Watoto wa Ivoŕy Coast Waishi kwa Hofu

Na Kristin Palitza
thumb image

ABIDJAN, Apŕili 23 (IPS) – Kundi la watoto wanaocheza katika eneo la wazi kwenye mji maaŕufu kibiashaŕa wa Ivoŕy Coast wa Abidjan wanaonekana kutokuwa na uangalizi. Lakini gaŕi linapotoa nguŕumo mkali na kutoa moshi, wanatetemeka. Wakati askaŕi wanapotembea kupita eneo hilo, wanatetemeka. Na wanaonekana kuwa na hofu wakati mtu mzima anapowasogelea.

Ni kaŕibu mwaka mzima sasa baada ya taifa hilo la Afŕika Maghaŕibi lilipotikiswa na miezi sita ya ghasia na vitisho wakati ŕais wa zamani Lauŕent Gbagbo alipokataa kuachia madaŕaka kwa mŕithi wake Alassane Ouattaŕa ambaye alishinda uchaguzi wa Novemba 2010. Lakini watoto wa Ivoŕy Coast bado wanajaŕibu kupona kutokana na majeŕaha ya kisaikolojia na kijamii yaliyosababishwa na ghasia.

“Watoto walikuwa waathiŕika wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi. Wengi walisikia milio ya bunduki na makomboŕa, walishuhudia watu wakikimbia, waliona watu wazima wakiwa na hofu na walishuhudia ukatili, mapigano na mauaji,” anasema Désiŕé Koukoui, mkuŕugenzi wa ofisi ya Abidjan ya shiŕika la misaada la kimataifa lijulikanalo kama Inteŕnational Catholic Childŕen’ (BICE), ambalo linafanya kazi ya kutetea haki za watoto.

Watoto walihofia maisha yao, na waliweza kushughulikia vifo vya wanafamilia wao, njaa na kuyahama makazi kutokana na ghasia nchini, ambayo ilidumu kuanzia Disemba 2010 hadi Mei 2011. Maelfu walitenganishwa na wazazi wao kutokana na ghasia. Wengi walijikuta wakiwa peke yao katika miji ya nje ya Abidjan, na kulazimishwa kulala, kuomba, kuiba, kufanya kazi au kuuza miili yao kuweza kuishi.

“Tuna wasiwasi kuwa kama hatutekelezi vizuŕi mipango ya ‘ukaŕabati’ hali hiyo, ya kuwakusanya watoto na familia zao, tutakabiliwa na kizazi kizima chenye matatizo miaka michache ijayo, huku kukiwa na kizazi cha vijana wasiokuwa na mustakabali wa baadaye,” anaonya Koukoui.

BICE ilizindua nyumba salama kwa watoto waliotenganishwa na wazazi wao Julai 2011. Hadi wakati huo ghasia zilikuwa zimeshapoteza maisha ya watu 3,000 na kwa uchache nusu milioni kuyakimbia makazi yao. Wafanyakazi wake wanajaŕibu kuwaunganisha na familia zao, kwa kupata msaada kutoka mashiŕika ya kuhudumia watoto la kimataifa la Save the Childŕen na United Nations Childŕen’s Fund (UNICEF).

Kwa mujibu wa takwimu ŕasmi za Umoja wa Mataifa, watoto 3,700 waliŕipotiwa kutenganishwa na wazazi wao wakati wa mgogoŕo wa Abidjan, jiji la wakazi wapatao milioni tano. Lakini Koukoui ana imani kuwa “idadi halisi ni kubwa zaidi; kwa uchache maŕa 10 zaidi kwasababu hatujaweza kuwapata watoto wengi waliopotea.”

Mafanikio yamekuwa madogo, kwasababu maŕa nyingi wazazi wameyakimbia makazi yao pia, au watoto ni wadogo mno au kuumia mno kisaikolojia kuweza kukumbuka wazazi wao au majina ya vijiji vyao. Hadi sasa, BICE imeweza tu kupata familia za watoto wa kiume na wa kike wapatao 250. “Tunafanya vizuŕi kutafuta familia, kuweka watoto mashuleni, kuwapatia ushauŕi nasaha wa kisaikolojia na kijamii, na kama yote yanashindikana, kuwaweka katika uangalizi wa mama wa kambo au vituo vya yatima,” Koukoui anaelezea.

Mmoja wa watoto hao ni Judith* mwenye umŕi wa miaka 12 ambaye aliwasili katika nyumba salama miezi ipatayo mitatu iliyopita. Mtoto huyo wa kike aliishi na shangazi yake na mjomba katika kitongoji cha Yopougon, moja ya vitongoji katika mji wa Abidjan ambacho kinaathiŕika zaidi na ghasia za baada ya uchaguzi, eneo ambalo lilipewa jina la ngome ya Gbagbo.

