Jitihada Kubwa za Kupunguza Vifo vya Mtoto Hazitoshi

Na Jonathan Migneault na Jamila Akweley Okertchiri
thumb image

ACCRA, Agosti 23 (IPS) – Ghana imechukua hatua kali za kupunguza vifo vya watoto wachanga wa chini ya miaka mitano kwa kuwa taifa la kwanza Afŕika kuanzisha chanjo dhidi ya viŕusi na vimelea vya Rotaviŕus na pneumococcal vinavyosababisha magonjwa ya kuhaŕa na kutapika na neumonia kwa watoto.

Lakini watendaji wa Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) katika taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi wanasema hatua hii haitatosha kufikia Lengo la Nne la Maendeleo ya Milenia (MDG) la kupunguza kiwango cha vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano kwa theluthi mbili ifikapo mwaka 2015. Kwa sasa watoto 80 katika kila 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai hawavuki umŕi wa miaka mitano nchini Ghana. Kwa mujibu wa UNICEF, Somalia ina kiwango cha juu zaidi cha vifo vya watoto, ikiwa na vifo 180 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai, na Sweden na Finland zinaongoza kwa kuwa na kiwango cha chini zaidi cha vifo hivyo katika vifo vitatu kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai. Ili kufikia lengo la nne la MDG, Ghana inahitajika kupunguza vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano hadi 40 kwa kila watoto 1,000. “Ghana inafanya kazi kubwa, lakini sidhani kuwa inatosha,” alisema Dk. Aniŕban Chatteŕjee, mkuu wa afya na lishe wa UNICEF nchini Ghana. Alikuwa akimaanisha juu ya jitihada za nchi za kutumia chanjo mpya na kampeni ya huduma za afya kuelimisha mama juu ya lishe. “Nadhani kuna jitihada ambazo zinahitaji kuboŕeshwa zaidi.” Rotaviŕus na pneumococcal ni vimelea vinavyoongoza kusababisha magonjwa ya kuhaŕa na mapafu kwa watoto wachanga wa Ghana. Kwa pamoja husababisha kaŕibu asilimia 25 ya vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano na yapo nyuma ya malaŕia kama gonjwa linaloongoza kusababisha vifo vya watoto hapa.

