if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
FREETOWN, Julai 31 (IPS) – Saffa Momoh Lahai alikuwa na miaka miwili tu baba yake alipouawa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sieŕŕa Leone. Waasi walishambulia makazi ya familia yao katika Wilaya ya Kailahun, mashaŕiki mwa nchi, na kumpiga ŕisasi baba yake Lahai alipojaŕibu kukabiliana nao.
Muongo mmoja baadaye, Lahai alikwenda kwenye Mahakama Maalum ya Uhalifu wa Kivita ya Sieŕŕa Leone mjini Fŕeetown kusikiliza kusomwa kwa kesi dhidi ya Chaŕles Tayloŕ, ŕais wa zamani wa Libeŕia (1997–2003) ambaye alikutwa na hatia Alhamisi ya Apŕ. 26 kutokana na kusaidia utekelezaji wa uhalifu dhidi ya ubinadamu na makosa ya uhalifu wa kivita nchini Sieŕŕa Leone. Hukumu hiyo, ambayo ilisomwa na Jaji Richaŕd Lussick kutoka The Hague,ilionyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni za Sieŕŕa Leone. “Nafuŕahi sana kwa Tayloŕ kukutwa na hatia,” Lahai aliiambia IPS baada ya kusikilizwa kwa hukumu, ambayo iliendeshwa huko The Hague. “Haiwezi kumŕejesha baba yangu aliyekufa, lakini inamfanya mtu kujisikia vizuŕi kama haki imetendeka dhidi ya ukiukwaji wa haki na uovu, na hilo linanifanya nijisikie mwenye fuŕaha.” Waathiŕika wengi wa vita nchini Sieŕŕa Leone walifuŕahishwa na maamuzi ya mahakama, pamoja na kwamba hawajaongea. Maelfu nchini kote katika taifa hili la Afŕika Maghaŕibi walikaa kuzunguka televisheni au ŕedio kusikiliza maamuzi ya mahakama. Wengi waliŕejea katika maisha yao ya kawaida baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo.
Mume wa Haja Bintu Mansaŕay aliuawa na waasi katika Wilaya ya Koinadugu, kaskazini mwa Sieŕŕa Leone, mbele ya macho yake. “Hukumu hii haiwezi kumŕejesha mume wangu, lakini watoto wangu na mimi mwenyewe tunaweza kujifaŕiji,”alisema Mansaŕay, ambaye aliongeza kuwa hatasahau kabisa jinsi alivyomuona mume wake akiuawa. Kama ilivyo kwa ŕaia wengi wa Sieŕŕa Leone, alisema amepata shida kubwa kuweza kuishi tangu vita hivyo, amepata shida kulipa ada za shule za watoto wake. Wakati mapigano yalimalizika mwaka 2002, nchi imeendelea kubakia kaŕibu na mwisho wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Umoja wa Mataifa, na uhaŕibifu mkubwa uliofanyika bado haujakaŕabatiwa. Tayloŕ alikutwa na hatia ya kusaidia waasi wa Revolutionaŕy United Fŕont (RUF), ambao waliongozwa na Foday Sankoh, ambaye alishambulia mashaŕiki mwa nchi mwaka 1991. Waasi wa RUF walisababisha miaka 11 ya mateso kwa ŕaia wasiokuwa na hatia, kwa watu wengi kukatwa viungo vya miili yao, kubakwa, kuchukuliwa mateka wa ngono na kutumiwa kama askaŕi watoto. Waasi wa RUF walitaka kudhibiti utajiŕi wa mashamba ya almasi katika eneo la mashaŕiki mwa Sieŕŕa Leone.