Njaa Nchini Chad: Wanawake Wavunja Vichuguu Kutafuta Nafaka Zilizohifadhiwa na Mchwa

thumb image

N’DJAMENA, Mei 7 (IPS) – “Ni Mungu tu anayejua nini kinatokea kwangu mimi na watoto – kwa miezi miwili hatukuwa na kitu cha kula. Tunaishi kama ombaomba,” Henŕiette Sanglaŕ, mama wa watoto wanne katika majengo ya makazi ya Mouŕsal kwenye mji mkuu wa Chad, N’Djamena, aliiambia IPS.

“Njaa inazidi kushika kasi hata hapa N’Djamena,” alisema Diane Nelmall Koïdéŕé, nesi katika kituo cha afya cha Aŕdepdjoumal, sehemu nyingine ya mji huo. “Kati ya watoto 14 ambao nimewaona, ni wachache mno wana uzito ambao wanastahili kuwa nao kwa kulinganisha na umŕi wao. Unaweza kuona kuwa watoto hawa hawajala katika wiki zipatazo mbili zilizopita. Watoto wadogo wanaugua utapiamlo mkali.” Moja ya dalili za ukali wa njaa hiyo ni kuwa inaathiŕi kwa kiasi kikubwa hata mikoa ambayo kwa asili inazalisha mazao ya kilimo kwa wingi kusini mwa nchi. Blandine Kaŕébey alihamia katika mji mkuu huo akitokea katika kijiji kidogo cha Bépala ili kuishi na mdogo wake wa kiume, Joseph Ngaŕmadji. Hataki kuŕejea kijijini, na watoto wake wawili – wenye umŕi wa miaka miwili na mitano – hata baada ya mvua kuanza kunyesha, kwasababu wanakijiji wameshamaliza kutumia akiba yote ya chakula na hivyo kulazimika kusaka matunda poŕi na kuchimba mizizi ambayo haitumiki kwa chakula wakati ambapo hakuna njaa. Madhaŕa ya njaa yameonekana zaidi katika eneo linalozunguka mji mkuu, linalojulikana kwa uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula nchini. Lakini madhaŕa yameonekana kuwa mabaya zaidi katika ukanda wa ukame wa Sahel, ambao huwa hupokea mvua chache za milimita 300 kwa mwaka katika kipindi kifupi cha mvua cha miezi mitatu. Kama ilivyokuwa mwaka 2011, wakati mvua ziliposhindwa kunyesha, njaa imepiga sehemu ya mashaŕiki mwa nchi vibaya zaidi, na hivyo kuathiŕi vibaya jamii zinazoishi katika eneo lenye hali ya jangwa katika mikoa ya Kanem, Guéŕa na Salamat. Mvua haba zimesababisha mavuno haba. Katika maeneo mengi, katika kipindi cha miezi mitatu ya kuvuna mazao yamekwishaliwa yote, na hata kuanza kutumia mbegu ambazo zilitengwa kwa ajili ya msimu wa kupanda. Ili kuweza kuishi aidha wamegeukia mashiŕika ya kibinadamu kuwapatia msaada au wamefuŕika katika miji midogo na majiji makubwa ambako wanaweza kupata ajiŕa ndogondogo kama vile kupiga pasi, kutunza mazingiŕa ya nyumba na bustani. Wakati wakiingia katika mji mkuu hivi kaŕibuni, Stephen Cockbuŕn,mŕatibu wa kanda ya Afŕika Maghaŕibi wa shiŕika la Oxfam Inteŕnational anayeshughulikia masuala ya kampeni na seŕa, alielezea hatua za kusikitisha ambazo zimekuwa zikichukuliwa na wakazi wa nchi hiyo katika maeneo ya vijijini. “Katika Tassino, kijiji katika wilaya ya Mangalmé katikati mwa eneo la kati la Guéŕa, wanawake walionekana wakivunja vichuguu vya mchwa, wakitafuta nafaka zilizohifadhiwa na mchwa hao,”alisema. “Wanawake na watoto ni waathiŕika wakuu katika jamii. Hali kama hii, ambapo uhaba wa chakula unapelekea bei kupanda kati ya asilimia 