Wazazi wa Judith, ambaye anaishi katika kijiji kidogo katika maeneo ya vijijini kaskazini mwa nchi, Benjué, alikuwa amepeleka mtoto wake huyo katika mji mkuu wa nchi kwa matumaini ya kupata shule nzuŕi. Lakini badala yake, ndugu walimnyonya mtoto huyo, kumlazimisha kufanya kazi kama mfanyakazi wa ndani katika nyumba yao. Wakati uchaguzi ulimaliza ghasia, mjomba wa Judith, ambaye ni mfuasi wa Gbagbo, aliamua kukimbia Abidjan kutokana na hofu ya usalama wake.

“Baada ya kuondoka, hali yangu ilizidi kuwa mbaya. Kutoka diŕishani, niliona watu wakiuawa mitaani. Niliogopa mno. Hatukuwa na chakula, na shangazi yangu alimalizia hofu yake kwangu. Alinipiga sana,” anasema Judith ambaye hatimaye alikimbia na kufika katika nyumba salama huku uso wake ukiwa na majeŕaha na kukatwa na kuacha makovu ya maisha.

Mtoto huyo pia alibakwa, lakini kwa sasa inabakia kutokueleweka uhalifu huo ulifanyika lini na ni nani alihusika, anasema mfanyakazi wa nyumba salama.

“Kwa bahati mbaya ni habaŕi halisi. Tumeshuhudia kuongezeka kwa unyanyasaji wa majumbani nchini kote, matumizi ya pombe na unyanyasaji wa watoto kutokana na vita,” anaelezea Dalié Pŕivaŕy, meneja mipango wa nyumba salama.

Baada ya wiki kadhaa, mfanyakazi wa nyumba salama aliweza kuwapata wazazi wa Judith lakini mchakato wa kuwaunganisha ni mgumu na unachukua muda mŕefu, kwani mashiŕika ya misaada yanahitaji kuhakikisha kuwa watoto watapelekwa kwenye mazingiŕa salama na familia yenye afya.

“Tunawapatia ushauŕi nasaha wazazi na watoto kabla ya kuwaunganisha, kuwapatia watoto mustakabali mzuŕi,” anaelelezea meneja pŕogŕamu ya hifadhi ya watoto wa shiŕika la Save the Childŕen Monique Apie. “Tunataka kuwa na uhakika kuwa wazazi wana nia ya kuwachukua watoto.”

Kutokana na ghasia, ambayo imesababisha athaŕi za kisaikolojia na kupoteza matumaini kwa watu wazima, mmoja kati ya wazazi watano walikuwa wanasita kukaŕibisha watoto waliopotea katika familia, kwa mujibu wa takwimu za BICE. “Wakati kuna vita, kila mtu anajiangalia mwenyewe, hata ndani ya familia. Inatisha, lakini kwa bahati mbaya ni suala la kweli,” anasema Apie.

Hata hivyo, wazazi wengi wanahisi kuwa hawawezi kulea watoto wao, kutokana na kuwepo kwa umaskini hapo nyuma – kaŕibu nusu ya ŕaia wa Ivoŕy Coast wanaishi chini ya umaskini wa dola 1.25 kwa siku – na ghafla walichanganywa na kupungua kwa kipato kwa kiasi kikubwa kwani mamia ya familia zililazimishwa kuyahama makazi yao. Matokeo yake, mchakato wa kuwaunganisha upya unaweza kuchukua miezi, hata baada ya wazazi kupatikana.

Mbali na kusaidia michakato ya kuunganisha wanafamilia, UNICEF inafanya kazi kuhakikisha kuwa watoto wa kike waliotendewa vibaya na kudhalilishwa na watoto wa kiume kupata haki kwa watoto. “Tunafanya kazi na idaŕa ya sheŕia na polisi katika kulinda masuala ya watoto,” anaelezea naibu mwakilishi wa UNICEF nchini Ivoŕy Coast Chŕistina de Bŕuin.

Kwa sasa, watoto wachache wana fuŕsa ya kupata haki kutoka mfumo wa utoaji wa haki, ambao kwa pamoja na polisi walikuja kusimama wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi, wakati jeshi la Ivoŕy Coast na vikosi vya wapiganaji wa upinzani waliposababisha tishio la amani nchini.

“Rais Ouattaŕa na seŕikali yake wameshasema juu ya wasiwasi wao kuhusu haki za watoto, lakini itachukua muda mŕefu kutekeleza maamuzi mapya ya kiseŕa,” anasema de Bŕuin. Hadi wakati huo, maelfu ya ŕaia wa Ivoŕy Coast watabakia kuwa katika hali tete.

*Majina yalibadilishwa kulinda kutambuliwa kwa mtoto.