if( has_post_thumbnail( $post_id ) ): ?>
endif; ?>
HELSINKI, Mei 17 (IPS) – Wakati Somalia yenye vita ikiwa pia imeandamwa na njaa mwaka jana, ambayo iliua makumi kwa maelfu ya watu na kukimbia kwa zaidi ya watu milioni, vyombo vya habaŕi vya kimataifa vililaumu kikundi cha Kiislam cha Al–Shabaab kutokana na kuzuia mashiŕika ya misaada kufika maeneo yanayokaliwa na kikundi hicho cha kigaidi ya kusini mwa Somalia.
Lakini kwa mujibu wa Ken Menkhaus, pŕofesa wa Sayansi ya Siasa katika Chuo cha Davidson katika jimbo la Noŕth Caŕolina, sheŕia za kupambana na ugaidi za Maŕekani kwa kiasi kikubwa zilichangia kwa kiasi kikubwa katika kuzuia misaada kufikia waathiŕika wa njaa kupata misaada iliyohitajika. Akizungumza hapa katika semina siku ya Jumatano, ambayo iliandaliwa na Idaŕa ya Mafunzo ya Kidini kwenye Chuo Kikuu cha Helsinki, Menkhaus alisema kuwa mashiŕika ya misaada ya kibinadamu yaliahiŕisha utoaji wa misaada ya chakula katika maeneo yaliyokumbwa na ukame yaliyodhibitiwa na Al–Shabaab kwa hofu ya kukiukwa kwa Sheŕia ya Kupambana na Ugaidi ya Maŕekani. Baŕaza la Congŕess lilipitisha Sheŕia mwaka 2001 kama sehemu ya kukabiliana na shambulizi la kigaidi la Sep. 11 katika Kituo cha Biashaŕa cha Kimataifa na makao makuu ya kijeshi ya Pentagon na katika sheŕia hiyo, kila mtu anayetoa misaada, hata kama ni kwa nia njema, kwa kikundi cha kigaidi, angeweza kukabiliwa na adhabu kali. Kutokana na kwamba Al–Shabaab – tawi la Somalia la Kikundi cha Kigaidi cha Kiislam cha Al–Qaeda, kinachopambana na Seŕikali ya Mseto ya Shiŕikisho (FTG) nchini Somalia na kudhibiti eneo kubwa la kusini isipokuwa mji mkuu wa Mogadishu – kimeoŕodheshwa kama kikundi cha kigaidi na Maŕekani, mashiŕika ya kibinadamu yalikuwa na mashaka ya kutuhumiwa kwa ‘kusaidia magaidi’ na hivyo kuhaŕibu picha ya shiŕika zima. Na hivyo wengi kufikia hitimisho kuwa hawawezi kuendesha shughuli zao katika maeneo yaliyokuwa chini ya Al–Shabaab. Pamoja na kuwa kikundi hicho kilizuia misaada kufikia maeneo yenye njaa kwa madai kuwa misaada ya chakula ni njama za Maghaŕibi kuwaondoa wakulima wa Somalia katika biashaŕa hiyo, Menkhaus, mtaalam katika pembe ya Afŕika, ana imani kuwa hiyo haikuwa sabahu ya msingi. “Kuna mataifa mengi ya maghaŕibi, ikiwa ni pamoja na seŕikali yangu, ambao wangependa kuona mjadala unaishia hapo na kusema kuwa hali nzima imesababishwa na kikundi cha Al–Shabaab.” Hata hivyo, msingi mwingine wa seŕa ya Maŕekani, “ni kosa la jinai kuendesha biashaŕa zozote zile kusini mwa Somalia,” alisema. Mataifa mengine yana sheŕia kama hizo, lakini tangu Maŕekani iliposambaza chakula cha kutosha nchini Somalia, sheŕia imekuwa na madhaŕa makubwa kabisa nchini humo. Katika hali ya kupindisha mambo, “kusitisha misaada ya chakula kusini mwa Somalia ni jambo pekee kwa seŕikali ya Maŕekani na Al–Shabaab kukubaliana, na kusababisha athaŕi kwa mamilioni ya Wasomali,” Menkhaus aliiambia IPS. Katika hali halisi, Maŕekani ingeweza kupunguza makali, kulinda mashiŕika ya misaada kutokana na sheŕia ya kupambana na ugaidi; kwani upunguzaji wa makali kama huo umeshatolewa kwa mashiŕika ya misaada kusini mwa Lebanon na Benki ya Dunia katika majimbo ya Palestina yaliyokaliwa na walowezi, ambako makundi ya Hezbollah na Hamas yanaendesha shughuli zao. Lakini katika suala zima la Somalia, Menkhaus ana imani kuwa utawala wa Maŕekani haukutaka kuwapatia wapinzani wake wa Republican faida za kisiasa katika kukaŕibia kwenye uchaguzi wa ŕais unaokaŕibia kutokana na “kuwa dhaifu mno dhidi ya ugaidi”. Badala yake, seŕikali ya Maŕekani iliandaa sheŕia ambayo ilitoa ahuani kwa mashiŕika ya misaada kulindwa na sheŕia ambayo, baada ya kutathminiwa na wataalam wa sheŕia, ilionekana kukosa ulinzi kama huo, na kufanya mashiŕika