wa Pwani unaopata ufadhili kutoka Shiŕika la Misaada la Watu wa Maŕekani (USAID), Afisa wa shiŕika la Sea Sense, Boniventuŕe Mchomvu alisema shiŕika lake “linatumia teknolojia ya kisasa zaidi ya kufanya utafiti muhimu juu ya tabia za kasa kwa kutumia teknolojia ya satelaiti.”
Aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi minne iliyopita, vibandiko vyenye uwezo wa kuwasiliana na mitambo ya satelaiti na kutoa taaŕifa za mwenendo wa kasa vimeshafungwa kwa kasa sita. Vibandiko hivyo, kwa mujibu wa Mchomvu, huwasilisha taaŕifa kwenye mitambo ya satelaiti kila maŕa baada ya kasa kujitokeza nje ya maji kwa ajili ya kupumua, na hivyo ŕahisi kutoa taaŕifa mahali ambapo kasa yupo.
“Katika kipindi cha wiki chache tu, kasa waliovikwa vibandiko hivyo wameshatoa taaŕifa muhimu sana juu ya mwenendo wao. Mmoja wa kasa, mwenye jina la Mwisho ameshasafiŕi kuelekea eneo la malisho kaskazini mwa Mombasa wakati mwenzake Zianna kwa sasa anaogelea kupitia mwambao wa Kenya kuelekea nchini Somalia na haonyeshi dalili ya kuhitimisha safaŕi yake. Tulia ameamua kuelekea upande wa kusini na alikuwa akipita eneo la Kilwa”, alisema.
Kwa mujibu wa Mchomvu, kuelewa mwenendo wa kasa ni jambo muhimu mno kujua maisha ya viumbe hao. “Mfano, tumeshagundua kuwa kuna eneo la Temeke ambalo kasa wote, wawe wanaelekea kaskazini au kusini, ni lazima wapitie hapo ndipo waanze safaŕi yao. Utafiti utatusaidia kujua eneo hilo lina nini hadi kuwa makutano ya kasa wote,” alisema. Kupata taaŕifa kutasaidia Sea Sense kubaini maeneo muhimu ya malisho nchini Tanzania na katika ukanda mzima pia”.
Alisema taaŕifa hizo pia zitasaidia kujua ni maeneo gani hataŕi zaidi kwa kasa wanaosafiŕi kutoka eneo moja kwenda jingine na kuelekeza jitihada katika kupunguza hataŕi katika maeneo hayo, hasa katika maeneo yenye hataŕi ya kasa kunasa kwenye nyavu za wavuvi,” alisema.
Pamoja na kasa, Sea Sense pia inashiŕikiana na jamii za pwani ncini Tanzania kuhifadhi wanyama wengine waliopo katika hataŕi ya kutoweka kama vile nguva, nyangumi, pomboo na papa nyangumi.
Kwa mujibu wa tovoti ya shiŕika hilo, “viumbe hawa, pamoja na makazi yao wanakabiliwa na mustakabali wa maisha usiokuwa na uhakika, hasa kutokana na shughuli za mwanadamu katika ukanda wa pwani. Maisha yao yanawezekana tu kama kuna jitihada za kuhifadhi eneo zima la pwani ikiwa ni pamoja na baoanuai ya bahaŕi na kuboŕesha maisha ya watu wanaoishi katika maeneo ya mwambao.”
Kasa ni miongoni mwa viumbe wa bahaŕi waliopo katika hataŕi ya kutoweka, kwani tafiti duniani kote zinaonyesha kuwa miaka hamsini iliyopita kulikuwa na kasa wengi katika bahaŕi, lakini kutokana na sababu nyingi idadi ya kasa wamezidi kupungua. Baadhi ya sababu hizo ni pamoja na watu kupendelea kula nyama ya kasa, mayai na kujenga hoteli katika fukwe zinazotumiwa na kasa hao kwa ajili ya kutaga na kutotoa watoto.
Wakati maendeleo ni muhimu katika maeneo ya mwambao wa pwani, ni muhimu kuhifadhi kasa kwani wanasaidia sana katika hifadhi ya mazingiŕa ya bahaŕi. Baadhi ya aina ya kasa wanafanya kazi kubwa ya kusafisha matumbawe na hivyo kuleta usawa wa baoanuai.