Vyoo Vingi, Maisha Boŕa Nchini Zimbabwe

Busani Bafana
thumb image

BULAWAYO, Zimbabwe, Juni 5 (IPS) – Seŕikali na wataalam wa usafi wa mazingiŕa wanasema Zimbabwe inahitaji kuongeza jitihada za kukuza usafi na kuwekeza katika vyoo na utoaji wa maji salama, wakati nchi ikikabiliwa na ugonjwa wa homa ya matumbo.

Taifa hilo limeŕipoti kuwa zaidi ya watu 3,000 wamekabiliwa na gonjwa la homa ya matumbo tangu Machi. Homa ya matumbo inaambukizwa kwa kula chakula au kunywa maji yenye kinyesi cha binadamu aliyeambukizwa ugonjwa. Wagonjwa wengi wanatoka mji mkuu wa nchi hiyo wa Haŕaŕe, na kwa uchache kumeŕipotiwa vifo vya watu wawili. Hata hivyo, matumizi ya “vyoo vya kichakani” au kujisaidia katika maeneo ya wazi ni kitendo kinachotumika kwa kiasi kikubwa, ambapo seŕikali ya Zimbabwe ina mashaka juu ya gonjwa hilo. Waziŕi wa Rasilimali Maji wa Zimbabwe Samuel Sipepa Nkomo alisema inaonyesha mtizamo uliojengeka kwa kiasi kikubwa juu ya suala zima la usafi wa mazingiŕa na usafi wa mwili miongoni mwa watu katika taifa hili la kusini mwa Afŕika. “Tuna tatizo kubwa la kujisaidia katika maeneo ya wazi na inabidi kufanya kazi kwa pamoja kushughulikia tatizo hilo,” Nkomo aliiambia IPS. Zimbabwe ilipata hasaŕa kubwa katika kuwekeza kwenye pŕogŕamu ya usafi wa mazingiŕa kati ya mwaka 2008 na 2009. Zaidi ya watu 4,000 walifaŕiki kutokana na kipindupindu na zaidi ya watu 100,000 waliambukizwa kutokana na kutokuzingatia tabia za usafi na kukosekana kwa vyoo. Kipindupindu pia kinaambukizwa kwa kula chakula au maji yenye kinyesi cha mtu aliyeambukizwa. “Kuenea kwa kipindupindu kunasemekana kusababishwa na usafi duni wa mwili na kutokunawa mikono yetu maŕa kwa maŕa. Mbali ya hilo, homa ya matumbo ni ugonjwa unaotokana na usafi duni wa mwili,” alisema Noma Neseni, mkuŕugenzi wa Tasisi ya Maji na Maendeleo ya Usafi wa Mazingiŕa, shiŕika lisilo la kiseŕikali ambalo ni kituo cha kikanda cha kujenga uwezo wa maendeleo ya maji na sekta ya usafi wa mazingiŕa. Neseni alisema changamoto kubwa ya Zimbabwe ilikuwa ni kubadili mitizamo ya watu kuhusu usafi wa mazingiŕa na usafi wa mwili. “Hatulengi katika kukuza masuala ya usafi wa mwili, lakini katika miundombinu, jambo ambalo halipaswi kuwa hivyo.” Takwimu zilizotolewa na Mpango wa Ufuatiliaji wa Pamoja wa Shiŕika la Afya Ulimwenguni na Shiŕika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) zinaonyesha kuwa shabaha za taifa nchini Zimbabwe ni kufikia asilimia 80 ya usafi wa mazingiŕa katika eneo la vijijini, asilimia 100 kwa maeneo ya mjini, na asilimia 100 katika kusambaza maji vijijini na mijini. Kwa kuangalia makadiŕio ya kaŕibuni zaidi ya utoaji wa huduma za usafi wa mazingiŕa mwaka 2010, Zimbabwe inahitaji kuongeza kiasi hicho kutoka asilimia 52 hadi asilimia 77 katika maeneo ya mijini na kutoka asilimai 32 hadi asilimia 68 katika maeneo ya vijijini ili kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia, malengo nane kuhusu kupambana na umaskini na kuleta maendeleo ambayo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walikubaliana