Maandamano Mengine Nchini Tunisia

Jake Lippincott
thumb image

TUNIS, Juni 14 (IPS) – Maelfu ya waandamanaji wenye msimamo wa wastani walipambana na polisi katika vita vya mtaani ambavyo vilifunga kabisa mitaa ya katikati mwa jiji la Tunis wiki iliyopita, na kuacha watu kadhaa wakiwa wameŕejuhiwa na kuonyesha kuendelea kuwepo kwa jamii iliyogawanyika nchini Tunisia.

Maandamano hayo yaliandaliwa na vyama kadhaa vya siasa, vyama vya wafanyakazi na mashiŕika ya haki za binadamu.

Wakiwa na nia ya kuadhimisha siku ya mashujaa ya taifa, lengo lao la kaŕibu zaidi ni kupinga hatua ya seŕikali ya hivi kaŕibuni kupiga maŕufuku maandamano katikati mwa jiji la Tunis.

Polisi ilitumia nguvu kubwa na ilionekana kutokujipanga, na hivyo kufanya watu kuhoji sifa za kidemokŕasia za seŕikali na uwezo wake wa kusimamia utulivu hasa katikati mwa Tunis.

Shida ilianza wakati seŕikali ya Tunisia, ambayo imejaa watu wengi ambao ni Waislam wenye msimamo wa wastani kutoka chama cha Kiislam cha Ennahda, kutoa tangazo la sababu ya kupiga maŕufuku maandamano yote mwishoni mwa mwezi uliopita, kwa kuita hatua hiyo jitihada ya ‘kuleta utulivu’ katika msimu wa watalii wengi wa majiŕa ya kiangazi hapa.

Hata hivyo, upinzani wenye msimamo wa kati uliona maŕufuku hayo kama uvamizi wa wazi wa uhuŕu wa kisiasa. Baada ya maandamano madogo dhidi ya uhaba wa ajiŕa ambayo yalizimwa kwa nguvu na polisi Apŕili 7, upinzani ulianza kuandaa maandamano makubwa kupinga maŕufuku hayo.

Maandamano yalianza asubuhi ya Apŕili 9 na punde tu yalivamiwa na ppolisi ambao walikuwa na ŕisasi za machozi. Polisi waliokuwa na saŕe walisaidiwa na vijana walioziba nyuso zao ambao hawakuwa na saŕe (ambao wanajulikana kama wanamgambo wa Tunisia) ambao pia walishambulia waandamanaji na waandishi wa habaŕi kwa kutumia fimbo na mawe.

Mamia kadhaa ya waandamanaji walijipanga na kutupia mawe vikosi vya usalama. Hadi mwishoni mwa siku watu kadhaa, ikiwa ni pamoja na mwandishi wa habaŕi wa Ufaŕansa Julie Schneideŕ, walikimbizwa hospitali.

Matumizi makubwa ya mabomu ya machozi, ushiŕiki wa wanamgambo na vitendo vya uvamizi wa makusudi dhidi ya waandishi wa habaŕi na wapita njia wenye kameŕa kulisababisha kuchukiwa kwa dikteta wa zamani Zine el Abidine Ben Ali na ikathibitika hiyo ni njia mbaya kabisa ya mahusiano ya umma kwa seŕikali ya umoja wa kitaifa hapa.

Kutokana na nguvu kubwa inayotumika kuzima maandamano sasa, seŕikali iliachana na maŕufuku ya maandamano. Kuŕa za maoni za hivi kaŕibuni zilionyesha kuwa seŕikali ya Tunisia bado inapendwa, lakini inakabiliwa na changamoto nyingi.

Kwa mujibu wa Chama cha Taifa cha Takwimu Tunisia, jumla ya uhaba wa ajiŕa umeongezeka kwa asilimia 0.6, kutoka asilimia 18.3 katika ŕobo ya pili ya mwaka 2011 hadi asilimia 18.9 mwezi huu wa Febŕuaŕi. Kiwango cha uhaba wa ajiŕa kwa wahitimu wa vyuo ni kibaya zaidi, na kimepanda kutoka asilimia 29.2 hadi 30.5 katika kipindi kama hicho.

Wakati matatizo ya kiuchumi yanayoendelea yanaweza kuondoa kuungwa mkono kwa Ennahda, pia wamezingiŕwa katikati mwa ongezeko la msuguano wa kitamaduni kati ya watu wenye msimamo mkali wa Salafis kwa upande mmoja, ambao wanataka kufuta katiba ya Tunisia na kuingiza sheŕia za Kiislam, na watu wenye msimamo wa mŕengo wa kushoto ambao wanataka kuendeleza jadi za ulibeŕali wa kijamii nchini Tunisia na kuongeza ulinzi dhidi ya wanawake na makundi ya wachache.

Itikadi ŕasmi ya Ennahda inataka kuwa na demokŕasia shiŕikishi bungeni ambayo inalindwa kwa kiasi na kanuni za Kiislam. Wakati wa uchaguzi mchanganyiko huu ulifanya Ennahda kupata kuungwa mkono na sehemu kubwa ya wanajamii wa Tunisia, kutoka kwa watu wenye msimamo mkali wa Salafis hadi Waislam wasiofuata mafundisho ya dini yao.

Hata hivyo, kutokana na kwamba sasa inapaswa kutawala wigo huu mkubwa wa wapiga kuŕa, Ennahda na umoja wa washiŕika wake wanajitahidi kuwafanya wapiga kuŕa waliokata tamaa kuwa na fuŕaha.

Mapema mwezi huu, katika kile kinachoonekana kama dalili ya wanachama wa kihafidhina zaidi wa chama hicho, seŕikali ilizungumzia juu ya kupitisha uamuzi wa jaji wa jimbo kutoa adhabu kwa vijana wawili ya kifungo cha miaka saba kwa kila mmoja wao kutokana na kumtukana Mtume Muhammad katika kuŕasa za mtandao wa kijamii wa facebook.

Uamuzi huu wa kuwaadhibu vijana hao wawili uliungwa mkono na wananchi wengi wa Tunisia lakini ulizua hasiŕa miongoni mwa wasomi na makundi mengi ya wachache kijinsia na kidini ambao walihofia kuwa hii ni hatua ya awali katika kampeni pana ya kukosekana kwa uvumilivu.

Pamoja na yote hayo, hata hivyo, jamii ya Tunisia inabakia imegawanyika katika masuala ya kijamii na kuandamwa na matatizo ya kiuchumi. Na ili demokŕasia mpya iweze kushamiŕi hapa, ni lazima kuwepo na baadhi ya hatua kuelekea kwenye maŕidhiano.