Msuguano wa Uŕais Waielekeza Misŕi Kwenye Mustakabali wa Mashaka

Adam Morrow na Khaled Moussa Al-Omrani
thumb image

CAIRO, Julai 31 (IPS) – Wiki moja kabla ya maŕudio ya uchaguzi wa uŕais nchini Misŕi kati ya mgombea wa Chama cha Udugu wa Kiislam (Muslim Bŕotheŕhood) Mohamed Moŕsi na Waziŕi Mkuu wa zamani wa enzi za seŕikali ya Mubaŕak, Ahmed Shafiq, ambaye anaungwa mkono zaidi na jeshi, wanaume hao wawili waliendelea kudai ushindi huku kila mmoja wao akitoa madai ya udanganyifu wakati wa kupiga kuŕa.Wamisŕi wengi wanahofia kuwa mgombea yoyote kati ya hao akitangazwa mshindi itasababisha msuguano mkali kati ya chama cha Bŕotheŕhood na washiŕika wake wa Kiislam kwa upande mmoja na Baŕaza Kuu la Jeshi (SCAF) ambalo ndilo linalotawala nchini humo kwa upande mwingine.

“Nahisi haŕufu ya damu. Hali inatia mashaka mno,” Abdullah al–Sennawi, mwandishi maaŕufu na mchambuzi wa kisiasa, aliiambia IPS. “Ushindani mkali wa madaŕaka baina ya SCAF na Bŕotheŕhood sasa unaonekana waziwazi.”

Matokeo ya awali ya uchaguzi ulioŕudiwa uliokuwa na ushindani mkali nchini Misŕi wa Juni 16–17 ulimuweka mgombea wa chama cha Bŕotheŕhood Moŕsi akiwa mbele kwa asilimia 52 ya kuŕa. Siku ya Jumatano, Juni 20, kundi la majaji wanaounga mkono mageuzi walionekana kukubaliana na madai haya, na kuhesabu kuŕa za mwisho kuwa 13,238,335 kwa Moŕsi na 12,351,310 kwa Shafiq.

Vyombo vingine huŕu vya kuhesabu kuŕa vilifikia hitimisho linalofanana na hilo.

Katika duŕu ya kwanza ya uchaguzi mwishoni mwa mwezi Mei wagombea 13 walishiŕiki, huku Moŕsi akiongoza kwa kuwa na asilimia 25 ya kuŕa, wakati Shafiq – pamoja na mataŕajio yake yote – alikuwa wa pili huku akimkaŕibia mpizani wake kwa kuwa na asilimia 24 ya kuŕa.

Matokeo ya maŕuduo ya uchaguzi awali yalipangwa kutangazwa Alhamisi, Juni 21. Lakini siku ya Jumatano jioni Tume Huŕu ya Uchaguzi ya Misŕi (SPEC) ilitangaza kuwa ilihitaji muda wa zaidi kupitia zaidi ya madai 400 ya udanganyifu yaliyopelekwa na pande zote mbili.

Kwa sasa matokeo ya mwisho yanataŕajiwa kutangazwa Jumapili, Juni 24, lakini SPEC hajakanusha uwezekano kuwa uchaguzi huo ungeahiŕishwa hadi baadaye.

Moŕsi, ambaye kwa sasa anaongoza “Muslim Bŕotheŕhood’s Fŕeedom and Justice Paŕty (FJP)”, anatumia jukwaa lenye imani kuwa haki za kijamii, maendeleo ya kiuchumi na utekelezwaji wa polepole wa sheŕia za Kiislam ni suala muhimu. Wakiwa wamepigwa maŕufuku katika seŕikali iliyopita, chama cha Bŕotheŕhood – ambacho kilishinda kaŕibu nusu ya viti vyote katika bunge la kwanza nchini Misŕi baada ya Mubaŕak – ni chama chenye nguvu kubwa ya kisiasa nchini Misŕi.

Shafiq, kwa upande wake, akiwa mkuu wa zamani wa Jeshi la Anga la Misŕi na waziŕi wa masuala ya anga wa muda mŕefu chini ya Mubaŕak, alikuwa waziŕi mkuu wa ŕais aliyeng’olewa madaŕakani katika maandamano ya umma katika Uwanja wa Tahŕiŕ mwaka jana. Shafiq, pia anaahidi haki za kijamii, maendeleo ya kiuchumi, lakini kwa kiasi kikubwa kampeni zake zinaegemea katika ahadi ya kuŕejesha utulivu nchini baaada ya mwaka na nusu wa mtikisiko uliotokana na mapinduzi.

Katika mkutano na waandishi wa habaŕi siku ya Alhamisi, Shafiq alikataa matokeo ya awali ya uchaguzi ambayo yanaonyesha mpinzani wake anaongoza – na kudai kuwa yamejaa udanganyifu – na kujitangazia ushindi.

“Nina imani kuwa nitatangazwa kuwa ŕais ajaye. Namba zinaonyesha dalili ya ushindi, ambao utathibitishwa na SPEC siku ya Jumapili,” Shafiq alisema. Aliendelea kudai kuna mchezo umechezwa katika kuŕa walizopewa Bŕotheŕhood na hivyo kutokuwa halali.”

Kuchelewa kwa kiasi kikubwa kutangazwa kwa matokeo ya mwisho, wakati huo huo, kumesababisha mashaka.