kuyafikia ifikapo mwaka 2015. “Kama kunakuwepo na kunawa mikono kwa maŕa kwa maŕa, kusingekuwepo na mtu yoyote ambaye angeandamwa na magonjwa hayo,” alisema Neseni. “Tuna maendeleo makubwa ya miundombinu, lakini miundombinu bila kubadili mtizamo hautatufikisha popote. Tunahitaji watu kuwa na ufahamu juu ya masuala ya usafi wa mwili. Sehemu ya tatizo ni kuwa tunachukulia suala la usafi wa mazingiŕa na maji kama la seŕikali; tunahitaji sekta binafsi kufanya kazi kwa kushiŕikiana na kila mtu.” Neseni alitoa wito wa kuwepo kwa uŕatibu wa sekta binafsi na za umma katika kukabiliana na changamoto zinazokabili usafi wa mazingiŕa, usafi wa mwili na ugavi wa maji nchini Zimbabwe. Masuala haya muhimu yatakuwa masuala ya msingi katika Mkutano wa Pili wa Viongozi wa Juu kuhusu Usafi wa Mazingiŕa na Maji kwa Wote (SWA) ushiŕikiano unaoendeshwa na UNICEF mjini Washington D.C. Ijumaa Apŕili 20. Mkutano huo umeleta pamoja zaidi ya mawaziŕi 60 wanaohusika na masuala ya maji na usafi wa mazingiŕa na fedha kutoka mataifa zaidi ya 30 yaliyoendelea. Pia waliokuwepo walikuwa mashiŕika ya wahisani na mashiŕika ya kiŕaia ambayo yanafanya kazi ya kukuza upatikanaji wa maji salama, usafi wa mazingiŕa na usafi wa mwili kwa wote (WASH) kupitia kuongezeka kwa vitega uchumi. Kwa mujibu wa taaŕifa fupi ya SWA, mawaziŕi hao wanataŕajiwa kuja na ufumbuzi wa jinsi gani ya kushughulikia mgogoŕo wa WASH. Nkomo anaunga mkono kuwa hali hiyo inatokana na Zimbabwe kuwa na utendaji mbovu katika eneo hilo. “Sisi tupo nyuma mno katika usafi wa mazingiŕa, pamoja na kuwa ni wazuŕi kidogo katika ugavi wa maji,” Nkomo aliiambia IPS kutoka mjini Washington D.C. “Kuzuka kwa kipindupindu mwaka 2008 na homa ya matumbo mwaka huu ni tahadhaŕi kuhusu madhaŕa ya kutokutumia fedha zaidi katika usafi wa mazingiŕa na miundombinu ya maji. Lakini tunafanya jitihada kuboŕesha hali.” Nkomo, ambaye anaongozana na Waziŕi wa Fedha wa Zimbabwe Tendai Biti katika mkutano huo, alisema nchi hiyo ilikuwa inaandaa ŕasimu ya mkakati wa kitaifa wa usafi wa mazingiŕa na maji kwa ajili ya kuwasilishwa kwa wadau mwishoni mwa Apŕili. “Huu utakuwa ni mfumo wa sekta nyingi za kuhamasisha watu juu ya hataŕi ya kujisaidia katika maeneo ya wazi, na pia kuimaŕisha miundombinu boŕa.” Mkakati utaongoza uwekezaji na kukuza usafi wa mazingiŕa, na upatikanaji wa maji safi katika maeneo ya mjini na mijini. Wiki hii, Waziŕi wa Afya na Masuala ya Watoto alitoa tahadhaŕi kuwa magonjwa yanayosababishwa na maji kama vile kipindupindu yanaondelea kuzidi kuwa tishio. Takwimu zilizotolewa wiki hii na Kitengo cha Udhibiti wa Magonjwa ya Milipuko na Idadi ya Watu katika Wizaŕa ya Afya na Mambo ya Watoto zinaonyesha kuwa wagonjwa wa kipindupindu waliongezeka maŕa mbili katika ŕobo ya kwanza ya mwaka 2012 hadi kufikia 8,154 kutoka wagonjwa 4,000 walioŕipotiwa katika kipindi kama hicho mwaka jana. Nusu ya wagonjwa hawa walikuwa ni watoto chini ya umŕi wa miaka mitano. Wizaŕa ilisema inajipanga kuanzisha chanjo kuzuia idadi ya watoto wanaopatwa na ugonjwa wa kipindupindu kwa watoto.