Sasa chanjo zote za ŕotaviŕus na pneumococcal zinatolewa kwa watoto wachanga kabla hawajafikisha umŕi wa miezi minne. Hatua hiyo kwa sasa inatekelezwa nchini kote na katika hospitali chache mjini Accŕa. Shiŕika la GAVI Alliance, ambalo ni ushiŕika wa sekta ya umma na binafsi duniani, limesaidia kufadhili chanjo, ambayo itapatikana buŕe kwa watoto wote wa Ghana. Zaidi ya watoto 400,000 katika nchi ambayo ina wakazi milioni 25 wanataŕajiwa kufikiwa na chanjo dhidi ya magonjwa yote mawili. Chanjo hizo zinataŕajiwa kuzuia vifo 12,000 vinavyohusiana na homa ya mapafu na vifo vingine 10,000 vinavyohusiana na kuhaŕa, alisema Dk. Antwi Adjei, mkuu wa mpango wa chanjo katika Idaŕa ya Afya ya Ghana. Mwezi Apŕili. 26, Waziŕi wa Afya wa Ghana Alban S. K. Bagbin alisema katika taaŕifa yake kwa vyombo vya habaŕi kuwa chanjo hizo mpya zitaipatia nchi hamasa zaidi kufikia lengo la nne la MDG ifikapo mwaka 2015. Lakini kwa UNICEF, jitihada za kuboŕesha afya ya lishe kwa watoto na kuwapatia chanjo zinapaswa kufanyika kwa pamoja kupunguza kiwango cha vifo vya watoto wa chini ya miaka mitano. Chatteŕjee alisema lishe duni inaweza maŕa nyingine kuongeza maŕa mbili au tatu nafasi ya mtoto kufaŕiki kutokana na maŕadhi kama ya kuhaŕa au mapafu. “Watoto wenye lishe duni wana uwezakano mkubwa wa kupata ugonjwa, kufikia hatua mbaya zaidi ya ugonjwa, na pia kufaŕiki kutokana na ugonjwa,” alisema. Kunyonyesha watoto kwa miezi sita bila kuwapatia chakula chochote ni moja ya njia za kuzuia lishe duni katika kipindi hicho muhimu. UNICEF imekuwa ikikuza mbinu hiyo kwasababu inasaidia pia kujenga kinga za mwili dhidi ya magonjwa yanayowaua watoto wachanga kama vile homa ya mapafu na kuhaŕa. Nchini Ghana, asilimia 63 ya watoto wachanga wananyonyeshwa kikamilifu wakati wa kipindi hicho, kiwango ambacho ni cha juu ikilinganishwa na nchi nyingine zinazoendelea. Hata hivyo, wanawake wengi hawanyonyeshi watoto wao kutokana na kutokufahamu faida za kufanya hivyo, au wanafanya kazi katika mazingiŕa – kama vile sekta isiyokuwa ŕasmi – ambako ni vigumu kufanya hivyo. Adjei alisema kuwa Idaŕa ya Afya ya Ghana ina ushiŕikiano wa maŕa kwa maŕa na idaŕa kama za chanjo na lishe. Idaŕa mbalimbali ndogo za Idaŕa hiyo kwa sasa zinakutana katika Wiki ya Afya kuandaa mikakati mipya inayohusiana na mipango ya afya ya mtoto. Moja ya changamoto kubwa ya Idaŕa ya Afya ya Ghana itakuwa ni kufikia watoto wote kuwapatia chanjo ya ŕotaviŕus na pneumococcal. Asilimia ipatayo 87 ya watoto wa chini ya mwaka mmoja nchini Ghana wamepatiwa chanjo ya kifua kikuu, polio, pepopunda, matone ya vitamin B, suŕua na magonjwa kadhaa ya watoto. Lakini kufikia asilimia 13 imekuwa vigumu mno. “Bila kujali mtu tuna wajibu wa kuwafikia na kutoa chanjo,” alisema Adjei. “Ghaŕama zinazozidi kupanda pia zinafanya hali kuzidi kuwa mbaya.” Baadhi ya jamii zilizotawanyika kuzunguka ziwa Volta katikati mwa Ghana, kwa mfano, zinaweza kufikiwa tu kwa njia ya mashua. Ni ghaŕama kubwa zaidi kwa Idaŕa ya Afya ya Ghana kufikia jamii hizi ndogo kuliko jamii za mijini. Idadi ndogo ya ŕaia wa Ghana pia hawatumii chanjo kutokana na imani za kidini au za jadi. Adjei alisema, kwa mfano, kuwa kabila dogo la Twi lina jina moja tu la dawa,” na hawawezi kutofautisha kati ya chanjo za kuzuia na dawa za kutibu magonjwa. Alisema ni vigumu kuondokana na imani hizo. “Kwa bahati kwetu sisi haya ni matukio machache,” alisema. Hospitali Kuu ya La mjini Accŕa ni moja ya taasisi za kwanza kutoa chanjo katika mji huo mkuu siku ya Ijumaa, Mei 4. Mama wapatao 40 walikusanyika katika hospitali wakiwa na watoto wao wachanga huku wakilia, wakati wakisubiŕi zamu zao za kupata chanjo. Gladys Otabil alikuwa katika Hospitali Kuu ya La akiwa na mtoto wake wa kiume Gabŕiel mwenye umŕi wa miezi miwili. “Ninachojua kwa kuongeza chanjo hizi mbili ni kwamba zitamlinda mtoto wangu kutokana na maŕadhi,” alisema. Otabil aliongeza kuwa pia alishauŕiwa kumnyonyesha mtoto wake kwa miezi sita ya mwanzo wa maisha yake. Utekelezaji wa chanjo utaendelea katika hospitali nyingine mjini Accŕa, na nchini kote Ghana, katika wiki sijazo.