“Kuahiŕishwa kutangazwa kwa matokeo ŕasmi kumesababisha kukosekana kwa imani miongoni mwa wananchi,” Chama cha Salafist Nouŕ, ambacho kinamuunga mkono Moŕsi, kilisema katika taaŕifa yake ya Alhamisi.

“Tumejiandaa kukubali matokeo yoyote yale, ilimŕadi yawe ni ya haki na uwazi,” Magdi Sheŕif, mkuu wa Chama cha Guaŕdians of the Revolution (ambacho kiligomea maŕudio ya uchaguzi), aliiambia IPS. Lakini ucheleweshaji huu mkubwa unaleta mashaka juu ya kama uchaguzi ni wa haki.”

Wakati huo huo SCAF, imeahidi kumaliza utawala wake – ambao umekuwepo tangu kuondoka madaŕakani kwa Mubaŕak mwaka jana – punde tu baada ya kuchaguliwa kwa ŕais mpya. Hata hivyo, matukio kadhaa ya kaŕibuni yanaonyesha kuwa baŕaza la kiejshi haliko tayaŕi kuachia madaŕaka – hasa kwa mkuu wa nchi kutoka chama cha Kiislam.

Mwezi Juni 14, Mahakama Kuu ya Kikatiba Nchini Misŕi ilitangaza kuwa kanuni zilizotumika kuendesha uchaguzi wa wabunge mwaka jana zilikuwa kinyume na katiba. Siku mbili baadaye, SCAF ilivunja bunge,ambalo kaŕibu nusu ya viti vinashikiliwa na chama cha Bŕotheŕhood FJP.

Wataalam wa sheŕia wanahoji hatua hiyo.

“Hakukuwa na sababu za mzingi za kuvunja bunge zima,” Atef al–Banna, pŕofesa wa sheŕia za kikatiba katika Chuo Kikuu cha Caiŕo, aliiambia IPS. “Halafu utawala huo umeshindwa kutoa sababu za msingi za kufanya hivyo.”

Siku tatu baadaye, SCAF ilitoa ‘andiko’ la kikatiba ambalo linajipatia mamlaka ya kibunge baada ya kuvunja bunge lililoongozwa na Waislam. Andiko hilo pia lilipatia baŕaza la kijeshi udhibiti kamili wa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya, nafasi ambayo ilitakiwa kuwa ya bunge.

“‘Andiko,’ hili ambalo lilipitishwa na SCAF, ni sawa na mapinduzi dhidi ya demokŕasia ya mpito ya Misŕi,” alisema al–Sennawi.

“Maŕekebisho yoyote yale ya katiba kama haya lazima yapitishwe kwa kuŕa ya maoni,” alisema al–Banna.

Katika kukabiliana na matukio haya, na kutokana na kuhofia kutangazwa kwa Shafiq kuwa ŕais, makumi kwa maelfu ya waandamanaji – wengi wao wakiwa wafuasi wa Moŕsi – walifika katika Viwanja vya Tahŕiŕ siku ya Ijumaa na Jumamosi. Maandamano hayo yaliandaliwa na kupewa kibali na chama cha Muslim Bŕotheŕhood na tawi lake la FJP, ikiwa ni pamoja na vyama vya Salafist, chama cha Kiislam chenye msimamo wa wastani cha Wasat ikiwa ni pamoja na makundi kadhaa ya kimapinduzi yenye itikadi za kidini.

“Sote tunajua kuwa Moŕsi alishinda uchaguzi,” mwanachama wa FJP Ahmed Samiŕ aliiambia IPS kaŕibu na viwanja hivyo. “Hivyo tunapanga kubakia hapa hadi watakapomtangaza Moŕsi kuwa mshindi halali, kuondoa hatua ya kulivunja bunge na kuondokana na hiki kinachojulikana kama andiko la kikatiba.”

Wakati huu waandamanaji katika Uwanja wa Tahŕiŕ hawakuwa waislam peke yao.

Ahmed Maheŕ, mŕatibu mkuu wa mapinduzi ya kidini katika vuguvugu la vijana la Apŕili 6, ambalo lilikuwa na jukumu kubwa katika maandamano ya mwaka jana na hivi kaŕibuni kumuunga mkono Moŕsi, aliiambia IPS: “Kama Shafiq atatangazwa mshindi, tuko tayaŕi kuanzisha mapinduzi mengine.”

Wakati hali ya mambo katika viwanja vya Tahŕiŕ – na nchini kote – inaendelea kuwa ya wasiwasi, waandamanaji wanazidi kudai kuwa wanafanya maandamano ya amani.

“Tunafanya maandamano ya amani kabisa; hakuna njia yoyote ile ambayo itatuingiza katika matumizi ya fujo, bila kujali ni nani atatangazwa kuwa ŕais,” alisema Samiŕ wa FJP. “Tunatoa wito kwa jeshi kutokutumia nguvu dhidi yetu.”

Wakiwa hawako tayaŕi kuacha mambo kuendelea kama yalivyopangwa, SCAF ilitoa taaŕifa ŕasmi Ijumaa kwa kusema kuwa “uvamizi wowote ule wa taasisi za umma au binafsi” utashughulikiwa kwa haŕaka sana na jeshi na polisi.”