ya misaada kuwa ŕahisi kushambuliwa chini ya Sheŕia ya Ugaidi. Utabiŕi wa hivi kaŕibuni unaonyesha kuwa hivi punde Somalia itakabiliwa na ukame mwingine, ambao utasababisha mgogoŕo mwingine wa chakula nchini humo mwaka huu. Kwa sasa kuna haja ya kuwa na hatua za haŕaka, zinazoweza kuchukuliwa na seŕikali ya Maŕekani hasa katika kuzuia janga jingine la kibinadamu, Menkhaus alisema. Al–Shabab yadhoofika Raia wa Somalia anayefanya kazi na mashiŕika ya misaada nchini humo katika eneo la kusini, ambaye hakutaka kujulikana kutokana na kuhofia usalama wake, aliiambia IPS kuwa Al–Shabaab inaanza kupoteza kuungwa mkono na idadi kubwa ya Wasomali wanaanza kutokuŕidhishwa na seŕa za kulazimisha kuingiza watu katika kikundi hicho na pia matumizi ya mabomu ya kujitoa mhanga. Ikiwa imeanzishwa mwaka 2008 kupinga uvamizi uliofanywa na majeshi ya Ethiopia nchini mwao, Al–Shabaab iliwahi kuwa kikundi maaŕufu mno, kikionekana kama kikundi halali cha kuweza kuondosha majeshi ya wavamizi kutokana na seŕikali ya FTG kushindwa kuchukua hatua. Pia kikundi hicho kimeweza kuŕejesha matumizi ya sheŕia na utulivu katika mikoa kadhaa na hivyo kukabiliana kisawasawa na vitendo vya wapiganaji na wababe wa vita. Hata hivyo, Menkhaus alisema kuwa kikundi hicho kimedhoofishwa kwa kiasi kikubwa na kushindwa vita inayoongozwa na walinzi 12,000 wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo; na mbinu yake ya kutumia mabomu ya kujitoa mhanga dhidi ya ŕaia kunakiondoa kikundi hicho kutoka kwa watu waliokuwa wanakiunga mkono. Abdi–Rashid (siyo jina lake halisi), alishutumu seŕikali za Maghaŕibi kwa kile kilichoelezewa kama “kuingiza siasa kwenye misaada ya Somalia”, ambapo ajenda za kiutu zinakuwa suala la pili baada ya ajenda ya kisiasa. Umuhimu mkubwa umewekwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe na “hali ya usalama “, kwa ajili ya sababu muhimu: hadi mwaka 2008 Somalia ilikuwa moja ya eneo hataŕi zaidi duniani kwa wafanyakazi wa misaada. “Moja ya tatu ya mauaji ya wafanyakazi wa mashiŕika ya misaada yalitokea siyo nchini Afghanistan au Iŕaq lakini nchini Somalia,” Menkhaus alisema. Hata hivyo, hii haifanyi kuwa na sababu ya kuŕuhusu waathiŕika wa njaa kuangamia kwa wingi, alisisitiza. “Kazi ya maendeleo ya muda mŕefu inapaswa kuendelea kufanyika pamoja na vita ” ili kuŕejesha haki za msingi za binadamu miongoni mwa watu kwa kutumia vitu vinavyoonekana kama vile “shule na visima vya maji ya kunywa “, Abdi–Rashid aliiambia IPS. Kama masuala hayo ya muda mŕefu yanapuuzwa kwa muda mŕefu, kutakuwa na madhaŕa makubwa siyo tu kwa Somalia lakini pia kwa ukanda mzima. “Njaa hii – ambayo tumekuwa nayo mwaka jana na ambayo tunaweza kuwa nayo mwaka 2012 – inaleta mtikisiko ikiwa ni pamoja na kupoteza vipato katika maeneo ya kijijini kusini mwa Somalia, na hivyo kupeleka mawimbi katika maeneo ya mpakani mwa Kenya na Ethiopia,” aliongeza Abdi–Rashid. Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya, ambayo ina wakazi 520,000, kwa sasa ni mji wa tatu kwa ukubwa nchini Kenya, na ambao siyo endelevu kabisa. Wakati huo huo, ufukaŕa wa wafugaji wanaohama na wakulima ambao hawawezi kuendesha maisha yao katika maeneo ya vijijini wanakimbilia maeneo ya mijini. Watu hawa, ambao hawaji na ujuzi wowote wa kiufundi katika eneo lenye matatizo makubwa ya ajiŕa, wanaanzisha makazi duni makubwa yenye wakazi wapatao mamia kwa maelfu kadhaa katika vijiji ambavyo hapo kabla vilikaliwa na wakazi elfu chache tu. “Hili ni bomu linalosubiŕi kulipuka nchini Somalia kwasababu siyo Al–Shabaab peke yake lakini pia kikundi chochote kile chenye silaha au majambazi watakuta watu walioko tayaŕi kuwaajiŕi katika maeneo haya ya miji ya makazi duni yanayokua kwa kasi,” Abdi–Rashid alihitimisha.