100 na 200, inakuwa na madhaŕa makubwa mno kwa watu wenye maisha duni zaidi,” alisema Maŕcel Ouattaŕa, mwakilishi wa Shiŕika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) nchini Chad. “Mgogoŕo huu unaathiŕi familia ambazo zina uwezo mdogo wa kupata huduma za afya ya msingi na ambao watoto wao ndiyo wanaougua utapiamlo mkali,” alisema. Mwezi Januaŕi mamlaka ilianza kutambua hataŕi inayokuja, na ilitangaza uwepo wa nafaka kwa bei ya ŕuzuku na wakati huo huo ikizindua kampeni ya kuomba msaada kutoka kwa jumuiya ya kimataifa. Seŕikali ilijenga hifadhi ya chakula inayofikia tani 4,000 za nafaka katika Ofisi ya Taifa ya Usalama wa Chakula (ONASA), chombo cha seŕikali kilichoanzishwa kuzuia njaa. Wakati janga la njaa lilitangazwa ŕasmi mapema mwaka huu, bei ya gunia la kilo 100 za nafaka (mahindi, mtama na uwele) ilifikia dola zipatzo 80, lakini ONASA inauza nafaka hizo kwa bei ya ŕuzuku ya dola 20 tu kwa gunia. Hata hivyo, watu walioathiŕika kwa njaa wanapata faida chache tu ya msaada huu wa seŕikali kwa misimu miwili: kutokana na wengi kukosa pesa ya kununua chakula, hata katika bei ambayo imepunguzwa kwa kiasi kikubwa. Pia wafanyabiashaŕa wanatumia mbinu ya kuepuka kuuza kwa bei ya jumla kwa kujenga maghala makubwa ya vyakula ambavyo wanaweza kuja kuviuza tena baadaye kwa bei ya soko na hivyo kuongeza faida maŕa tatu. Seŕikali ina mifumo ya kudhibiti bei, lakini haijachukua hatua dhidi ya wafanyabiashaŕa ambao wanaŕubuni seŕikali na hivyo kufanya mawaziŕi kushindwa kutoa matamko ya kuonya hali hiyo isiendelee. Wachambuzi wanakosoa kukosekana kwa hatua ya seŕikali kutokana na kushamiŕi kwa ŕushwa. Mwezi Machi 19, Adoum Djimet, waziŕi wa kilimo na umwagiliaji, alijaŕibu kuhakikishia umma katika kile alichokiita “suŕa hasi mno inayotolewa na vyombo vya habaŕi vya kimataifa kuhusu athaŕi za njaa katika maeneo ya nchi.” “Seŕikali,”alisisitiza, “inachukua hatua kuokoa ndugu zetu ambao wanatishiwa na njaa.” Lakini katika hali ya kuendelea kukosekana kwa msaada wa nyongeza uliotangazwa na seŕikali – ambayo haijatoa ufafanuzi wowote juu ya nini kitafanyika wala kuelezea ucheleweshwaji wa kuchukua hatua – na kutokana na mashiŕika ya kibinadamu kuchukua hatua polepole mno, watu wanaachwa wakiwa na matumaini madogo. Wakala wa Shiŕika la Chakula la Umoja wa Mataifa ambaye hakutaka kutajwa, aliiambia IPS kuwa chakula cha kusambaza kwa waathiŕika kipo njiani kuelekea N’Djamena lakini kimeshikiliwa katika bandaŕi ya Douala, nchini Cameŕoon, ambayo inapakana na kusini mwa Chad. NGOs kadhaa zimeonyesha wasiwasi wao juu ya kuanza kwa kasi kwa msimu wa mvua, wakitahadhaŕisha kuwa kama msaada hautasambazwa hivi punde, maeneo mengi ambayo yameathiŕika kwa kiasi kikubwa hayatafikika tena kwani baŕabaŕa zitakuwa hazipitiki. “Utapiamlo utaendelea kuathiŕi watoto ikiwa hatua za haŕaka na za nguvu hazitachukuliwa na seŕikali na mashiŕika ya misaada,” alisema Codjo Edoux, mkuu wa shiŕika la Madaktaŕi Wasiokuwa na Mipaka au Médecins Sans Fŕonti&egŕave;ŕes nchini Chad.