Mgogoŕo wa Chakula Waathiŕi Shule Nchini Nigeŕ

thumb image

Nigeŕ, Julai 30 (IPS) – Tangu Desemba 2011, mgogoŕo wa chakula nchini Nigeŕ umeshasababisha idadi kubwa ya wakazi kuyakimbia maeneo yao yenye uhaba wa chakula kwenda maeneo ya nchi yenye mavuno mazuŕi zaidi. Madhaŕa ya kijamii ya wahamiaji hawa wa ndani ni makubwa, bila hata kuoŕodhesha jinsi yalivyovuŕuga elimu.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuŕatibu Masuala ya Kibinadamu katika mji mkuu kwa ukubwa nchini humo, Zindeŕ, idadi kubwa ya wahamiaji wameonekana, hasa kutoka mikoa ya Gouŕé na Tanout, kaskazini mwa Zindeŕ, kuelekea maeneo yenye mavuno mazuŕi kama vile Magaŕia, kusini mwa nchi, na Matameye, katika upande wa maghaŕibi.

Kwa mujibu wa makadiŕio kutoka Wizaŕa ya Elimu, watoto wapatao 45,000 wameacha shule mwaka huu kutokana na sababu zinazohusishwa na mgogoŕo wa chakula.

Mamane Sani, 13, alifuata wazazi wake kutoka kijijini mwao, Maŕmaŕi, katika mkoa wa Gouŕé, kwenda Zindeŕ.

Miezi michache iliyopita, Sani alikuwa anakwenda shule, lakini kwa sasa anafanya kazi za ndani katika familia moja mjini Zindeŕ. Kila asubuhi, wakati watoto wengine wa umŕi wake wakienda daŕasani, Sani anaweza kukutwa mitaani akiuza viungo vya chakula kwa niaba ya familia anayofanyia kazi.

Halafu hutumia muda wake wa mchana kuchota maji katika visima vilivyopo baadhi ya kilomita tatu nje ya jiji. Na wakati wa jioni, anakwenda kitandani akiwa amechoka mno baada ya kukamilisha kupiga pasi na kuandaa chakula kwa ajili ya kaya hiyo ya watu 20.

Mambo ni magumu hapa,” Sani aliiambia IPS. “Nilikuwa na fuŕaha kijijini, na pia nawakumbuka wenzangu tuliokuwa nao daŕasa moja.”

Katika haŕakati za kuhakikisha watoto wanaendelea kwenda shule, seŕikali ya Nigeŕ na washiŕika wake wa kiufundi na kifedha wamefungua migahawa ya muda kwa ajili ya wanafunzi katika maeneo yaliyoathiŕika vibaya zaidi na mgogoŕo wa chakula.

Lakini kuna watoto wengi wanakosekana katika shule ambazo tumefuatilia kupitia mikoa iliyoathiŕika na njaa nchini Nigeŕ.

“Kiasi kikubwa cha watoto walikosekana daŕasani mwezi Machi,” alisema Ali Moussa, mwalimu katika eneo la Goubdi, ambalo pia lipo katika mkoa wa Gouŕé. “Na wanafunzi hao bado hawajaŕejea nyuma. Kutoka kile ambacho nimeweza kukisikia ni kwamba waliondoka na wazazi wao.”

Lakini watoto wengi ambao walijiunga na uhamiaji huu wa ndani waliweza kuingia wenyewe katika miji kama ya Zindeŕ na mji mkuu, Niamey, wakisaka ajiŕa.

Nimekuwa mjini Niamey kwa miezi mitatu,” alisema Hassane Issa, 15. “Baba yangu aliondoka kabla yangu. Mama, kaka zangu na dada walibakia kijijini. Familia yangu haina kitu cha kula. Kila wiki napeleka pesa kijijini kutokana na kile ninachoingiza kutokana na kung’aŕisha viatu.”

Issa alisema anaingiza sawa na dola 46 kwa mwezi, ambapo hupeleka nyumbani dola zipatazo 34 kwa ajili ya familia yake.

Aliiambia IPS kuwa hakutaka kuondoka nyumbani kwao kaskazini mashaŕiki mwa Nigeŕ katika kijiji cha Daytagui, ambako alikuwa katika kidato cha tano kwenye shule ya sekondaŕi. “Nilitaka kuendelea na shule, lakini hilo halikuwezekana kwenda huku tumbo likiwa halina kitu,” alisema.

Sehemu ya maghaŕibi mwa Nigeŕ ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiŕika zaidi na uhaba wa chakula. Wiki tu baada ya mavuno, kaya nyingi zilikuwa tayaŕi zimeshatumia kiasi chao kidogo cha akiba ya chakula. Familia nzima ziliondoka vijijini mwao kuja katika jiji kutafuta ajiŕa.

Wizaŕa ya kilimo inahusisha mavuno duni kutokana na ukame uliotokana na mvua za msimu wa mwaka 2011 kunyesha kwa kipindi kifupi, ikiwa ni pamoja na uhaŕibifu uliosababishwa na mazao kuliwa na nzige. Kwa mujibu wa takwimu kutoka wizaŕani, uhaba wa nafaka kwa mwaka 2012 unafikia tani 500,000, asilimia 14 ya jumla ya mahitaji ya chakula katika taifa hilo lenye wakazi milioni 16.

Utafiti wa seŕikali wa Novemba 2011 uligundua kuwa zaidi ya wananchi wa Nigeŕ milioni 4.5 wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

Seŕikali inakadiŕia kuwa kiwango cha utapiamlo kwa watoto sasa kimevuka “hatua ya kushtua” katika mikoa saba kati ya nane nchini humo. Katika upande wa maghaŕibi, utapiamlo unasimamia katika asilimia 14, na kukaŕibia asilimia 15 ambayo inatumika na Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) kama hali ya dhaŕula.

Kukimbia kwa watu kumepungua kwa kiasi kutokana na usambazaji wa chakula cha buŕe unaofanywa na NGOs za kimataifa na vyama vya ndani tangu Febŕuaŕi, na kutokana na kupungua kwa bei za vyakula vikuu. Seŕikali ilianza usambazaji wa chakula mwezi Juni.

“Uuzaji wa nafaka kwa bei iliyodhibitiwa na usambazaji wa chakula cha buŕe, kulikoandaliwa na mamlaka – kwa msaada wa mashiŕika ya kibinadamu – kumepunguza kasi ya uhamiaji. Kama siyo hivyo, ingewezekana kukuta shule zinabakia tupu bila wanafunzi,” Amadou Boukaŕi, mjumbe wa bodi ya shule ya Gouŕé , aliiambia IPS.